Wakili Kimomogoro amuelimisha Nape

Wakili Kimomogoro amuelimisha Nape

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2007
Posts
869
Reaction score
239
• ASEMA KUHOJI KADI YA DK. SLAA NI KUJIDHALILISHA

WAKILI maarufu wa kujitegemea jijini Arusha, Method Kimomogoro, amesema hoja ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye kuhusu uhalali wa Dk. Willibrod Slaa kumiliki kadi ya CCM ni ya kijinga na yenye nia ya kujidhalilisha mwenyewe.

Kimomogoro ambaye pia ni wakili wa baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA katika kesi mbalimbali za kisiasa zinazowakabili kwenye mahakama za jijini humo, alisema kuwa amelazimika kutoa ufafanuzi wa kisheria ili kufuta ujinga unaoenezwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, wakili huyo alisema kuwa wote wanaoungana na Nape, kueneza hoja hiyo ni wajinga kwa vile kadi ya chama ni mali ya mwanachama tofauti na zilivyo kadi nyingine za taasisi kama benki ambapo ni mali ya benki.

Ufafanuzi huo wa kisheria unakuja siku chache tangu, Nape aibue hoja hiyo akiwa ziarani jijini Mwanza ambako alidai kuwa Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA, ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wanaoendelea kumiliki kadi za CCM na kulipia ada licha ya kuhama.

Hata hivyo, Dk. Slaa alijibu hoja hiyo na kumtaka Nape aache kupiga mayowe badala yake awaeleze wananchi serikali ya chama chake imefanya nini kuwaondolea umaskini unaowakabili.

Pia alikiri kuwa na kadi hiyo, lakini akakanusha kuilipia ada, akisema ni kinyume kwa mujibu wa sheria mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili, kwamba ameihifadhi kama mali yake ili iwe kumbukumbu kwa wajukuu zake.

Licha ya ufafanuzi huo, Nape bado ameendelea kueneza propaganda hiyo, huku akitambua wazi kuwa sharti mojawapo la Katiba ya CCM linabainisha kuwa uanachama wa mtu unakoma endapo atahamia chama kingine cha siasa.

Ni katika upotoshaji huo, wakili Kimomogoro alijitokeza kutoa ufafanuzi wa kisheria akisema, kadi ya CCM na hata vyama vingine ni mali ya mwanachama, hivyo anapohama anaweza kuipeleka popote atakapo na hata kuichoma moto akitaka.

"Wanaoibua hoja hii ni wajinga, tena inasikitisha sana kuona kiongozi na msemaji wa chama kama Nape ndiye anaibua ujinga huu, kama haelewi taratibu za chama chake alipaswa kufanya utafiti kwanza," alisema.

Kimomogoro alisema kuwa, kadi ya chama ni sawa na cheti cha kuzaliwa au cha ndoa, kwamba mtu anapokufa au ndoa yake kuvunjika hakuna anapoulizwa ama kutakiwa kurejesha vyeti hivyo maana ni mali yake.

"Kama wakina Nape wanataka Dk. Slaa na wengine walioondoka CCM wawarejeshee kadi zao, basi wabadili katiba yao na kuliweka kisheria kama ilivyo kwa kadi za mabenki ambazo huwa mali za benki husika," alisema.

Wakili huyo aliongeza kuwa, anachofanya Nape ni maajabu na hivyo wako watakaomtaka awaeleze kadi za CCM za hayati Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine waliofariki zimerejeshwa kwa nani kama ni mali ya chama.

Alisema kuwa, Nape anatakiwa kujikita kwenye mambo ya msingi ya kuendeleza chama chake na serikali wanayoiongoza, badala ya kuibua hoja za kijinga zisizo na tija kwa wananchi.
 
Nape hana hoja za kijinga tu bali za kipumbavuuu. Mbona yeye ana kadi ya chama chake cha jamii na hakuna anayemgusa? Kweli nyani haoni kundule na wanaomuunga mkono nadhani ni wale wale wenye mawazo mgando kama yeye.
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

Mkuu hoja ya kijinga ni hoja ya kijinga tu. Haijalishi hoja hiyo imetoka wapi, hata kama Nape ameitoa kwako au hata kama alikuja nayo mwenyewe, hiyo si hoyja. Hoja ni yaliyomo kwenye hoja yenyewe.

Lakini sikubaliani na wale wanaowakashifu waliotoa hoja hiyo na walioitangaza hoja hiyo. Cha muhimu ni kujibu hoja kwa hoja.

Kuna wana CCM wengi tu wana kadi za Chadema na hata wengine, na wanachadema wengi tu si SLaa peke yake wana kadi za CCM, muulize Mabere Marando....and his likes.

Let us look on bigger picture, tusiwe tunaangalia mambo ya kitoto.
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

kwa hiyo wewe ndio unastahili kuambiwa kuwa umeanzisha hoja ya kijinga na sio Nape? au basi wote kwa mujibu wa Kimomogoro mmeanzisha hoja ya kijinga kwa tafsiri nyingine nyie ni wajinga maana mtu aliye na akili hawezi kuanzisha hoja ya kijinga kama wewe na Nape!
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa
Kwa hiyo mjinga hapa ni wewe!
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

Ni kweli Makupa, huyu wakili anatakiwa akutafute wewe uliofichua hii kitu sio Nape...huyu wakili ndio mjinga anataka kupingana na ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hoja ya kijinga ni
hoja ya kijinga tu. Haijalishi hoja hiyo imetoka wapi, hata kama Nape
ameitoa kwako au hata kama alikuja nayo mwenyewe, hiyo si hoyja. Hoja ni
yaliyomo kwenye hoja yenyewe.

Lakini sikubaliani na wale wanaowakashifu waliotoa hoja hiyo na
walioitangaza hoja hiyo. Cha muhimu ni kujibu hoja kwa hoja.

Kuna wana CCM wengi tu wana kadi za Chadema na hata wengine, na
wanachadema wengi tu si SLaa peke yake wana kadi za CCM, muulize Mabere
Marando....and his likes.

Let us look on bigger picture, tusiwe tunaangalia mambo ya
kitoto.

Ivi kuna mtu kakataa kwamba si hoja ya kijinga? Tatizo ni majibu ya BABU
 
acheni kumwonea nape hoja ya kuwa dr slaa anamiliki kadi ya ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi makupa
jamaa alivyoanza kwa kusema wakili wakujitegemea nikavutiwa na mada ni kidhani atakuwa na jipye kusomasoma naona mwanachama wa chadema nikapata picha nzima ya anachotaka kuzungumza .sasa ushangae,thread kama hii iko humu ila mtu anaanzisha nyengine.kazi kwelikweli.
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

Makupa ni kati ya ID za Nape humu
 
Naona makupa anapigania 'cheo' cha ujinga na kwamba kwa lugha nyngne anaomba atambulike kwamba yeye ndo mjinga na sio bosi wake kama watu wengi wanavyofikiri!
 
  • Thanks
Reactions: KUN
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

Ujinga wa mtoa hoja na muenezaji unatofautiana.

unafikiri nani mjinga zaidi, aliyeitoa au aliyeichukua kama ilivyo na kuipigia debe?
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa.......

Kwa hiyo wewe ni mjinga kuliko huyo bosi wako Nape, pole sana.
 
Wa TZ .........wavivu wa kufikiri.......Kuna babu mmoja namfahama alienda kwenye mkutano wa CDM akanunua kadi akasema ataiunga mkono sana...lakini nilipomdadisi mbona sikumuona akirudisha kadi ya sisim akaniambia anaiweka kwa ajili ya ukumbusho wake
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa........

Kwa hiyo wewe ndiye mjinga usielewa katiba za vyama, na maana ya kuwa na kadi ya chama kama ni mali ya mtu binafsi. Ebu jiulize umefanikiwa nini katika kuleta hoja hii? Nape, JK, Mwakyembe, Sitta ni wanzilishi wa CCJ kadi za CCJ wamerudisha lini? Pia soma kwa ungalifu taarifa ya Kimomogolo kisheria. Wewe ulikurupuka kupata wachangiaji hapa JF kuisaidia CCM kuweni wavumilivu mnaponyolewa na wembe mlioutayarisha.

Juzi mmechukua kadi 200 za CDM kwenda kuzichakachukua ili mtazamwe na jicho la huruma, kwa tunaoelewa mchezo wenu mchafu tunawaangalia. Ebu muwe serious sasa siasa zimebadirika na watanzania wanajua kuchambua pumba na mchele.
 
Ni kweli Makupa, huyu wakili anatakiwa akutafute wewe uliofichua hii kitu sio Nape...huyu wakili ndio mjinga anataka kupingana na ukweli.

Ritz unaheshimika kwa hoja propaganda zinakupeleka kwingine kwa kujiingiza kundi la wajinga. Kwani wewe hujui kadi yako ya CCM ni mali yako haiwahusu Lumumba wala Chadema. Kama hujui huo ni ujinga.
 
Je hakuna mtu ambaye hafahamu kama Dr alikuwa ccm hapo kale?

Je alipo kuwa ccm alikuwa kama nani?

Je kama alikuwa mwanachama nini kilikuwa kinamtambulisha uwanachama wake?

Kumbe ni lazima kikatiba unapotoka kwenye chama kimoja kwenda kingine inakubidi urudishe kadi?

Mwisho kama Nape anasema Dr bado analipia kadi hiyo na fikiri kuna ushahidi tosha wa risiti za malipo hivyo atuletee copy ili tujue kati ya yeye na Dr nani ndio muongo


La msingi hapa tuna lazimika kuwajulisha kina Nape kuwa Tanzania hatuhitaji kujua nani ana kadi sisi tunahitaji uwajibikaji kwenye mambo ya msingi, watu hawasomi, watu wana kufa kwa njaa, hakuna ajira, hakuna uwezeshaji mahiri wa kujiajiri nk. Haya ndio mambo ya kuangalia na kutujulisha watanganyika si sera za umiliki wa kadi.
 
Wa TZ .........wavivu wa kufikiri.......Kuna babu mmoja namfahama alienda kwenye mkutano wa CDM akanunua kadi akasema ataiunga mkono sana...lakini nilipomdadisi mbona sikumuona akirudisha kadi ya sisim akaniambia anaiweka kwa ajili ya ukumbusho wake

Mtatunga hadithi nyingi kama ni ukumbusho yeye Slaa mbona hakuwaachia wengine nao wakae na ukumbusho?
 
Back
Top Bottom