Wakenya na lugha ya kiswahili

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Utasikia unajua sisi Wakenya hatujui Kiswahili sana, sawa kwa hiyo mnajua lugha gani sasa? Kwa maana hata English hamjui pia, kwani Kenya siyo an English speaking country!

Au mnafikiri kutokujua Kiswahili ndiyo ujanja? Kiswahili ni Lugha ya Taifa Kenya na imeandikwa kwenye Katiba ya Kenya, sasa kujivunia kutokujua Lugha ya Taifa ya nchi yako ujinga wa mwisho Dunia hii!
 
Huku Dar es Salaam Gor Mahia hadi sasa wameshampiga AFC Leopard goli mbili... Bravo Raila and your co...
 
naona watanzania wana machungu hehe...:D:D:D:D yaani povu imemwagwa kwel kwel aisee...
 
6f88c43b12cadca19fe736f440a47eb3.jpg
na dio mana hawatii mimba... in kenyan slang
 
cha msingi watanzania msiwe watu wa kukasirika haraka haraka...wakenya wana tabia ya kudhani wao ni wazuri kuliko waafrika mashariki wengine...ningewashauri msitilie hili rohoni...otherwise mtakufa na pressure...
 
Hahahahahaaaa!... are you a psychologist, counsellor or something?... huku Dar es Salaam Gor Mahia wameshamaliza kazi, wamempiga AFC Leopard 3-0...
 
Mleta mada achana na pombe jumapili jioni maana kesho jumatatu utaamka na mateso, ama kama vipi hakikisha umekula na pia unywe maji kwa wingi.
Haya mambo ya kulewa halafu unaingia JF na kuanza kubonyeza bonyeza simu na kutuletea ulevi wako humu yatakutoka puani siku moja.
 
Utasikia unajua sisi Wakenya hatujui Kiswahili sana, sawa kwa hiyo mnajua lugha gani sasa? Kwa maana hata English hamjui pia, kwani Kenya siyo an English speaking country!

Au mnafikiri kutokujua Kiswahili ndiyo ujanja? Kiswahili ni Lugha ya Taifa Kenya na imeandikwa kwenye Katiba ya Kenya, sasa kujivunia kutokujua Lugha ya Taifa ya nchi yako ujinga wa mwisho Dunia hii!

Mbona Watz ndio hututusi hapa eti hatujui Kiswahili? Hata tukijaribu vipi bado lazima mtutusi hatujui Kiswahili, Vipi tena ugeuze kwamba ni sisi husema hivyo??

Kiswahili Kizuri kipo pwani ya Kenya hata Wabongo mkifika kule nyinyi limbukeni tu! Mtasoma
 
Tatizo siyo kujua au kutokujua Kiswahili, bali tatizo langu na Wakenya ni kujivunia kutokujua Kiswahili, hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa kwani Kiswahili ni Lugha ya Taifa ya Kenya, sasa iweje Mtu ajivunie kutokufahamu Lugha yake ya Taifa?
Tanzania ni aibu kutokujua Kiswahili na wala hakuna anawezea kujivunia hili!

Cha kushangaza zaidi Mkenya huyo huyo anayejivunia hajui Kiswahili, kazi ikitangazwa na UN, Google au au sijui Microsoft kwamba wanahitaji Mtu mwenye uwezo wa kutumia Lugha ya Kiswahili kwa Ufasaha, Wakenya wale wale wasiokitaka Kiswahili na ambao wanajivunia kila siku kutokukifahamu ndiyo wa kwanza kutuma maombi ya kazi na kusema Kiswahili ni lugha yao, na hapo ndipo tatizo langu na Wakenya lilipo!
 
Ni watu wachache sana wanaojua na kutumia Kiswahili ipasavyo, hata hiyo Tanzania yenu. Au unafikiria ule uharo nyie huandika ndio Kiswahili. Mtu anapokua muwazi na kukuambia hakifahamu Kiswahili vizuri unamchukulia kuwa mjinga, ilhali huo ndio ukweli.
Kiswahili chenyewe bado hakieleweki, maneno mengi yanaendelea kubuniwa kila siku maana hakijaiva. Juzi tu ndio mumejua maana ya 'makinikia', miaka yote wakati mlikua mnaliwa, mlikua mnaita mchanga wa madini.
Nyie majanga kweli, kwanza lugha zenu za asili hamzijui, Kiswahili chenyewe ndio hicho kinazingua, Kingereza lugha ya dunia kimewashinda.

Binafsi nimejikuta kwenye huu upumbavu wa nyie kutuona wajinga kisa tumekiri kutokujua Kiswahili ipasavyo, ipo siku nilitaka tafsiri ya Kiswahili ya maneno kwa mfano kama 'source code', 'software' n.k. Niliishia kuhangaika maana hata wenyewe hamjui.
Sheria zenu zenyewe mumeshindwa kuziandika kwa Kiswahili, na pia hata stakabadhi muhimu. Juzi hapo kuna zabuni imetangazwa ya kiserikali halafu nikakumbana na maneno kama 'Proposal must be written in English'. Wenyewe mnajua mapungufu ya hii lugha lakini kutwa huwa mnajifanya jeuri, hamna kitu cha ovyo kama maskini jeuri asiyetaka ushauri au kuambiwa.

Leo hii nenda hapo kwenye mgahawa Tanzania na uagize 'sharubati' uone jinsi watakushangaa, hadi pale utaagiza 'juisi' ndio utaeleweka.
 
Tatizo siyo kujua au kutokujua Kiswahili, bali tatizo langu na Wakenya ni kujivunia kutokujua Kiswahili, hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa kwani Kiswahili ni Lugha ya Taifa ya Kenya, sasa iweje Mtu ajivunie kutokufahamu Lugha yake ya Taifa?
Tanzania ni aibu kutokujua Kiswahili na wala hakuna anawezea kujivunia hili!

Cha kushangaza zaidi Mkenya huyo huyo anayejivunia hajui Kiswahili, kazi ikitangazwa na UN, Google au au sijui Microsoft kwamba wanahitaji Mtu mwenye uwezo wa kutumia Lugha ya Kiswahili kwa Ufasaha, Wakenya wale wale wasiokitaka Kiswahili na ambao wanajivunia kila siku kutokukifahamu ndiyo wa kwanza kutuma maombi ya kazi na kusema Kiswahili ni lugha yao, na hapo ndipo tatizo langu na Wakenya lilipo!

Wewe naona umekosa kazi. Tunaposema hatujui kiswahili huwa tunakubali upungufu wetu. Tatizo lenu ni kujigamba eti kiswahili mnakijua ilhali hamkijui kamwe. Ndiposa Haya mashirika huwaajiri wakenya kwa kuwa sisi tunajua kwamba kuna vitu ambavyo hatuvijui na tuna nia ya kujifunza. Bunge lenu watu huongea SwaEnglish jambo ambalo halikubalika hapa Kenya. Katika bunge la kenya, huwezi kusema "hizo ndizo conditions ambazo development partners wanataka." Ukitenda upuuzi kama huo utaambiwa uketi chini. Kule kwenu mie huona Runinga na Magazeti yakiandika "Dokta", na mambo mengi ya kipuuzi ili kuonekana wastaarabu. Makosa ya L na R zimejaa ilhali bado mwajigamba eti kiswahili mnakijua. Tafuta mada tofauti.
 
Back
Top Bottom