Tutandelea siku tukiweza kuwa sisi, kifkra, uvumbuzi kujitegemea kwa kila kotu

FANALEKI

JF-Expert Member
Jul 28, 2023
240
434
Habari..?

Majuzi majuma kadhaa yaliyipita Raisi Samia alilalamikia kitendo cha nchi kama Thailand kutuacha kimaendeleo wakati uhuri tulipata wakati unaokaribiana.

Yes, tumjibu raisi wetu kuwa akianza kuibomoa CCM na kuweka katiba mpya itakua tumeweza kusogea hatua ya kwanza. Hili taifa letu lina kwamisha kwa CCM na watu wake japo sio wote ila walio wengi ni useless kabisa.

Mfano kitu kdogo cha kukifanya siku moja ndani ya ofisi itachukua majuma kadhaa. Let say kuandika hata barua watatumia majuma 10 au mwezi au miezi 😁😁😁😁 hii ni hatari afu kesho watajitapa tunachapa kazi kweli kweli. 😁😁😁😁.

Hiki ni kichekesho kinachopatikana Tanzania tukubali muda umetuacha hata kwa afrika tumeachwa parefu na wenzetu, hata kenya tu hapo wametupiga gap kiasi kweli kweli. Ni wakati waliopo juu wajue wao ndio mzizi wa kuicheleweshea hii nchi kufikia walipo wale tulioanza safari nao kipindi kile.

Dereva ujilaumu kwa kukosa weledi au ulaumu chombo chako kuwa kibovu au chakavu kilichokosa maboresho yakuendana na kasi ya kufikia mahala pale walipo wale tulioanza nao hii safari. Nchi yetu inarasilimali nyingi je zinatusaidia nini..? Kama sio kuishia kwenye matumbo ya wachache tu tena wanaojifanya wanatumbania kumbe wanatuingiza shimoni tena shimo lenye moto wa gesi tunaungua sisi wakina lala njaa.

Kiongozi alie pita kwa kura zq magumashi atakuaje na uchungu na hili taifa? Kiongozi anaejua hata akila pesa za uma hatachukuliwa hatua yoyote kisheria au kiwajibishwa anaanzaje kutuonea huruma sisi walala njaa. Ifike hatua mtambue kuwa nyie ndicho kiini cha kupitwa sisi na wale tunaosema tulikua nao.

Hii inanikumbusha ule utani wa shuleni tukiambizana kuwa usije kusema nilisoma na yule jamaa, alikua rafiki yangu nk. Toka mwanzo mlikamatia mpini nyinyi ila ajabu jembe halilimi sawa sawia na kasi ya muda. Jambo la kufanya siku 1 Tanzania hii ni miez itatumika au mwaka.

Kwa sababu hapo kuna wanataka rushwa, uongo, kukwamishana, kudharauliana, waliopewa vyeo kimchongo hawa hawana maadili ya taaluma husika wapo coz ni watiifu na wanaomsujudia mtu fulan mwenye kuwalisha. Hili liondolewe. Lina kwamisha maendeleo ya hili taifa.

Kitu cha kufuta kwenye hii nchi ni CCM. Msije sema mm chama fulani sina chama na sijawahi kupiga kura na sitaja piga kura mpaka nikiona tume huru na katiba inayoeleweka itakayo wawajibisha mafisadi na sio hizi bla bla blaa mara hiki mara hiki nchi yangu inatafunwa na wenye ukijani kama mtoto anavyo lamba na kunyonya peremende maana hajali kuchafuka kwa kuwa hajui tabu ya kujisafisha.

Siku tukiamua kuilinda Tanzania (Tanganyika &Zanzibar, bara tupewe nchi yetu na raisi wetu tujipambanie wote wote why kule kuna raisi wao ila huku hakuna hii ngumu kuielewa hapa nyerere alifanya matope aisee).

Tutailinda Tanzania tukiweza kufuta hiki chama na hii katiba ikirekebishwa na kuruhusu kuwawajibisha watawala. Kuna people zinafanya kazi zinazohitaji weledi wa hali ya juu ila zenyewe maamuma sema coz zinajua kulamba asali, kusujudu na kutetea kila jambo hata baya, zenyewe zipo kwa ofisi zibakula kiyoyozi afu wale wenye maarifa hata ya kuuliza hapa ni nini na nini wanaonekana kikwazo acha tujidanganye kutafuta mchawi ni nani wakati uchawi mnao nyie nyie.
 
Back
Top Bottom