Wakenya bana kwa hiyo kukosa kura ya Tanzania UNSC imekuwa nongwa?

buffalo44

JF-Expert Member
May 8, 2016
3,140
6,287
Umofia kwenu wakuu.

Naona kila thread ya jukwaa hili kwenye comment wakenya wanahasira na chuki za juu baada ya kutoa kapepa ambako me binafsi sijaconfirm kuwa Tanzania haijapigia Kenya kura.

Wakenya hebu tulieni bana, sisi ni nchi huru na kupiga kura tunapiga kwa hiari tukiwa na akili timamu kabisa.

Sasa nyie kukosa mnakomaa na sababu za kina Geza Ulole, Joto la Jiwe na Kadhalika.

Serikali ndiyo inajua kwa nini?

Urafiki na undugu upo, ila kutumia neno urafiki ili mpate mnachotaka sio urafiki huo.

Heshimuni maamuzi ya rafiki zenu.

Kumbuka muda huu wa kura kumekuwa na mikwaruzano kati ya Kenya na Tanzania juu ya janga la Corona.

Mmesahau mlivyokuwa mnatoa maneno machafu kipindi tunadili na Corona na fake news zenu.

Basi kama kumpakazia tope ndugu na rafiki yenu, huku mkitegemea awafaidishe muda mnaotaka ndio nini hicho?

Tulieni basi hata nyie mmeenda kinyume na Tanzania mara nyingi sana na hatujalilia huku mitandaoni.

Alafu nakumbuka mlisema Ethiopia ni ndugu yenu wa kweli kuliko Sisi inakuwaje mnamuelewa alafu sisi mnatukomalia.

Uganda mnadai anategemea mombasa Port duh!

Niishie hapa.

Heshimuni maamuzi ya Tanzania yakiwa hasi au chanya hatupo hapa kufurahisha nyie. Tupo huru.
 
Habari ndio hiyo, hatuna muda na uchawi wenu nyie wadjibouti. Hamna namna itabidi mjikunyate huko pembeni kwenye kona hadi mwaka wa 2023.
Tunachowashangaa ni Kenya kuchanganyikiwa baada ya kusikia Tanzania hatukupigia Kenya, hilo linatushangaza sana. Mbona ninyi mnafanya maamuzi yenu bila kutushirikisha sisi hatuwasemi?
 
Kukosa kura ya nyeusi mwenzetu yeyote ukanda huu wa Sahara lazima tupigie kelele, waarabu wamekusanyika na kuungana huko na kuwa kimoja, hata Rwanda au Uganda wangepeleka kura yao Uarabuni lazima tungeng'aka balaa, haya mambo hayafanwyi kwa demokrasia za kwenye vitabu, hii ni high level geopolitics, sidhani kajamba wa Tandale anaweza kuwa na ufahamu wake akishavimbiwa uji wa ulezi.

Hii hata Afrika Kusini wasingetupigia, lazima tugewasema.
 
Kukosa kura ya nyeusi mwenzetu yeyote ukanda huu wa Sahara lazima tupigie kelele, waarabu wamekusanyika na kuungana huko na kuwa kimoja, hata Rwanda au Uganda wangepeleka kura yao Uarabuni lazima tungeng'aka balaa, haya mambo hayafanwyi kwa demokrasia za kwenye vitabu, hii ni high level geopolitics, sidhani kajamba wa Tandale anaweza kuwa na ufahamu wake akishavimbiwa uji wa ulezi.

Hii hata Afrika Kusini wasingetupigia, lazima tugewasema.

Mzee sababu yako inakosa mshiko Somalia na Ethiopia vipi?

Unazingua tu.

Toa sababu moja ya kuiandama Tanzania ukiacha Nchi nyingine hizo za Africa
 
Uamuzi wa kutowapigia kura hau-reflect matazamo wa Tanzania wote Bali mataahira wachache possibly two or one
 
Mzee sababu yako inakosa mshiko Somalia na Ethiopia vipi?

Unazingua tu.

Toa sababu moja ya kuiandama Tanzania ukiacha Nchi nyingine hizo za Africa

Narudia tena, nyeusi mwenzetu kutotupigia kura lazima tupige makelele, na kwa taarifa yako hao Wasomali, Wahabeshi na Waarabu wote lao moja, huzungumza kimoja, hivyo Msukuma kwenda kushobokea waarabu na kuwaacha wenzako wote ndani ya SADC na EAC ni ujuha.

Leo hii Msomali mkiwa naye Uarabuni utabaguliwa aachwe yeye hata kama mtakua nyote wa dini moja.
 
Leo hii Msomali mkiwa naye Uarabuni utabaguliwa aachwe yeye hata kama mtakua nyote wa dini moja.


Kumbe hili ni suala ya Ubaguzi???!!--- ama kweli Wakenya ndiyo maana ubaguzi wa kikabila hauishi huko kwenu sasa mnataka kuambukiza na Watz, haitawezekana.
 
Kumbe hili ni suala ya Ubaguzi?? Ama kweli Wakenya ndiyo maana ubaguzi wa kikabila hauishi huko kwenu sasa mnataka kuambukiza na Watz, haitawezekana.

Hii inaitwa geopolitics, huna uwezo wa kuielewa nje ya hapo Tandale. Dunia haipo black and white kama mnavyofundishwa shuleni, huwa kuna balances fulani huzingatiwa kwenye mahesabu kama haya, kwanza kabisa lazima uangalie nani kati ya wote ambaye huwa unang'ang'ania kuingia kwake, takwimu za kibiashara, soko, maslahi na mambo mengine mengi tu.
 
Hii inaitwa geopolitics, huna uwezo wa kuielewa nje ya hapo Tandale, dunia haipo black and white kama mnavyofundishwa shuleni, huwa kuna balances fulani huzingatiwa kwenye mahesabu kama haya, kwanza kabisa lazima uangalie nani kati ya wote ambaye huwa unang'ang'ania kuingia kwake, takwimu za kibiashara, soko, maslahi na mambo mengine mengi tu.

Wewe ungeongelea juu ya hiyo Geopolitics yako na sio masuala ya tribalism, au wataka kusema Geopolitics ndani yake kuna Tribalism?

Mimi sikuipenda hii point yako ambayo umei associate na Upigaji kura wa Tz katika UN.👇🏻

Leo hii Msomali mkiwa naye Uarabuni utabaguliwa aachwe yeye hata kama mtakua nyote wa dini moja.
 
Hii inaitwa geopolitics, huna uwezo wa kuielewa nje ya hapo Tandale.....dunia haipo black and white kama mnavyofundishwa shuleni, huwa kuna balances fulani huzingatiwa kwenye mahesabu kama haya, kwanza kabisa lazima uangalie nani kati ya wote ambaye huwa unang'ang'ania kuingia kwake, takwimu za kibiashara, soko, maslahi na mambo mengine mengi tu.

Hivi unaijua origin ya hicho ki page cha kura fake kinachowatoa povu?

Hahahah TZ ni babalao nyumbu nyie, mtacheza tu mziki tunaotaka.
 
Kwani wao walikuja kuomba tuwapigie kura au walilala nyumbani wakidhani kwa sababu ni majirani basi kura watapata?
 
Djibouti alikuwa anastahili, nakumbuka kipindi kile Kenya na kampeni yao ya kuzuia kuuza stock ya pembe za ndovu, kushadadia kutokujenga barabara mbugani n.k Wakenya ni mashetani siyo watu.
 
buffalo44,

Kwa sisi tuliopembeni tunahitimisha yafuatayo:

- Ukiona unagombea uenyekiti wa mtaa wenu, na una sifa zote za kuwa mwenyekiti wa mtaa, na ikatokea jirani yako mliyewekeana mpaka wa nyumba zenu amekupigia kura ya HAPANA akampigia NDIYO wa nyumba ya mwisho mtaani kwenu basi tambua kwamba hakuna ujirani tena ila mmepakana tuu.

- Hatutashangaa minyukano huko EAC ikiendelea, na huko mipakani wakitunishiana misuli.
 
La. Ni upendo. Kama ingekuwa ni chuki basi hatungepiga kelele.
Hakuna maisha bila changamoto,wakati mwingine aina budi kukubaliana na hali halisi,japo sina hakika kama hatujawapigia kura.
Unaweza kuthibitisha ya kwamba hatujawapigia kura?
 
Wewe ungeongelea juu ya hiyo Geopolitics yako na sio masuala ya tribalism, au wataka kusema Geopolitics ndani yake kuna Tribalism???!!

Mimi sikuipenda hii point yako ambayo umei associate na Upigaji kura wa Tz katika UN.👇🏻

Kama hauyajui haya kwaheri, naona bado unahitaji darasa.
 
Back
Top Bottom