Wakili maarufu anadaiwa kuponza na ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakili maarufu anadaiwa kuponza na ushauri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Aug 8, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,011
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wakili maarufu anadaiwa kuponza na ushauri
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 07 August 2011 21:46 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwandishi Wetu
  IMEBAINIKA kukamatwa kwa wakili maarufu mkoani hapa na makachero wa polisi, kunatokana na ushauri wake wa kisheria aliotoa kwa wateja wake kuhusu utaratibu wa uanzishaji kampuni na kuwatambulisha benki kufungua akaunti.Akizungumza na gazeti hili jana, ofisa mmoja wa polisi alisema wakili huyo alitoa ushauri kwa wateja wake jinsi ya kuanzisha kampuni na aliwatambulisha benki ambako walifungua akaunti.

  “Kinachomfanya ashikiliwe polisi ni kwamba wanataka awaonyeshe wale wateja wake aliowatambulisha mpaka benki na yeye anadai hafahamu walipo,” alidai ofisa huyo.Taarifa za awali zilidai wakili huyo alikutwa na kiasi hicho kikubwa cha fedha katika akaunti yake na kwamba, alipokamatwa kwenye gari lake zilikutwa Sh20 milioni.

  Chanzo hicho cha habari kilipasha kuwa, akaunti ya kampuni hiyo aliyoshauri kufunguliwa ilikutwa na dola 500 za Marekani sawa Sh800,000, ambazo zilitumika kufungulia akaunti hiyo.Simu za wakili huyo zimekuwa hazipatikani tangu akamatwe na polisi Agosti 2, mwaka huu ingawa habari za uhakika zilisema aliachiwa kwa dhamana juzi jioni.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu taarifa za kukamatwa kwa wakili huyo, hakukiri wala kukataa zaidi ya kusema suala hilo liko ngazi za juu, hivyo hawezi kulizungumzia.
  “Kwa kweli hilo suala liko juu ya ngazi yangu, siwezi kulizungumzia chochote kwa sasa hadi nipate idhini kutoka kwa wakubwa wangu,” alisema Andengenye.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tawi la Arusha, Duncan Ooola, alikiri kukamatwa kwa wakili huyo na kwamba, walipofuatilia waliambiwa anachunguzwa na polisi.“Ni kweli wamemkamata Jumanne (wiki iliyopita), lakini sijui saa ngapi, tulikwenda polisi kujua chanzo walitwambia anachunguzwa, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kukupa,” alisema Ooola. [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,011
  Trophy Points: 280
  hivi huyu mwanasheria maarufu mbona hatajwi jina au hata magazeti yanamwogopa?
   
 3. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Maybe walipewa jina na vyanzo visivyothibitika...
   
 4. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alishatajwa jina mara kadhaa anaitwa Mwale...

  Tusubiri uchunguzi ukamilike tujue hiyo account ina issue gani, na hayo mabililioni ni ya nini
   
Loading...