Wake za watu mna nini?

ismail hassan

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
685
1,612
Kumekuwa na wimbi kubwa sana siku hizi kuhusu wake za watu kutongoza vijana. Mara nyingi mimi kama kijana nakumbana na hii kadhia mara nyingi sana, na hasa hasa kutoka mitandao ya kijamii na mitaani pia.

Unakuta mmama mtu mzima anamtongoza kijana bila hata ya hofu na aibu, mama kimtazamo anajistiri. Unaweza ukasema huyu ndo mke sasa. Mama ana watoto watatu wanne lakini kijana ana miaka 20-25 ni makamu ya mtoto wake wa kumzaa lakini bado tu anamtaka.

Binafsi Juzi, nipo nimetulia zangu magetoni, Nakuta text toka mtandao mmoja wa kijamii. Kufupisha story, tulichart kawaida sana na huyo mama. (nina mfahamu vizuri na yeye pia ananifahamu) tuliwahi kukaa mtaa mmoja miaka hiyo. Maelezo yake ni kwamba amenipenda na anataka tufanye siri baasi tu hana jinsi alikuwa ananipenda toka siku nyingi tu. Nilimuuliza swali hili. Mumeo ana matatizo gani mpaka unatak kuja kwangu?

Alinijibu hivi! kwann una maswali mengi hivyo! au kwakuwa nlikwambia nataka kuchepuka na ww? nimeshakwambia mm nmkupend tu na nikakuahid nitakutunza kivyovyote vile mana watu wakijua haitakuwa aibu kwako itakuwa ni aibu kwangu mana mm ni mama mtu mzima lazma aibu iwe kwangu tu. Tunafanya yetu kisiri tu na hakuna lolote baya litatokea.

Nikamuuliza swali 1.
Unaniahid kuwa hutochepuka na mwengine? na utanitunza kama ulivyosema?

Her.. Nakuahid ni ww tu upo moyon stochpuka na mwengine na zaid ya mume wng.

me...Binafsi nilimuahid mpenz wng hivyohivy kutochepuka...kwaiy ibaki hivyo...stay on your way..Naomba tuishie hapa.

Bado ananismbua na Leo nina mblock, ni msmbuf mno.

Ukiachana na huyo wapo wengi tu wamama huwa wana tabia hii. Hili tatizo linatokana na nini? si mimi tu, mara nyingi vijana rika langu wanayoyaongea ni haya haya nnayoandika mimi. Muda mwengine unaweza ukahis labda ni story tu, kumbe mambo ndivyo yalivyo. Wanawake wengi hasa wake za watu wanapenda sana vijana. Ni wengi mno.

Naandika kwa uchungu mana najua mm pia nitaoa na wanawake tunaoenda kuoa ndo hao hao. Unamuona ni mstaarabu kumbe chini ya kapeti anafanya makubwa ambayo hata ukisimuliwa hutoamini. Wadau wa JF hebu toeni michango tufanye nini hii issue iishe au nini hasa kinasababisha mpaka kufikia hali hii. Au kama yupo alokumbana na hali kama hii ashushe uzi hapa hapa. Ilikuwaje na alikabiliana nalo vipi?

Karibuni.
 
Back
Top Bottom