Wakili aidai Fastjet Sh60 mil kwa usumbufu

Pianist

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2010
Posts
681
Reaction score
372
Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea, John Mhozya amefungua kesi ya madai ya zaidi ya Sh60 milioni dhidi ya Shirika la Ndege la Fastjet katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika kesi hiyo, inayotarajiwa kusikilizwa na Hakimu Gabriel Mirumbe Mei 14, mwaka huu, Mhozya anaiomba Mahakama iiamuru Fastjet kumlipa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni fidia kutokana na kumsababishia usumbufu huku akitaka limuombe radhi.

Mhozya alidai kuwa Agosti, 2013 alitoa alikata tiketi ya safari ya kwenda Mwanza na kurudi Dar es Salaam kwenye ofisi za shirika hilo kwa lengo la kusafiri Oktoba 23, 2013 kuhudhuria kesi ya ardhi namba 3/2004 iliyokuwa ikisikilizwa Oktoba 24-30, 2013 mbele ya Jaji Jacqueline Dimelo mjini Mwanza.

Wakili huyo alidai kuwa ilipofika Oktoba 23, 2013 siku ambayo alipaswa kusafiri na ndege ya saa 12 jioni, Fastjet saa 8 mchana walimpigia simu wakimweleza kuwa kuna tatizo lililojitokeza na kumwuliza iwapo abadilishiwe ndege au arudishiwe fedha zake.

Alidai kuwa aliwataka wamtafutia ndege nyingine aliyosafiri nayo siku ya kesi Oktoba 24, 2013 asubuhi.

Alidai kuwa Oktoba 30, 2013 siku ambayo alipaswa kurudi Dar es Salaam kwa ndege ya shirika hilo kutoka Mwanza, alikwenda uwanja wa ndege lakini hakukuta hata wafanyakazi wa Fastjet wala ndege husika aliyotakiwa kusafiri nayo.

“Nilikuwa na namba zao za simu niliwapigia na kuuliza tatizo lilikuwa nini na kwa nini hawakunipa taarifa wakati namba yangu ya simu wanayo? Walinieleza kuwa ndege haikuwapo na safari ilikuwa imefutwa,” alidai Mhozya.

Aliongeza kuwa alitumia gharama zake kwenda Dar es Salaam ili kuwahi mikutano muhimu na kwamba alipofika aliandika taarifa ya kutaka kurejeshewa gharama zake lakini hakupata majibu hivyo kulazimika kufikisha suala hilo mahakamani.
 
hata mimi wameshawahi kuhahirisha safari yangu bila kunitaarifu kabla.
 
Niliwahi kureport hapa jinsi hawa jamaa wanavyofanya biashara kibabe!!!! Wamempata mtoto wa mjini ngoja awapeleke kasi kidogo!!!!!

Tiba
 
kumbe kuna hela kwenye hizi safari, ngoja jamaa akishinda na mimi nifuatilie, 60m si kidogo.
 
Natamani sana nikutane na huyo wakili, nna kesi nyingi za kumpa. Tanzania tunasumbuliwa kijinga sana.

Kuna siku nimeenda BRELA nikaambiwa rudi baada ya masaa mawili, kwenda baada ya masaa mawili sikumkuta huyo afisa aliyeniambia nirudi baada ya masaa mawili. Nikakaa saa nzima kumngoja hajatokea, ikabidi niondoke na nirudi tena siku inayofatia, nikamkuta, nikamueleza alichonifanyia jana. Bila hata remorse au samahani akanambia njoo kesho. Can you imagine? Nami sikukubali nikaenda kwa maboss nikawaeleza. Wakanitatulia tatizo langu in 2 minutes. Hebu fikiri, kazi ya dakika 2 imenichukuwa siku mbili, ni gharama ngapi ameniingiza yule kijana.

Tafadhali nijulisheni huyu lawyer nimtafute.
 
Hii nchi sehemu za kudai fidia nyingi sana, Sema watanzania wengi hatufatili haki zetu.

Kingine wengi hatujui sheria na hata ukijua sheria Maamuzi yanapindishwa.
 
Du kumbe fastjet wahuni hv! Yawezekana kuna jambo wanajivunia nyuma ya pazia
 
Natamani sana nikutane na huyo wakili, nna kesi nyingi za kumpa. Tanzania tunasumbuliwa kijinga sana.

Kuna siku nimeenda BRELA nikaambiwa rudi baada ya masaa mawili, kwenda baada ya masaa mawili sikumkuta huyo afisa aliyeniambia nirudi baada ya masaa mawili. Nikakaa saa nzima kumngoja hajatokea, ikabidi niondoke na nirudi tena siku inayofatia, nikamkuta, nikamueleza alichonifanyia jana. Bila hata remorse au samahani akanambia njoo kesho. Can you imagine? Nami sikukubali nikaenda kwa maboss nikawaeleza. Wakanitatulia tatizo langu in 2 minutes. Hebu fikiri, kazi ya dakika 2 imenichukuwa siku mbili, ni gharama ngapi ameniingiza yule kijana.

Tafadhali nijulisheni huyu lawyer nimtafute.

BRELA NI WATU WEMA SANA, wewe utakuwa ulileta UCCM na udini

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Natamani sana nikutane na huyo wakili, nna kesi nyingi za kumpa. Tanzania tunasumbuliwa kijinga sana.

Kuna siku nimeenda BRELA nikaambiwa rudi baada ya masaa mawili, kwenda baada ya masaa mawili sikumkuta huyo afisa aliyeniambia nirudi baada ya masaa mawili. Nikakaa saa nzima kumngoja hajatokea, ikabidi niondoke na nirudi tena siku inayofatia, nikamkuta, nikamueleza alichonifanyia jana. Bila hata remorse au samahani akanambia njoo kesho. Can you imagine? Nami sikukubali nikaenda kwa maboss nikawaeleza. Wakanitatulia tatizo langu in 2 minutes. Hebu fikiri, kazi ya dakika 2 imenichukuwa siku mbili, ni gharama ngapi ameniingiza yule kijana.

Tafadhali nijulisheni huyu lawyer nimtafute.

Sio lazima huyo dada angu hata wakili yoyote anafaa kwa kesi ndogo kama hiyo!
 
Jamaa kanifurahisha Sana. Watanzania tumeanza kuamka maana poor services tunaona Ni halali yetu.
 
Hii nchi sehemu za kudai fidia nyingi sana, Sema watanzania wengi hatufatili haki zetu.

Kingine wengi hatujui sheria na hata ukijua sheria Maamuzi yanapindishwa.
Kiongozi ni kweli kabisa! Yaani kuna sehemu nyingi sana watanzania tungeweza kuwashikisha adabu hawa wenye makampuni. Kwa mfano mitandao yote ya simu, ATMs n.k.
 
Safi sana...sasa ilitakiwa wahanga wote wa fastjet wakutane wafungue kesi ya pamoja ndo itapata nguvu zaidi
 
Natamani sana nikutane na huyo wakili, nna kesi nyingi za kumpa. Tanzania tunasumbuliwa kijinga sana.

Kuna siku nimeenda BRELA nikaambiwa rudi baada ya masaa mawili, kwenda baada ya masaa mawili sikumkuta huyo afisa aliyeniambia nirudi baada ya masaa mawili. Nikakaa saa nzima kumngoja hajatokea, ikabidi niondoke na nirudi tena siku inayofatia, nikamkuta, nikamueleza alichonifanyia jana. Bila hata remorse au samahani akanambia njoo kesho. Can you imagine? Nami sikukubali nikaenda kwa maboss nikawaeleza. Wakanitatulia tatizo langu in 2 minutes. Hebu fikiri, kazi ya dakika 2 imenichukuwa siku mbili, ni gharama ngapi ameniingiza yule kijana.

Tafadhali nijulisheni huyu lawyer nimtafute.
punguza unafki mtaa unaoishi ni mtaa wa kariakoo ndio mtaa una ofisi nyingi za mawakili na baada ya jengo tu la makao makuu ya ccm lumumba wakili twaha taslima ofisi zake zipo hapo na lunch anakula kwa abeid falcon.
 
hata mimi wamewahi kukatiza safari yangu DAR-MWZ bila kurudisha gharama zangu..ikabidi nichukue flight nyingine.....hawana huruma hawa jamaa ni kama wakenya vile. wanaamini wao ndo wako sawakila kitu kumbe watuwengine tunajua air idustry zaid yao.
 
Nilisafiri nao mara moja tu, sitaki kabisa kuwasikia hawa majamaa, yaani wanafanya kazi kama daladala
 
  • Thanks
Reactions: amu
Natamani sana nikutane na huyo wakili, nna kesi nyingi za kumpa. Tanzania tunasumbuliwa kijinga sana.

Kuna siku nimeenda BRELA nikaambiwa rudi baada ya masaa mawili, kwenda baada ya masaa mawili sikumkuta huyo afisa aliyeniambia nirudi baada ya masaa mawili. Nikakaa saa nzima kumngoja hajatokea, ikabidi niondoke na nirudi tena siku inayofatia, nikamkuta, nikamueleza alichonifanyia jana. Bila hata remorse au samahani akanambia njoo kesho. Can you imagine? Nami sikukubali nikaenda kwa maboss nikawaeleza. Wakanitatulia tatizo langu in 2 minutes. Hebu fikiri, kazi ya dakika 2 imenichukuwa siku mbili, ni gharama ngapi ameniingiza yule kijana.

Tafadhali nijulisheni huyu lawyer nimtafute.

Hizi njoo kesho mbona tutapishana mahakamani hadi zifurike? Siyo siri, asilimia kubwa sana ya watendaji wetu wanatusababishia hasara za maelfu ya fedha kwa utendaji wao dhaifu...
 
punguza unafki mtaa unaoishi ni mtaa wa kariakoo ndio mtaa una ofisi nyingi za mawakili na baada ya jengo tu la makao makuu ya ccm lumumba wakili twaha taslima ofisi zake zipo hapo na lunch anakula kwa abeid falcon.

Huyo wakili wa siasa mie simtaki. Anakufaa wewe huyo, maana naona Lissu hawafai tena pale Ufipa anapelekeshwa na kijana mdogo.
 
Back
Top Bottom