Wakazi wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge

Kwa kweli Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ni mtu muhimu sana kwenye hiki kipindi wakazi wa Musoma Mjini lulu yenu hiyo.
tayari mmesahau yaliyomkuta mathayo mpelekeni na huyo apewe shule yake
 
Huyu ritz ni muongo na mnafki hizo habari umezipata wapi, umbea umekuzidi!
 
mura hizo habari umezitoa mtaa gani mbona huyo muhongo hafahamiki hapa msm town ukweli kazi wanayofanya chadema hawa ccm wasahau hili jimbo kabisa naomba wadau mfike musoma mjione wenyewe haya tunayosema

Mura wewe lazima utakuwa unakaa Migori Kenya, ulizia mitaa ya Mkendo-Kati mpaka Uhuru, Kawawa, kote anafahamika.
 
Wewe ni Muongo wa kutupwa kwa lindi la sahaurika.

Wakazi wa Majita ambao wapo katika jimbo la Musoma Vijijini; jimbo ambao kwa sasa linaitwa Wilaya Butiama ndio waliomuomba.

Muhongo hawezi kufurukuta kwa Vincet Nyerere wa Musoma Mjini isitoshe hata kwa Nimrod Mkono atafanikiwa kuula wa chuia hasa pale Majita kwingineko mf. Kiabakari, Busegwe, Mazami, Buhemba, Butiama ataambulia patupu.

Funga kazi: Usilolijua na usiku wa Giza Ritz
 
Last edited by a moderator:
Sio kweli..Mkendo tupo wenyewe - The Kigeras hatumfahamu..

ha haa ha, Mkuu Mkandara, hunajua Prof. Muhongo ni rafiki mkubwa ma Madaraka Nyerere, wote watoto Musoma sijui itakuaje kama akigombea ubunge dhidi ya Vicent Nyerere.
 
Last edited by a moderator:

mwitaz,
Sasa unanishambulia mie muongo sasa wewe hizo habari zako umezitoa wapi? Mkuu wasalimie majita kwikona.
 
Last edited by a moderator:
Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini..
...Ni waziri wa Nishati na madini lakini hajawawezesha kabisa wananchi wa Mara kufaidika na dhahabu ya North Mara...
Mpeni muda hata miezi sita hana toka rais amteue.
Sasa ni kwa vipi hao wakazi wengi wa Musoma Mjini wameonekana kumkubali kwa utendaji wake na hata miezi sita hana!

 
mhe. Profesa sospeter muhongo, ni mzaliwa wa musoma mjini. Ana haki ya kugombea.

ni kweli ana haki kama mzaliwa wa tanzania na musoma mjini kugombea!
Swali je wananchi wamekutuma umwombe agombee kwa niamba yao?
Je kura za kuidhinisha hii sanaa zilipigwa wapi na chini ya uangalizi wa;...
 
Sasa ni kwa vipi hao wakazi wengi wa Musoma Mjini wameonekana kumkubali kwa utendaji wake na hata miezi sita hana!

Lidies Official Tiara-Show Mag-3. Mag3,
 
Last edited by a moderator:

umedanganya!!!! huyu mtu ni mwenyeji wa musoma vijijini siyo mjini, kama anataka ubunge basi ajiandae kupambana na mbunge wa maisha mh mkono.
 
umedanganya!!!! huyu mtu ni mwenyeji wa musoma vijijini siyo mjini, kama anataka ubunge basi ajiandae kupambana na mbunge wa maisha mh mkono.

Wakati mwingine kama kitu hujui ni bora kukaa kimya kuliko kujidhalilisha kama hivi Prof. Muhongo kwao ni Musoma Mjini.
 
Wakati mwingine kama kitu hujui ni bora kukaa kimya kuliko kujidhalilisha kama hivi Prof. Muhongo kwao ni Musoma Mjini.
mijini watu wanahamia tu kwa ajili ya kazi, biashara nk mfano ukienda da slam utakuta watu kibao wenye asili ya maeneo mbalimbali wanaishi huko wamejenga majumba na wengine wanakufa na kuzikwa huko huko, lakini wale wenye hamu ya kugombea ubungei wanarudi kwenye majimbo ya asili zao.
 
Musoma Mjini maeneo ya Mkendo Kati.
Mkendo kati ni sehemu ndogo sana ya Musoma mjini.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa mzee wake hayati Mutaragara Chirangi alikuwa mtu maarufu sana pale Musoma; akitumia jina la Chirangi anaweza kupeta, ingawa atakuwa anapambana na jina la Nyerere.
 
una kila dalili ya kuwashwa, hakujawahi kuwa na mkutano , mwisenge, mkendo wala makoko sasa kama sio kuwashwa washwa anakosema mabumba ni nini?

Sijui kama Nyasho huyu jamaa kafika akaongea nao ...hata Mwigobelo na Kigera sembuse Rwamlimi hajafika wala hajaitisha kikao nao sijui sasa ameyapata wapi hayo maoni ya wakazi wa Musoma...labda waishio DSM lakini kwa vyovyote hao watakuwa wajanja hawawezi kudanganyika kirahisi all the way from musoma to dar.
 

PWENTI ndinani
 

Mkuu mbona mbishi narudia tena Prof. Muhongo kazaliwa Musoma Mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…