Wakili wa Mbowe ameshinda pingamizi lake lakini kwa sababu halikuwa na madhara yoyote limetupwa. Jaji awapongeza mawakili kwa umakini!

Logic inakataa ruling ya Jaji. Kama kifungu cha citation hakipo, ushahidi usiingizwe, uwe na madhara au usiwe na madhara. Kama hauna madhara, unauingiza wa nini wakati sheria imegoma?

Logic imekataa hapo. Jaji huyu ni sawa na wale.
Kabisa.Yeye mwenyewe jaji amekubali sasa anapinga nini tena
 
Haya ni maajabu kama kitu kiko kinyume na sheria mahakama ambayo kazi yake ni kutafsiri sheria inakubali kabisa kwamba jambo hilo liko kinyume na sheria lakini eti halina madhara sasa ni nini maana ya mahakama?
Ni ujuha wa kiwango cha lami. Kama kusingekuwa na madhara basi hao wabambikaji wasingeomba kuuwakilisha.
 
Hivi hakuna namna ya kumkataa huyo mwana CCM anayejitambulisha kama Jaji?
 
Kwenye kesi ya Mbowe mahakama imegeuka badala ya kutafsiri sheria sasa imekuwa inarekebisha sheria, kitendo cha kutafsiri japo mmeshinda pingamizi lenu lakini hata mkishinda halitakuwa na maana, maana yake jaji ameona hiyo sheria ya wrong citation ina mapungufu akaamua kuirekebisha hapo mahakamani.

Naona lile bunge halina kazi tena, kama linatunga sheria zenye makosa halifanyi kazi yake kwa umakini, bora livunjwe tu waende kulima.
hii kesi inamvuruga hangaya
 
Hii kesi hukumu yake imeshaandaliwa tayari ipo kwenye flash ya Jaji, ni suala la muda tu
Mabingwa wa udukuzi wa Mtandaoni sijui bado wamelala... ingefaa waidukue hiyo flash halafu wamwage contents zake kwa style ya wiki leak na Panama papers...ndicho kilichobaki kwa sasa
 
Na kama ushahidi hauna madhara, wanausoma kwa sababu gani au Siku hizi mahakamani pia ni sehemu mojawapo ya kuwachafua watu na ushadi usio na madhara? Ya nini usomwe ?
 
Hajitambui huyo Jaji anatembea na hukumu toka kwa Chifu Hang ya na kesi yake aliyombambikia Mbowe.



Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV ni kwamba mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe wameshinda pingamizi lao ila kwa sababu hawakuonyesha wataathirika vipi hati hizo zikipokelewa Jaji amelitupa pingamizi hilo.

Hata hivyo Jaji amewapongeza mawakili hao kwa umakini waliouonyesha kwani vifungu hivyo vimekuwa vikileta utata mahakamani mara kwa mara.

Source: ITV habari
 
Back
Top Bottom