Wakili Kimomogoro amuelimisha Nape

Wakili Kimomogoro amuelimisha Nape

Huyu Nape ni vuvuzela,hajawahi hata kuchaguliwa na mwananchi,amekuwa akiteuliwa kwa asante mjomba,yeye ni viti maalumu.
 
...kumbe ni dhambi kumiliki kadi ya chama kingine!
 
Mtatunga hadithi nyingi kama ni ukumbusho yeye Slaa mbona hakuwaachia wengine nao wakae na ukumbusho?

Na pia hakuwalazimisha kuzirudisha ili zichomwe moto, ni watu tu na mapenzi yao waliamua kuzichoma moto. Na ukichunguza kadi nyingi zinazorudishwa na kuchomwa moto ni hizi zilizotoka kipindi cha mafisadi, nyingi zimesainiwa na mafisadi, wakati zile za wakati wa Nyerere watu wengi wanazihifadhi kwa kumbukumbu ya uadilifu wake na wala sio kwa mapenzi yao kwa ccm ya sasa hivi.
 
Ujinga uliotopea zaidi kupingana na ukweli

Hakuna aliyepingana na ukweli. Dr amekiri kumiliki kadi na wala sio kuwa mwanachama wa gambaz. Kadi ya Dr ni miongoni mwa zile zilizotoka enzi zile chama kikimilikiwa na wakulima na wafanyakazi. Sio sasa hivi ambapo chama kimeshikiliwa na mijangili. Hata mimi ningekuwa na kadi ya enzi zile nisingeirudisha kamwe, lakini hizi za kina Nape ningeichoma bila kupepesa macho.
 
Jamaa kauliza swali la msingi kadi za Mahayi Nyerere, Sokoine, Kawawa, Omari Juma etz ziko wapi?
 
Kadi ni mali ya chama na ndio sababu chama husika kinaweza kukulazimisha urejeshe kadi yao!

tupe mstari katika katiba ya chama ambapo kuna kipengele cha mwanachama kurudisha kadi. Ndo maana hata simba na yanga wanapofanya mikutano yao ya wanachama sio wote wenye kadi wanaruhusiwa kuingia, ni lazima uwe hai (umeilipia ada ya uanachama) kinyume na hapo wewe si mwanachama hata kama unamiliki kadi na viongozi hawana jeuri ya kukunyang'anya kwasababu uliinunua kwa fedha yako
 
Wakili na yeye hamna kitu naye ni mjinga na ujinga unatofautiana,hebu tofautisha sheria na siasa.Anachosema Nape ile ni SIASA haiwezekani yeye Dr. apokee kadi za wengine wanaotoka CCM na hata hawaambii kwamba hizo ni mali zao hivyo wasirudishe sasa cha kushangaza mbona hawaambii.Huu nao ni upuuzi wa mwanasheria huyu anashindwa kutofautisha Siasa na Sheria.Tungekubali hoja yake endapo kama ipo kauli ya Dr. Slaa ya kuwaeleza wanaorudisha kadi za CCM waendelee kukaa nazo kwa vile ni mali yao.Huku ni kujidhalilisha kwa mwanataaluma.Anachofanya Nape ni kupiga Siasa ambapo kikawaida mtu anayehama chama anarusha kadi ukisema walikokufa warudishe sasa ye aliona wapi maiti inarudi?Hao waliokufa wamekufa wakiwa na itikadi hiyo tofauti na Dr.
Ulishamsikia wapi Dr analazimisha watu kurudisha kadi za ccm?? kama sio ushabiki wako wa kijinga, watu wenyewe wanaamua kuzikabidhi. Na tena ukichunguza kadi nyingi zinazorejeshwa ni zile zilizotolewa wakati wa Makamba, Nape, Mangula, et al. Lakini zile zilizotolewa wakati wa Nyerere watu wanazitunza kwaajili ya kumuenzi Mzee wetu. KEEP IT ON MIND
 
Ama kweli humu JF sisi tu wajinga yaani Makupa azue jambo basi mpaka kimomongoro aitwe hatuwezi jadili mabo mengine ila kukicha Nape, Kinana, Slaa, G. Lema CCM, CDM 2015 nimeamini
Jukwaa la Siasa lichanganywe na Jokes la sivyo tutaoana meno na sura kwa matusi
 
Last edited by a moderator:
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa

Uliianziasha wapi??? Coz vitu vingi tunavijadili kutokana na habari tunazo zipata kwa njia tofuti tofauti.... Sasa wewe uliianzisha wapi wakati watanzania wengi waloskia hawajajiunga na jf.... Mie mwenyewe niliiskiz kwanza kwenye redio... Na nape anaonewa nini.. Kadi huwa si ya mwanachama au?? Na uanachama unapokufa katiba inasemaje?? Wale wanaorudisha kadi kwenye majukwaa ya CDM huwa zinachomwa moto mbona hawaziulizii???? Nape tunataka maelezo na mipango mikakati ya nchi yetu sio huo ujinga unao eneza hautufaidishi chochote...
 
acheni kumwonea Nape hoja ya kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya Ccm ipo hapa jamvini tangu mwezi wa tisa na mwazilushi wa hii hoja ni mimi Makupa


Tatitizo sio nani kaanzisha hoja, Tatizo ni katiba ya chama cha mapinduzi, Katiba inasemaje umiliiki wa kadi ya chama cha mapinduzi hasa pale mwanachama anapoamua kuhamia chama kingine
? nafikiri Kimomogoro amefafanua vizuri!!Nape ameelewa !!!
 
Na pia hakuwalazimisha kuzirudisha ili zichomwe moto, ni watu tu na mapenzi yao waliamua kuzichoma moto. Na ukichunguza kadi nyingi zinazorudishwa na kuchomwa moto ni hizi zilizotoka kipindi cha mafisadi, nyingi zimesainiwa na mafisadi, wakati zile za wakati wa Nyerere watu wengi wanazihifadhi kwa kumbukumbu ya uadilifu wake na wala sio kwa mapenzi yao kwa ccm ya sasa hivi.

Unayo ushahidi wa hayo unayosema?
 
Hakuna aliyepingana na ukweli. Dr amekiri kumiliki kadi na wala sio kuwa mwanachama wa gambaz. Kadi ya Dr ni miongoni mwa zile zilizotoka enzi zile chama kikimilikiwa na wakulima na wafanyakazi. Sio sasa hivi ambapo chama kimeshikiliwa na mijangili. Hata mimi ningekuwa na kadi ya enzi zile nisingeirudisha kamwe, lakini hizi za kina Nape ningeichoma bila kupepesa macho.

maneno mepesi sana hayo kwa mtu mwenye fikra!
 
Yeye na akae nayo tunajua bado ana mapenzi na sisi
Haya ndiyo mapenzi yenyewe aliyonayo kwenu, mnahaha kujaribu kutumia vyombo vya dola kumhujumu Slaa na CDM

BY FRANK KIMBOY, 5 MARCH 2011
Chama Cha Mapinduzi (CCM) has urged the government to take legal measures against Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) allegedly for making incitement remarks in its ongoing public rallies in the Lake zone.
Speaking to reporters here yesterday the CCM publicity secretary Mr John Chiligati urged the government to have zero tolerance with Chadema leaders since the remarks they made during the public rallies are against the law.
"Anyone who dare to play with the countries' peace and tranquility should be punished according to the law...the government must have zero tolerance to anyone regardless of his/her party," he said.
Adding, "the police should understand that not only those who break banks are criminals but Chadema leaders are also criminals."
Mr Chiligati accused Chadema leaders especially its Secretary General Dr Wilbroad Slaa of inventing lies in their rallies with the aim of inciting wananchi to rise against President Jakaya Kikwete's administration.

For stance Mr Chiligati said in one of Chadema public rallies in the lake zone, Dr Slaa said that the government was to blame for the Gongo la Mboto bomb blasts because it turned down a request for money from TPDF which would have been used to destroy the out dated bombs prior to the blasts.
"Where did he find out that while even the investigating teams are still on the field, yet to announce the source of the blasts, Dr Slaa is inverting lies to the people," he said.
Mr Chiligati advised Chadema leaders to concentrate on selling their party policies and find out what led to their defeat in the last year election instead of making remarks that might destroy the country.
The CCM press conference came hot in the heels of similar criticism this week directed at Chadema by among others cabinet ministers Joseph Wassira and Sofia Simba who all rooted for stiff action to stop the ongoing public demonstrations led by the opposition party to protest rising costs of living and corruption.
Some opposition leaders like John Cheyo (UDP) and Augustine Mrema (TLP) have also joined in condemning Chadema in what appears like a planned assault against the party.
However, Chadema denied any accusations leveled against it and its officials are challenging those attacking the party to show proof to back their claims.

Hivyo ndivyo anavyojenga CCM!
 
Wewe Makupa ni janga kama walivyo magamba wengine. Kama umekwenda shule wewe ni matokeo ya shule za kata. jkadi ay uanachama ni mali ya mtu kama zilivyo nguo zako za ndani ukifika ukomo wake una halali ya kuitunza au kuitupa jalalani ama kuichoma. Unajitoa kimasomaso kuwa ndiye uliyeibua hoja mufilisi hii mkiwa na lengo la Dr (wa kweli sio kama hayo mabomu yenu!). Huyu hang'oki kwa sababu za kipuuzi kama hizo. hatuhitaji wanasheria na mawakili watueleze mambo yako wazi. rudini kuangalia mfumo wa elimu maana unawaathiri mpaka mnashindwa kuwaza vitu vidogo. akili zenu zifunguke kuwa hakuna mtu kung'oka mpaka kazi ya kugaragaza magamba iwe imemalizika. Mmekwisha eti maandamano Arusha, Mza, Mby kushinikiza Slaa aenguliwe. Katafute chakula ule naona hata njaa inachangia. Si bure: kwa magamba profesa anachangia hoja kama mtu wa kidato cha pili.
 
Je hakuna mtu ambaye hafahamu kama Dr alikuwa ccm hapo kale?

Je alipo kuwa ccm alikuwa kama nani?

Je kama alikuwa mwanachama nini kilikuwa kinamtambulisha uwanachama wake?

Kumbe ni lazima kikatiba unapotoka kwenye chama kimoja kwenda kingine inakubidi urudishe kadi?

Mwisho kama Nape anasema Dr bado analipia kadi hiyo na fikiri kuna ushahidi tosha wa risiti za malipo hivyo atuletee copy ili tujue kati ya yeye na Dr nani ndio muongo


La msingi hapa tuna lazimika kuwajulisha kina Nape kuwa Tanzania hatuhitaji kujua nani ana kadi sisi tunahitaji uwajibikaji kwenye mambo ya msingi, watu hawasomi, watu wana kufa kwa njaa, hakuna ajira, hakuna uwezeshaji mahiri wa kujiajiri nk. Haya ndio mambo ya kuangalia na kutujulisha watanganyika si sera za umiliki wa kadi.

Umenena mkuu, hawa kina Nape, Makupa, etc wajinga, badala ya kuisaidia serikali yao kuwaletea maendeleo wananchi, wamebaki na kazi ya kupika majungu na fitna...
 
• ASEMA KUHOJI KADI YA DK. SLAA NI KUJIDHALILISHA

WAKILI maarufu wa kujitegemea jijini Arusha, Method Kimomogoro, amesema hoja ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye kuhusu uhalali wa Dk. Willibrod Slaa kumiliki kadi ya CCM ni ya kijinga na yenye nia ya kujidhalilisha mwenyewe.

Kimomogoro ambaye pia ni wakili wa baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA katika kesi mbalimbali za kisiasa zinazowakabili kwenye mahakama za jijini humo, alisema kuwa amelazimika kutoa ufafanuzi wa kisheria ili kufuta ujinga unaoenezwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, wakili huyo alisema kuwa wote wanaoungana na Nape, kueneza hoja hiyo ni wajinga kwa vile kadi ya chama ni mali ya mwanachama tofauti na zilivyo kadi nyingine za taasisi kama benki ambapo ni mali ya benki.

Ufafanuzi huo wa kisheria unakuja siku chache tangu, Nape aibue hoja hiyo akiwa ziarani jijini Mwanza ambako alidai kuwa Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA, ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wanaoendelea kumiliki kadi za CCM na kulipia ada licha ya kuhama.

Hata hivyo, Dk. Slaa alijibu hoja hiyo na kumtaka Nape aache kupiga mayowe badala yake awaeleze wananchi serikali ya chama chake imefanya nini kuwaondolea umaskini unaowakabili.

Pia alikiri kuwa na kadi hiyo, lakini akakanusha kuilipia ada, akisema ni kinyume kwa mujibu wa sheria mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili, kwamba ameihifadhi kama mali yake ili iwe kumbukumbu kwa wajukuu zake.

Licha ya ufafanuzi huo, Nape bado ameendelea kueneza propaganda hiyo, huku akitambua wazi kuwa sharti mojawapo la Katiba ya CCM linabainisha kuwa uanachama wa mtu unakoma endapo atahamia chama kingine cha siasa.

Ni katika upotoshaji huo, wakili Kimomogoro alijitokeza kutoa ufafanuzi wa kisheria akisema, kadi ya CCM na hata vyama vingine ni mali ya mwanachama, hivyo anapohama anaweza kuipeleka popote atakapo na hata kuichoma moto akitaka.

“Wanaoibua hoja hii ni wajinga, tena inasikitisha sana kuona kiongozi na msemaji wa chama kama Nape ndiye anaibua ujinga huu, kama haelewi taratibu za chama chake alipaswa kufanya utafiti kwanza,” alisema.

Kimomogoro alisema kuwa, kadi ya chama ni sawa na cheti cha kuzaliwa au cha ndoa, kwamba mtu anapokufa au ndoa yake kuvunjika hakuna anapoulizwa ama kutakiwa kurejesha vyeti hivyo maana ni mali yake.

“Kama wakina Nape wanataka Dk. Slaa na wengine walioondoka CCM wawarejeshee kadi zao, basi wabadili katiba yao na kuliweka kisheria kama ilivyo kwa kadi za mabenki ambazo huwa mali za benki husika,” alisema.

Wakili huyo aliongeza kuwa, anachofanya Nape ni maajabu na hivyo wako watakaomtaka awaeleze kadi za CCM za hayati Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine waliofariki zimerejeshwa kwa nani kama ni mali ya chama.

Alisema kuwa, Nape anatakiwa kujikita kwenye mambo ya msingi ya kuendeleza chama chake na serikali wanayoiongoza, badala ya kuibua hoja za kijinga zisizo na tija kwa wananchi.

Hizi ndizo elimu zinazotakiwa kutolewa kwa Umma, Heko Wakili Kimogoro, lakini kwa upeo wa katibu mwenezi wa CCM sijui kama ataelewa ulichosema, zaidi atasema amezoea kutukanwa na wapenzi wa chadema. Kizungumkuti cha joka la ndimi mbili ndani ya CCM sio cha mchezo...hapa maskani tunasemaga CHEZEA JOKA LA NDIMI MBILI WEWE?!
 
Back
Top Bottom