buffalo44
JF-Expert Member
- May 8, 2016
- 4,286
- 10,046
yani kila siku kushindanisha vi2 vya kupita tu ndugu zangu hebu fikiria ufalme wa babeli wenye kiburi katika kitabu cha danieli. japokuwa mji ulikuwa umepambwa kwa dhahabu na kuwa na upekee duniani mungu aliufanya ukawa makao ya mbwa mwitu na wanyama wakali je, mungu hatafutilia mbali hii miundombinu inayotupa kiburi sasa cha kukomoana kila kukicha? je, hamjui kuwa njia zenu zi mbele ya mungu mkuu ambaye aliwapa nyinyi maliasili za kila namna kuonyesha upendo wake kwenu badala yake mnazitumia kumringishia jirani yako. naanza na wakenya nyinyi mpepiga hatua katika kuzalisha vya nje bali vya ndani hamjaviimarisha kama kiburi kwa kila mnachopanga na mlichojenga je, mnaweza kwenda kuvifaid kuzimu vitu ambavyo mmevikuta hapa duniani? ndugu zangu wakenya badala ya kumpenda jirani yako mnakuwa watu WA kukejeli japo natambua kuna wakenya wengine ni wema Bali nyinyi mlio wachache mnatumia talanta zenu kuifanya Kenya ichukiwe bila sababu maalumu hivyo ndugu zangu mnapaswa kutumia muda wenu WA maana na sio kuweka majisifu na majivuno yapitayo. pili kwa watanzania wenzagu japo nchi yetu inasimangwa na majirani ni bora tukawajibu kwa upole kwa sababu hawana hekima nzuri ya tunakoelekea japo tuna vitu vya pekee ni bora tukafikiria jinsi ya kuondokana na umaskini kumbuka hata nehemia alipata upinzan kutoka kwa majirani ili kuzua ukuta kujengwa basi nanyi mnapaswa kupuuza dhihaka za wakenya maana hawataki tukamilishe ukuta na pia naomba muachane na wakenya wenye roho mbaya mkashirikiane na mkenya mwema.
wasalaam
wasalaam