Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nchi ya Kenya inajihusisha na vita Somalia ambayo haiwahusu, hii ni proxy war yaani Wakenya wanapigana vita kwa niaba ya Wazungu na haina maslahi yoyote yale kwa nchi ya Kenya!
Acheni kutumiwa na Wazungu kwa maana gharama mnayolipa mpaka leo hii ni kubwa sana hivi juzi hapa ingawaje Serikali yenu haisemi ukweli lkn Wanajeshi walioliwa na Somalia wanafikia 100 sasa hii ni namba kubwa kwa lipi hasa?
Mnafaidika nini na Somalia zaidi tu ya kujenga uadui wa kudumu? Msisahau kwamba mna raia wengi sana wenye asili ya Somalia na wanafedha mpaka leo hii wanamiliki sehemu kubwa tu ya uchumi wa Kenya na hawa wote hawako upande wa Kenya kisiasa bali wa Somalia!
Hivyo narudia tena ondoeni Majeshi Somalia na muache kutumiwa na Wazungu, nimesikia Waziri Mkuu wa Uingereza anakuja Kenya ingawaje wengi mtadanganywa sababu ya safari yake lkn kilicho nyuma hasa ya hii safari ni kuishawishi Kenya iendelee kubakia Somalia na kupigana vita kwa ajili ya Uingereza, acheni hizo waambieni Wazungu waje wapigane vita yao wenyewe na siyo kuwatumia ninyi, hawa askari 100 waliokufa walipaswa wawe Wazungu na siyo Wakenya!