Wakili maarufu kukamatwa baada ya 'kupost' uharibufu kwenye kituo cha mwendekosi kwenye mitandao

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Hivi karibuni serikali ilionya watu kujichukulia hatua za kupiga picha za mnato au video katika uharibufu wowote unaofanyika katika miondombinu ya serikali i.e Majengo n.k jambo ambalo lilimtia hatiani mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu baada ya kusambaza picha za video na mnato akionyesha uharibifu mkubwa wa nyufa zilizoonekana hivi karibuni katika jengo mojawapo kati ya ya yale mabweni ya Magufuli pale chuo kikukuu na baadae serikali ikatoa ufafanuzi kuwa ile inaitwa 'Expansion joint' na sio uharibifu.

Kama haitoshi na kama waswahili wasemavyo kwamba kamwe sikio la kufa halisikii dawa. leo katika akaunti yake ya Instagram, Wakili maarufu hapa mkoani Arusha na kada wa wa TLP ambaye kwa sasa 'amehamishiwa' CCM amerusha picha inayoonyesha uharibufu mkubwa katika mojawapo ya vituo vya mabasi ya mwendo kasi kitu kinachopelekea mvua kuwanyeshea abiria wanapokuwa wanasubir usafiri.

Kutokana na kosa hilo ka kama ambavyo tulivyoshatangaziwa hapo awali tunategemea atatiwa nguvuni mda si mrefu kwa kosa kusambaza habari za uchochezi....
 
Mapandikizi ya ukawa yamenza kufanya kazi polepole tunakuambia tutaendelea kupandikiza hapo ccm hadi 2019 kisha wote kurudi ukswa na ndio hapo ccm 2020 mwisho wa kutesa na kutawala kibane.


FID Q wa magogoni nae akiande mairizi yake kiunoni


Swissme
 
Nashindwa kuelewa kabisa haya mambo.
Kwani kuonesha huo uharibifu kunaleta shida gani?
Na kama usipooneshwa hadharani, serikali itajuaje ili ichukue hatua haraka?
Na kam mambo hayo yakioneshwa nani anaathirika?

LAKINI mbona serikali inatuomba kushirikiana nayo katika kufichua uovu. Sasa inakuaje inabagua aina ya uovu?
 
Haya mambo maneno mengi huna hata ushahidi umeanza lini?

Nikirudi nikute picha na jina lake
 
Wanataka tureport habari za Ujambazii tu na kuonesha ushirikianoo ila sio kureport utumboo wao na kuukosoa.. shwain kabisaa..
 
Aaaah ndo ile video niliyoiona maji yakivuja kwenye kituo cha mwendokasiii....!
 
Hii nchi ukitaja tu uharibifu Basi unakamatwa. Wacha Kila kitu kiharibike, Sisi tubaki tu tunapiga makofi Kila tuonapo uharibifu
 
Yaani miundo mbinu inajengwa kwa kodi yako. Ikiharibika kaa kimya usitoe taarifa kwa walipa kodi wenzio
 
Back
Top Bottom