Wakili Medium Mwalle alazwa Mount Meru

Wakili Medium Mwalle alazwa Mount Meru

<font color="#800000"><font size="4"><b>Hivi Interpol wanajifanyia kazi kiholela tu Tanzania? Maana kila jambo sasa utasikia Interpol whats cooking?</b></font></font>
<br />
<br />
Serikali yetu haina meno hivyo wanaisaidia kuuma.
 
Wana JF,

Habari za kuaminika nilizo zipata toka Arusha Kuwa Adv. Mwale kalazwa Mt.Meru baaada ya kupata maumivu kwenye chumba cha mateso walikuwa wakitaka kujua hizo Billion ni za wateje gani, Na mpaka hivi sasa Adv.Mwale kashikilia msimamo huo huo kuwa ni pesa za mteja wake ila hajamtaja ni nani na zilikuja kwa ajili gani.

Watu wa Arusha walio karibu na Mt.Meru Hospital watupe zaidi details
Jetro, pamoja na ukweli kuwa torture ni sehemu ya interogation techniques za polisi wetu, sidhani kama wanaweza kutumia kwa wakili.
Pili kuna uhusiano maalum kati ya wakili na mteja wake ambao huitwa 'fidutiary relationship' ambapo sheria inamlinda wakili against any disclosure za wateja wake, mathalan mtu ameua kwenye fist degree murder, wakili wake atamshauri akanushe, ili kesi igeuke manslaughter kunusuru maisha yake. Hata kama mtuhumiwa atamweleza wakili wake ukweli halisi, kuwa kuwa alikusudia kuua, wakili atapindishi kuwa ni kaua bila kukusudia na sheria inamlinda wakili huyo.

Baada ya September 11, US wametushinikiza kuipitisha anti terrorisim act, na miongoni mwa vipengele hivyo, mabenki yamelazimishwa kutoa taarifa kitengo FIU cha BOT mara waonapo any suspicious transactions. Wakili Mwale, has the right to keep the comfidentiality of his clients, na serikali haina uwezo kuhoji hilo, bali anatakiwa kuiridhisha FIU ya BOT in compliance with terrorism act, ili wajiridhishe sio money laundering, au fedha za Al Qaeda au Al-Shababi oparations!.

Naamini Mwale, atakuwa anaumwa tuu kama mtu mwingine yoyote anavyoweza kuugua, hili la kuteswa, nasisitiza no!.

Pia nitamuomba mleta mada, akithibitisha hakuteswa, aache kuidramatize hii issue ionekane kubwa!, kosa la Mwale ni kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha, ni kama Chenge tuu, kosa lake kuziweka off shore ya Jersey yenye access ya Waingereza, wenzao waliodeposit kwenye Swiss acconts, they are all safe!.
 
Kwani wamemuona mwalle peke yake tu??? Mbona wengi wana mabillions ya shilling na hawaulizwi???? acheni kumuonea mtu wa watu,hata kama kapata kiujanjaujanja sio peke yake kamateni na wengine zaidi ni kutoka kwenu magamba......
 
it is really embarrasing to read some of the views reported herein, kwa mfano tu unasema WAKILI MWALE ALIKUA ANAHONGA KESI NA NDIO MAANA ALIKUA AKISHINDA KESI, haya mambo mbona hamkuyasema siku zote na iwe leo? Sabaabu kubwa ya watu kudharau hii jamii forum na taarifa zinazoolewa humu ndani ni kwakua taarifa nyingi zinazotolewa zinakua sio za kweli,zenye kupandikiza chuki, sio za kuchunguzwa na vinginevyo, ni nani aneyeweza simama leo hii na kudhibitisha kua alishawahi kuhonga? Anabillion 40 kwenye account yake? Na n.k, mi nadhani wakili yoyote yule jukumu lake linaishia kwenye ku draw document tu, he/she can not go beyond that,swala la yeye kujua nia na dhumuni la kmpuni iliyofunguliwa sio la kwake, mimi nadhani mzigo huu wangekua nao brella baada ya kuutwisha kwa mawakili. Na hata kwenye ANT MONEY LOUNDERING ACT bado inamapungufu mengi, kwa mfano tu, the phrase " ought to have known" ni phrase ambayo hua ina mtwisha wakili mzigo mkubwa sana in the sense that he is supposed to go beyond human neture to become aware with people he introduce to the bank vide bank introduction letters, memarts and the like, worse enough, WAKILI MWALE HAKUWAHI KUIBA HELA YA MTU HATA HIYO AMOUNT INAYOSEMEKANA ANAMILIKI HAIPO KWENYE ACCOUNT YA KAMPUNI INAYOTILIWA MASHAKA ACHILIA MBALI ACOUNT YAKE MWENYEWE, NI NANI HASA MLALAMIKAJI KWENYE KESI HIYO? AMBAYE KWA MFANO TU ANALAAMIKA HIZO HELA ZIMEIBIWA KWAKE AMA KWENYE ACCOUNT YAKE, ni vyema before we commentt on anything whatsoever TUKAYAONJA MANENO YETU KABLA YA KUYAONGEA, si vyema , kupandikiza chuki ama kuongea kwa ushabiki, ni faida gani hasa unayopata kwa mfano tu kumjengea mtu maneno ambayo sio ya kweli? Finally kama unajua unachokiandika ni kwa ajili ya chuki binafsi( nina uhakika hua tuna jua pale tunapofanya hivyo) elewa wazi kua KAMA UNAMCHUKIA MTU HUA UNADHIHIRISHA YEYE NI MKALI KULIKO WEWE"
 
Habari imekaa kiumbea alafu Jamaa anajiaminisha kwa wana JF eti! Habari ya kuaminika , hiyo siyo ya kuaminika ni tetesi coz wewe kama wewe hujathibitisha hilo na wala hujaongea na madaktari wala kumwona
 
it is really embarrasing to read some of the views reported herein, kwa mfano tu unasema WAKILI MWALE ALIKUA ANAHONGA KESI NA NDIO MAANA ALIKUA AKISHINDA KESI, haya mambo mbona hamkuyasema siku zote na iwe leo? Sabaabu kubwa ya watu kudharau hii jamii forum na taarifa zinazoolewa humu ndani ni kwakua taarifa nyingi zinazotolewa zinakua sio za kweli,zenye kupandikiza chuki, sio za kuchunguzwa na vinginevyo, ni nani aneyeweza simama leo hii na kudhibitisha kua alishawahi kuhonga? Anabillion 40 kwenye account yake? Na n.k, mi nadhani wakili yoyote yule jukumu lake linaishia kwenye ku draw document tu, he/she can not go beyond that,swala la yeye kujua nia na dhumuni la kmpuni iliyofunguliwa sio la kwake, mimi nadhani mzigo huu wangekua nao brella baada ya kuutwisha kwa mawakili. Na hata kwenye ANT MONEY LOUNDERING ACT bado inamapungufu mengi, kwa mfano tu, the phrase &quot; ought to have known&quot; ni phrase ambayo hua ina mtwisha wakili mzigo mkubwa sana in the sense that he is supposed to go beyond human neture to become aware with people he introduce to the bank vide bank introduction letters, memarts and the like, worse enough, WAKILI MWALE HAKUWAHI KUIBA HELA YA MTU HATA HIYO AMOUNT INAYOSEMEKANA ANAMILIKI HAIPO KWENYE ACCOUNT YA KAMPUNI INAYOTILIWA MASHAKA ACHILIA MBALI ACOUNT YAKE MWENYEWE, NI NANI HASA MLALAMIKAJI KWENYE KESI HIYO? AMBAYE KWA MFANO TU ANALAAMIKA HIZO HELA ZIMEIBIWA KWAKE AMA KWENYE ACCOUNT YAKE, ni vyema before we commentt on anything whatsoever TUKAYAONJA MANENO YETU KABLA YA KUYAONGEA, si vyema , kupandikiza chuki ama kuongea kwa ushabiki, ni faida gani hasa unayopata kwa mfano tu kumjengea mtu maneno ambayo sio ya kweli? Finally kama unajua unachokiandika ni kwa ajili ya chuki binafsi( nina uhakika hua tuna jua pale tunapofanya hivyo) elewa wazi kua KAMA UNAMCHUKIA MTU HUA UNADHIHIRISHA YEYE NI MKALI KULIKO WEWE&quot;
<br />
<br />
Hakika hili tunatakiwa tulielewe vyema kabla ya kukurupuka kwa chuki binafsi.
 
Kwani wamemuona mwalle peke yake tu??? Mbona wengi wana mabillions ya shilling na hawaulizwi???? acheni kumuonea mtu wa watu,hata kama kapata kiujanjaujanja sio peke yake kamateni na wengine zaidi ni kutoka kwenu magamba......
<br />
<br />

Unajua wajinga wengi hawakufurahi sana Kuona Nyari katoka, walihisi mwhakimu wamehongwa, pia watu wanaojiona vigogo wa Arusha na ambao ni maswahiba wa wakubwa huwa hawapendi kuona matanuzi ya Mwale, pia tujue pia habari inaweza kuchochewa pia na watu maalum kwa makusudi maalum. tz kila jambo lawezekana.
Tusimchukie mtu kwa mafanikio yake jamani.
 
siamini kama polisi wanaweza kumtesa mwanasheria maarufu hivyo huku ushahidi wote wanao....................hii ni kesi ya ughaidi na money laundering...............................ni vigumu kuthibitisha ugaidi lakini money laundering is a straight forward case.............
 
Pili kuna uhusiano maalum kati ya wakili na mteja wake ambao huitwa 'fidutiary relationship' ambapo sheria inamlinda wakili against any disclosure za wateja wake, mathalan mtu ameua kwenye fist degree murder, wakili wake atamshauri akanushe, ili kesi igeuke manslaughter kunusuru maisha yake. Hata kama mtuhumiwa atamweleza wakili wake ukweli halisi, kuwa kuwa alikusudia kuua, wakili atapindishi kuwa ni kaua bila kukusudia na sheria inamlinda wakili huyo.
Kaka, habari za mida hii.

Naomba unitajie kitabu, au jina la kozi inayofundisha hayo maudhui ya "fidutiary relationship", au jina la Mwalimu na mahala uliposoma, au sheria ya Bunge au legal precedent au chanzo kingine chochote chini ya jua na juu ya vilindi vya bahari za dunia hii, kinachofundisha kwamba wakili anatakiwa amsemee mteja uongo katika mazingira kama uliyotolea mfano, kwamba mtuhumiwa kakiri kwa wakili kwamba aliua kwa kukusudia na ni first degree murder, na wakili atatakiwa akaseme uongo mahakamani kwamba mteja hakukusudia, ili "kupindisha" kesi kuwa manslaughter.
 
Wana JF,

Habari za kuaminika nilizo zipata toka Arusha Kuwa Adv. Mwale kalazwa Mt.Meru baaada ya kupata maumivu kwenye chumba cha mateso walikuwa wakitaka kujua hizo Billion ni za wateje gani, Na mpaka hivi sasa Adv.Mwale kashikilia msimamo huo huo kuwa ni pesa za mteja wake ila hajamtaja ni nani na zilikuja kwa ajili gani.

Watu wa Arusha walio karibu na Mt.Meru Hospital watupe zaidi details





=======

Ni lazima aeleze ni kwa ajli gani fedha yote hii inaingizwa nchini!! Ni kwa ajili ya kuwalipa akina nani? Wafanye nini?
 
Inawezekana magamba wamehisi anasaidia CDM,Pesa zake ni ndogo magamba wana mahela ya kufa mtu,ya huendeshea nchi,mbona hawahojiwi wametoa wapi?Mkono vipi?RA?EL? na wengine wengi tu.
 
kalazwa kwa sababu ya presha au maumivu ya kudundwa na polisi?.
ila jamani kuwekewa 18 billion as a single transaction inatia shaka. yawezekana ni pesa halali lakini mwenye wajibu wa kuthibitisha ni mwale
kwamba hayo ni malipo ya kazi gani. it a highly suspicious transaction, na kwa mujibu wa sheria ya pesa haramu (money laundering) lazima taarifa ya pesa kama hizo zitolewe taarifa. (STR- Suspicious Transaction Reporting).
 
Jetro, pamoja na ukweli kuwa torture ni sehemu ya interogation techniques za polisi wetu, sidhani kama wanaweza kutumia kwa wakili.
Pili kuna uhusiano maalum kati ya wakili na mteja wake ambao huitwa 'fidutiary relationship' ambapo sheria inamlinda wakili against any disclosure za wateja wake, mathalan mtu ameua kwenye fist degree murder, wakili wake atamshauri akanushe, ili kesi igeuke manslaughter kunusuru maisha yake. Hata kama mtuhumiwa atamweleza wakili wake ukweli halisi, kuwa kuwa alikusudia kuua, wakili atapindishi kuwa ni kaua bila kukusudia na sheria inamlinda wakili huyo.

Baada ya September 11, US wametushinikiza kuipitisha anti terrorisim act, na miongoni mwa vipengele hivyo, mabenki yamelazimishwa kutoa taarifa kitengo FIU cha BOT mara waonapo any suspicious transactions. Wakili Mwale, has the right to keep the comfidentiality of his clients, na serikali haina uwezo kuhoji hilo, bali anatakiwa kuiridhisha FIU ya BOT in compliance with terrorism act, ili wajiridhishe sio money laundering, au fedha za Al Qaeda au Al-Shababi oparations!.

Naamini Mwale, atakuwa anaumwa tuu kama mtu mwingine yoyote anavyoweza kuugua, hili la kuteswa, nasisitiza no!.

Pia nitamuomba mleta mada, akithibitisha hakuteswa, aache kuidramatize hii issue ionekane kubwa!, kosa la Mwale ni kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha, ni kama Chenge tuu, kosa lake kuziweka off shore ya Jersey yenye access ya Waingereza, wenzao waliodeposit kwenye Swiss acconts, they are all safe!.

Unataka kusema hizo za Chenge huko Jersey ndio zina maelezo? hujaongea hapa ingawa unajitahidi kutete kisichoeleweka; kama mtoa taarifa alivyosema kama wewe unavyopinga hata wewe hauna ushahidi kama hajateshwa unatumia hisia zako binafsi, ambazo haziko bayana.

Sijaona kinachokusukuma kubisha zaidi ya kuwa labda wewe ni mmoja wa watesaji huko Polisi.
 
kalazwa kwa sababu ya presha au maumivu ya kudundwa na polisi?.
ila jamani kuwekewa 18 billion as a single transaction inatia shaka. yawezekana ni pesa halali lakini mwenye wajibu wa kuthibitisha ni mwale
kwamba hayo ni malipo ya kazi gani. it a highly suspicious transaction, na kwa mujibu wa sheria ya pesa haramu (money laundering) lazima taarifa ya pesa kama hizo zitolewe taarifa. (STR- Suspicious Transaction Reporting).

We upo usingizini amka!
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Polisi wataka Magereza wamlinde wakili Mwale [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 18 August 2011 22:15 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Peter Saramba, Arusha
JESHI la Polisi limeomba kujivua jukumu la kumlinda hospitalini alikolazwa wakili maarufu nchini, Medium Mwale anayekabiliwa na mashtaka 13 yakiwamo ya uhujumu uchumi, kugushi na kujipatia fedha kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye alisema jana kwa njia simu kuwa tayari ofisi yake imeandika barua kwenda Idara ya Jeshi la Magereza kuomba kukabidhi jukumu la ulinzi la mshtakiwa huyo kwenye idara hiyo baada ya taratibu za kumsomea mashtaka kukamilika juzi.

"Tayari tumewaandikia wenzetu wa magereza kuomba kuwakabidhi mtuhumiwa kwa sababu kisheria jukumu la polisi kumlinda mtuhumiwa linaishia pale anapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka. Kwa sababu hilo limeshafanika na mtuhumiwa kunyimwa dhamana kutokana na kosa lake kukosa dhamani lazima tumkabidhi Idara ya Magereza," alisema Andengenye.

Alisema hadi jana taratibu zilikuwa zinaendelea na alitegemea kumkabidhi mtuhumiwa huyo magereza ili polisi wanaomlinda wabadilishane na wale wa Idara ya Magereza.Juzi Wakili Mwale, alisomewa upya mashtaka 13 yakiwamo ya kuhujumu uchumi, kugushi nyaraka na kujipatia fedha haramu zaidi ya Sh18 bilioni.

Mwale alisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Fredrick Manyanda akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha alikopelekwa siku kadhaa zilizopita baada ya kujisikia vibaya akiwa mikononi mwa polisi alikorejeshwa baada ya mahakama kukataa kupokea hati ya awali iliyokuwa na makosa ya kisheria.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kwa siku tofauti, mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa kuhamisha fedha hizo kwenda kampuni tofauti na kuzitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Oliva Green, Nyamao Mbeche Hollo, Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John H. Adam na Mosoto O.Haye.

Alidai kuwa mshtakiwa alikuwa akihamisha fedha hizo kutoka kampuni moja kwenda nyingine hadi kufikia kwenye akaunti yake na kujipatia fedha hizo. Wakili Mwale aliyejizolea sifa kwa kuendesha na kushinda kesi kubwa kubwa nchini alikana mashtaka yake akiwa kitandani ndani ya chumba kilichojaa askari polisi wenye sare na waliovalia kiraia pamoja na maofisa kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 31, mwaka huu na huku mshtakiwa akiendelea kuwa chini ya ulinzi kutokana mashtaka ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Hatimaye wakili Mwale akabidhiwa Magereza [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 19 August 2011 20:13 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Peter Saramba, Arusha
HATIMAYE wakili maarufu nchini, Mediam Mwale, anayekabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo uhujumu uchumi na kupatikana na fedha haramu zaidi ya Sh18 bilioni, amekabidhiwa idara ya magereza baada ya kunyimwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Habari zilizopatikana kutoka polisi na magereza mkoani hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, zinadai mtuhumiwa huyo alipelekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, nje kidogo ya Manispaa juzi baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.Baada ya kukamilisha taratibu hizo, Mwale alichukuliwa na kupelekwa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha lililopo Kisongo hadi kesi yake itakapotajwa Agosti 31, mwaka huu.

Wakili Mwale alisomewa mashtaka 13 akiwa wodini Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua akiwa mikononi mwa polisi, baada ya mahakama kukataa kupokea hati ya awali mashtaka iliyokuwa na makosa kisheria.

Mwale anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena Agosti 31, mwaka huu kesi yake itakapotajwa, anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali na kufanikiwa kujipatia kiasi hicho kikubwa cha fedha, kinyume cha sheria kati ya Januari mwaka jana hadi Julai mwaka huu.

Hati ya mashtaka inataja kosa la kwanza hadi la tatu kuwa, ni kughushi na kuorodhesha majina na kampuni sita zilizotumiwa na mshtakiwa kuhamishia fedha hizo kwa nyakati tofauti kuwa, ni Oliva Green, Nyamao Mbeche Hollo, Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John H.Adam na Mosoto O. Hoye.
Mashtaka ya uhujumu uchumi yanadaiwa kutendeka kuanzia Februari 16, mwaka jana, Wakili Mwale anadaiwa kuhamisha Sh1.9 bilioni kati ya Kampuni ya Ogambo Chacha na Gregg Motachwa Mwita.

Shtaka la nne anadaiwa kuwa Machi 5, mwaka jana, alihamisha dola 200,000 za Marekani wakati shtaka la tano lililotendeka Machi 30, mwaka huohuo alihamisha dola 159,500, huku katika shtaka la sita anadaiwa kuhamisha dola 5,500 Septemba 27, mwaja jana.
Shtaka la saba anadaiwa kuwa, Novemba 2, mwaka jana alihamisha zaidi ya dola 1.2 milioni, kabla kufanya hivyo tena Desemba 21, mwaka huohuo alipohamisha dola 416,000 na kumalizia mwaka kwa kuhamisha dola 521,000 Desemba 24, 2010.

Januari 17, mwaka huu alihamisha dola 808,000 na Februari 9, alihamisha dola 527,000 kabla ya kukamilisha zoezi hilo Julai 13, mwaka huu kwa kuhamisha zaidi Sh300 milioni.

Katika hatua nyingine, mahakama imeamuru polisi kurejesha mali za mshtakiwa ikiwamo gari la kifahari aina ya BMW na simu ya kiganjani baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Charles Magesa, anayesikiliza shauri hilo kukubaliana na ombi la Wakili wa utetezi, Loomu Ojare kuwa hazijaorodheshwa kwenye hati ya mashtaka.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Haya mambo ya mawakili..balaa! Fikra ni kujilimbikizia mali tupu!
 
How can you put all that money in a bank account...that kind of money is better split into properties and shares. That's a way to keep the money rolling sio kulundika bank! Financial Intelligence Unit wapo kweli?
 
kitendo cha kusplit into properties and shares ndo money laundering yenyewe
 
Back
Top Bottom