Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,359
- 4,814
Mtaalamu wa Masuala ya Katiba na Sera Wakili Edson Kilatu ameeleza wasiwasi wake, na kutilia shaka kuhusu utendaji wa 'Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)' Nchini akidai kwamba akidai kwamba uhuru iliyopewa Tume hiyo kwa mujibu wa Katiba na Sheria hautumiki ipasavyo
Akihojiwa na Jambo TV kupitia kipindi cha 'Jambo Asubuhi' leo, Jumanne Machi 24.2026, Wakili Kilatu amesema wasiwasi unatokana na kwamba Makamishna wote wa Tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao wote wanalazimika kuteuliwa na Rais hivyo huenda wanafanya kazi kwa 'nidhamu ya kuogopa mamlaka ya uteuzi', sambamba na hiyo pia ameitaja Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa ni miongoni mwa taasisi anazotilia shaka utendaji wake hasa kwenye eneo la uhuru.