Mpitagwa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 2,339
- 1,119
Jamani wiki iliyopita nilitembelea Kenya, kilichoishangaza ni kuwa kila unaponunua kitu lazima upewe risti na usipochukua mtoaji na walio jirani wanakushangaa sana. Na wanakwambia kuwa ni jukumu la kila mkenya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanalipa kodi. Na hili linatimizwa kwa kuhakikisha kuwa kila unaponunua, unachukua risti yako. Nikawaza na kupata hisia kuwa labda tabia hii imechangia Kenya kujiendesha kwa asilimia 98 kwa bajeti yake yenyewe. Hapa kwetu wanaJF wenzangu mnajua. tunafikia hata hatua ya kujadiliana na mfanyabiashara kuwa hii ni bei ya risti na hii ya bila risti na unajua kabisa kuwa hapa huyu anakwepa ushuru na unashiriki vizuri kabisa bila wasiwasi. Tufanyeje ili nasi tujifunze hili kwa wakenya?