Suala la handling ya wadada ni tete na kila mara limekuwa linajitokeza katika sura anuwai.
Kuna familia naifahamu dada na watumishi wengine hawatumii chakula sawa na wana familia. Sijui kwanini wanadamu tunapenda kujisahau hivi!
Muumba huyu huyu angeweza kubadili kibao na ukajikuta wewe mwajiri wa leo ndio mdada ( mwajiriwa).
Mimi naamini ukijiweka katika nafasi ya mdada au mtumishi, utajikuta unakuwa fair . Sio mbaya kugombeza lakini tuwe na kiasi na iwe justified na isigeuke kuwa nagging , eti kisa kwa vile ni mtumishi.
Huwa nasikitika saana kwa kweli maana hawa ni binadamu kama sisi.
Sasa kufungua friji kama mtu hajawahi kuona friji nayo igeuke nongwa? Je mkeo akipelekwa ofisi za NASA huko mambele, naye akaambiwa kufungua mitambo ili mtambo upae sayari ya Mars naye ataweza bila kugombwa? Kila kitu ukijuacho ni relative ujue na sio kuwa kuwa mjini ni nongwa!
Jirani yangu mwingine kwa mwaka hukaa na wasichana 6 hadi 8 ; wastani wa mwezi mmoja na nusu per msichana!
Sielewi asilani. Nilitangulia kusema katika thread fulani kuwa namshukuru Mungu, wangu nimeishi naye mwaka wa 7 huu nikiwa sina watoto na hata sasa nikiwa nimejaliwa watoto. Kwakweli namshukuru Mungu tu kwa yote maana nikisema mengine itakuwa kama kukosa hekima, shukrani na kujisifia.
Mungu atubariki sote na atupe moyo wa mapendo kwa kila mwanadamu kadri tujaliwavyo!