Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,601
Leo, tarehe 17 Machi 2026, nimemtembelea Tundu Lissu katika Gereza Kuu la Ukonga kwa ajili ya mazungumzo ya kisheria kuhusu mwenendo wa kesi yake.
Hata hivyo, mazungumzo kati yangu na yeye yalifanyika katika mazingira yasiyozingatia faragha inayotakiwa kisheria, kinyume na Kanuni za Usimamizi wa Magereza za mwaka 1968, pamoja na Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa Kuhusu Wajibu wa Mawakili (UN Basic Principles on the Role of Lawyers) na Kanuni za Umoja wa Mataifa za Viwango vya Chini vya Usimamizi wa Wafungwa (Kanuni za Nelson Mandela) ambazo zinasisitiza kuwa mawasiliano kati ya wakili na mteja yanapaswa kuwa ya faragha.
Suala hili pia ameshalilalamikia mara kadhaa Mahakamani, ikiwemo wakati wa mwenendo wa ukabidhi na wakati wa usikilizwaji wa kesi ya uhaini katika Mahakama Kuu. Tarehe 24 Februari 2025, wakati wa kuahirishwa kwa kesi hiyo, alikumbushia Mahakama kuhusu suala hili, ambapo kiongozi wa Jopo la Majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Mhe. Jaji Nduguru, alieleza kuwa Mahakama imepokea hoja hiyo na kuwa hatua zingechukuliwa kupitia majaji wanaotembelea magereza.
Hata hivyo, Mhe. Lissu amesema hadi sasa hajaweza kutembelewa na jaji yeyote, hali inayoendelea kuathiri faragha ya mawasiliano kati yake na mawakili wake. Hivyo, ni muhimu hatua stahiki zichukuliwe ikiwa ni pamoja na majaji husika kumtembelea gerezani.
Paul Kisabo (Wakili)