Wakili wa Mbowe ameshinda pingamizi lake lakini kwa sababu halikuwa na madhara yoyote limetupwa. Jaji awapongeza mawakili kwa umakini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV ni kwamba mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe wameshinda pingamizi lao ila kwa sababu hawakuonyesha wataathirika vipi hati hizo zikipokelewa Jaji amelitupa pingamizi hilo.

Hata hivyo Jaji amewapongeza mawakili hao kwa umakini waliouonyesha kwani vifungu hivyo vimekuwa vikileta utata mahakamani mara kwa mara.

Source: ITV habari
 
Ndondocha hawawezi ona madhara , wana shupaza tu shingo ili watu waathilike, labda angekumbushwa doctrine of pre emptive strike ndio angekubali madhara si lazima yaonekane moja kwa moja... Tiganga nawenzake wanakubali kwamba vifungu vimekosewa sasa ya nini tena kuthibitisha madhara, si ni ujuha huu...Tiganga ajitathmini kwa kweli na mahakama yake hiyo...Pathetic
 
Logic inakataa ruling ya Jaji. Kama kifungu cha citation hakipo, ushahidi usiingizwe, uwe na madhara au usiwe na madhara. Kama hauna madhara, unauingiza wa nini wakati sheria imegoma?

Logic imekataa hapo. Jaji huyu ni sawa na wale.
 
Ndondocha hawawezi ona madhara , wana shupaza tu shingo ili watu waathilike, labda angekumbushwa doctrine of pre emptive strike ndio angekubali madhara si lazima yaonekane moja kwa moja... Tiganga nawenzake wanakubali kwamba vifungu vimekosewa sasa ya nini tena kuthibitisha madhara, si ni ujuha huu...Tiganga ajitathmini kwa kweli na mahakama yake hiyo...Pathetic
Haya ni maajabu kama kitu kiko kinyume na sheria mahakama ambayo kazi yake ni kutafsiri sheria inakubali kabisa kwamba jambo hilo liko kinyume na sheria lakini eti halina madhara sasa ni nini maana ya mahakama?
 
Kwenye kesi ya Mbowe mahakama imegeuka badala ya kutafsiri sheria sasa imekuwa inarekebisha sheria, kitendo cha kutafsiri japo mmeshinda pingamizi lenu lakini hata mkishinda halitakuwa na maana, maana yake jaji ameona hiyo sheria ya wrong citation ina mapungufu akaamua kuirekebisha hapo mahakamani.

Naona lile bunge halina kazi tena, kama linatunga sheria zenye makosa halifanyi kazi yake kwa umakini, bora livunjwe tu waende kulima.
 
Logic inakataa ruling ya Jaji. Kama kifungu cha citation hakipo, ushahidi usiingizwe, uwe na madhara au usiwe na madhara. Kama hauna madhara, unauingiza wa nini wakati sheria imegoma?

Logic imekataa hapo. Jaji huyu ni sawa na wale.....
Jambo hili linaichafua sana mahakama yetu . Yaani wanakubali kwamba sheria hiyo hakuna halafu bado wanaikubali document... labda huko mbeleni ... kwa sasa huyo Tiganga anajipaka tu Kinyesi na laana za wafungwa wanaoteseka kwa maamuzi ya kijinga anayo fanya... ni Jaji wa ajabu sana huyu sijui katokea wapi huyu na mwalimu wake huko chuo chao alikuwa ni nani sijui? au labda ni jaji wa voda fasta.. ,
 
Kesi nyingi hushindwa kwa makosa ya tafsiri ya sheria (technicalities) rejea kesi ya uhaini dhidi ya Maalim Seif
Sasa huyu jaji anajitia hamnazo kupokea kielelezo kilicholetwa bila sheria yoyote hai.
Hahahaaaa.......eti Hamnazo?
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV ni kwamba mawakili wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe wameshinda pingamizi lao ila kwa sababu hawakuonyesha wataathirika vipi hati hizo zikipokelewa Jaji amelitupa pingamizi hilo.

Hata hivyo Jaji amewapongeza mawakili hao kwa umakini waliouonyesha kwani vifungu hivyo vimekuwa vikileta utata mahakamani mara kwa mara.

Source: ITV habari
Sina uhakika kama nimeelewa maana proceeding inaonesha kilichokuwa kinapingwa na Upande wa Utetezi kimetupiliwa mbali na mahakama na Hati ya Kukamata Mali imepokelewa mahakamani kama kielelezo. Labda nieleweshwe hapo.
 
Kesi nyingi hushindwa kwa makosa ya tafsiri ya sheria (technicalities) rejea kesi ya uhaini dhidi ya Maalim Seif
Sasa huyu jaji anajitia hamnazo kupokea kielelezo kilicholetwa bila sheria yoyote hai.
Mkuu, Nadhani kilichosemwa na jaji ni kwamba utetezi wameshindwa Kuonyesha kukosewa kwa sheria kumeathiri vipi haki za mteja wao. Mahakama inatafsiri sheria kwa kuangalia haki zaidi(unfortunately hili linafuatwa kwa upande wa mashtaka tu)

Binafsi nachelea kuishuku hukumu ya leo si kama ilivyokuwa kwa mtukufu Siyani.
 
Sina uhakika kama nimeelewa maana proceeding inaonesha kilichokuwa kinapingwa na Upande wa Utetezi kimetupiliwa mbali na mahakama na Hati ya Kukamata Mali imepokelewa mahakamani kama kielelezo. Labda nieleweshwe hapo.
Jaji amekubaliana na Kibatala kuwa ni kweli hati ina makosa ya vifungu vya sheria vilivyotajwa.

Ila kwa sababu Kibatala hajasema kukosewa huko kutamuathiri vipi mteja wake anaamua kipokelewe na kufanyiwa marekebisho!
 
Back
Top Bottom