DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata, ameonesha masikitiko yake kwa vyama vya siasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi licha ya kuwepo madai ya kukosekana kwa mabadiliko ya msingi katika mfumo wa uchaguzi nchini.
Akizungumza kupitia kipindi cha Maswali na Majibu kinachoendeshwa na mtangazaji Wilberforce Ngoto, Wakili Matata amesema msimamo wa “No Reforms, No Election” ulipaswa kuwa wa vyama vyote vya upinzani ili kulinda masilahi ya wananchi.
Amefafanua kuwa uchaguzi ni tendo takatifu ambapo wananchi huamua kumkabidhi mtu mmoja mamlaka ya kuwawakilisha, hivyo ni lazima uhakikishe haki na usawa. Hata hivyo, amesema vyama vilivyoshiriki vimesaliti msimamo huo, huku CHADEMA ikibaki imara kutoshiriki na kuapa kutumia njia halali kuhakikisha uchaguzi unazuiwa endapo mabadiliko hayatafanyika.