Wakenya na lugha ya kiswahili

Haujaelewa ninachokiongelea, ni kweli kwamba Watanzania wengi wana matatizo na Lugha ya Kiswahili kama vile ilivyo sehemu yoyote ile Dunia hii, hata USA kuna wengi wana matatizo na English language, Uingereza, Uchina hivyo hivyo kuna Wachina wana matatizo na Mandarin, ila tofauti ni kwamba hakuna Mtanzania ambaye anajivunia kutokufahamu Kiswahili, kwetu sisi nia aibu kutokujua Kiswahili, wakati Kenya kutokujua au kujifanya haujui Kiswahili ni sifa, yaani watu wanajivunia kutokujua Kiswahili, wkt mtu huyo huyo ukimwambia hajui Kiingereza mnaweza mkagombana, na hiki ndicho ninachokiongelea!

Girlfriend wangu Mkenya aliniambia Kenya kuna Gazeti la Kiswahili na Wakenya wengi hulisoma kwa kujificha kwa kuogopa stigma kwamba kwa nini anasoma Gazeti la Kiswahili, ndicho ninachomaanisha!

Kwamba kuna tofauti ya kutokujua lugha vizuri na kujivunia kutokuijua lugha wkt ukweli ni kwamba Wakenya wengi wanajua Kiswahili tena vizuri sana tu, kwani sijawahi kupata shida ya kuwasiliana nikiwa huko, ila nimewahi kukejeliwa sana kwamba najua Kiswahili kizuri!

Umeshinda ukiturudiarudia hii ya wewe kuwa na "girlfriend mkenya", you are now ceasing to be credible!

Please!
 
Wewe naona umekosa kazi. Tunaposema hatujui kiswahili huwa tunakubali upungufu wetu. Tatizo lenu ni kujigamba eti kiswahili mnakijua ilhali hamkijui kamwe. Ndiposa Haya mashirika huwaajiri wakenya kwa kuwa sisi tunajua kwamba kuna vitu ambavyo hatuvijui na tuna nia ya kujifunza. Bunge lenu watu huongea SwaEnglish jambo ambalo halikubalika hapa Kenya. Katika bunge la kenya, huwezi kusema "hizo ndizo conditions ambazo development partners wanataka." Ukitenda upuuzi kama huo utaambiwa uketi chini. Kule kwenu mie huona Runinga na Magazeti yakiandika "Dokta", na mambo mengi ya kipuuzi ili kuonekana wastaarabu. Makosa ya L na R zimejaa ilhali bado mwajigamba eti kiswahili mnakijua. Tafuta mada tofauti.

Mkajifunze kutofautisha "thambi na dhambi" makosa zimejaa kwenye makomwe yenu makubwa na sura zenu mbayaa kama roho zenu.
 
Wewe naona umekosa kazi. Tunaposema hatujui kiswahili huwa tunakubali upungufu wetu. Tatizo lenu ni kujigamba eti kiswahili mnakijua ilhali hamkijui kamwe. Ndiposa Haya mashirika huwaajiri wakenya kwa kuwa sisi tunajua kwamba kuna vitu ambavyo hatuvijui na tuna nia ya kujifunza. Bunge lenu watu huongea SwaEnglish jambo ambalo halikubalika hapa Kenya. Katika bunge la kenya, huwezi kusema "hizo ndizo conditions ambazo development partners wanataka." Ukitenda upuuzi kama huo utaambiwa uketi chini. Kule kwenu mie huona Runinga na Magazeti yakiandika "Dokta", na mambo mengi ya kipuuzi ili kuonekana wastaarabu. Makosa ya L na R zimejaa ilhali bado mwajigamba eti kiswahili mnakijua. Tafuta mada tofauti.
 
Hii yote yaletwa na usomi usomi mwingi tu, hata hapo bongo yapo tu haya jamaa anachanganya ndimi ilimradi aonekane yupo juu kisa amefika chuo kikuu, kwa kenya hili la kudharau kiswahili lipo kwa sana hasa nyanda za juu (bara) ni sababu kusoma sana kwao. Hapa kenya kuanzia chekechea lugha ni uzungu hadi chuoni jumatatu hadi alhamisi lugha ni kiingereza so isiwasumbue sana.
 
Mleta mada achana na pombe jumapili jioni maana kesho jumatatu utaamka na mateso, ama kama vipi hakikisha umekula na pia unywe maji kwa wingi.
Haya mambo ya kulewa halafu unaingia JF na kuanza kubonyeza bonyeza simu na kutuletea ulevi wako humu yatakutoka puani siku moja.
We jamaa kiswahili umejifunzia wapi? Mbona kimenyooka sana
 
Utasikia unajua sisi Wakenya hatujui Kiswahili sana, sawa kwa hiyo mnajua lugha gani sasa? Kwa maana hata English hamjui pia, kwani Kenya siyo an English speaking country!

Au mnafikiri kutokujua Kiswahili ndiyo ujanja? Kiswahili ni Lugha ya Taifa Kenya na imeandikwa kwenye Katiba ya Kenya, sasa kujivunia kutokujua Lugha ya Taifa ya nchi yako ujinga wa mwisho Dunia hii!
Kijana....unataka kuamsha DUDE..!!
Subiri waje wenyewe..
 
Ni watu wachache sana wanaojua na kutumia Kiswahili ipasavyo, hata hiyo Tanzania yenu. Au unafikiria ule uharo nyie huandika ndio Kiswahili. Mtu anapokua muwazi na kukuambia hakifahamu Kiswahili vizuri unamchukulia kuwa mjinga, ilhali huo ndio ukweli.
Kiswahili chenyewe bado hakieleweki, maneno mengi yanaendelea kubuniwa kila siku maana hakijaiva. Juzi tu ndio mumejua maana ya 'makinikia', miaka yote wakati mlikua mnaliwa, mlikua mnaita mchanga wa madini.
Nyie majanga kweli, kwanza lugha zenu za asili hamzijui, Kiswahili chenyewe ndio hicho kinazingua, Kingereza lugha ya dunia kimewashinda.

Binafsi nimejikuta kwenye huu upumbavu wa nyie kutuona wajinga kisa tumekiri kutokujua Kiswahili ipasavyo, ipo siku nilitaka tafsiri ya Kiswahili ya maneno kwa mfano kama 'source code', 'software' n.k. Niliishia kuhangaika maana hata wenyewe hamjui.
Sheria zenu zenyewe mumeshindwa kuziandika kwa Kiswahili, na pia hata stakabadhi muhimu. Juzi hapo kuna zabuni imetangazwa ya kiserikali halafu nikakumbana na maneno kama 'Proposal must be written in English'. Wenyewe mnajua mapungufu ya hii lugha lakini kutwa huwa mnajifanya jeuri, hamna kitu cha ovyo kama maskini jeuri asiyetaka ushauri au kuambiwa.

Leo hii nenda hapo kwenye mgahawa Tanzania na uagize 'sharubati' uone jinsi watakushangaa, hadi pale utaagiza 'juisi' ndio utaeleweka.
We jamaa una vijembe sana
 
Hii yote yaletwa na usomi usomi mwingi tu, hata hapo bongo yapo tu haya jamaa anachanganya ndimi ilimradi aonekane yupo juu kisa amefika chuo kikuu, kwa kenya hili la kudharau kiswahili lipo kwa sana hasa nyanda za juu (bara) ni sababu kusoma sana kwao. Hapa kenya kuanzia chekechea lugha ni uzungu hadi chuoni jumatatu hadi alhamisi lugha ni kiingereza so isiwasumbue sana.
Bora wewe umekubali na kuelewa ukweli maana nimewasoma hapo juu jamaa wote wanapingana na hoja ya Barbarosa
 
Uni bora kujifunza kingereza kuliko kiswahili maaneka kiswahili ni lugha inazungumzwa maeneo machache sana duniani ukilingalinisha na kingireza .so uzungumze kiswahili sanifu au bofu haina tija yeyote kwako maanake hatokufikisha popote utashinda ukihangakia hapa east africa tu ndio maanake bongolalas wengi wamejaa humo hawatoki nje kutupiga vijembe humu.juzi katika uzinduzi wa sportpesa tanzania niliona maajabu mzungu anazungumza kingereza then mnatafusiriwa kwa kiswahili .bure kabisa nyie mjifunze kingereza ka si hivyo itakua ngori.
 
6f88c43b12cadca19fe736f440a47eb3.jpg
na dio mana hawatii mimba... in kenyan slang
we ni mnouma...tibiim
 
Back
Top Bottom