Wakazi wa Musoma Mjini wamuomba Prof Sospeter Muhongo kugombea ubunge

Mkendo kati ni sehemu ndogo sana ya Musoma mjini.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa mzee wake hayati Mutaragara Chirangi alikuwa mtu maarufu sana pale Musoma; akitumia jina la Chirangi anaweza kupeta, ingawa atakuwa anapambana na jina la Nyerere.

Pitia vizuri bandiko langu sijasema Mkendo peke yake, nilikuwa na mjibu mtu, sehemu nyingi wamemuomba maeneo ya Kawawa, Uhuru, Nyasho, Mwigobelo.
 
Mkendo kati ni sehemu ndogo sana ya Musoma mjini.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa mzee wake hayati Mutaragara Chirangi alikuwa mtu maarufu sana pale Musoma; akitumia jina la Chirangi anaweza kupeta, ingawa atakuwa anapambana na jina la Nyerere.

Kwenye red mkuu, ni kweli kuwa Marehemu, Mutaragara wa Chirangi wa Musuto wa Muhongo wa Nyawayega wa Marero alikuwa mzee wake, kwa maana ya Baba Mdogo, lakini Baba Mzazi wa Prof. Sospeter Muhongo ambae pia ni marehemu anaitwa Mzee Faru wa Mwijarubi wa Muhongo wa Nyawayega wa Marero!
 
Kwanza Muhongo si mzaliwa wa Musoma mjini bali ni mzaliwa wa musoma vijijini katika kijiji cha Suguti. Pili haki ya kugombea anayo kama mtanzania tena mahali popote ndani ya tz hii si lazima iwe musoma mjini. Tatu amuulize mbunge aliyepita bwana mathayo kwanini hataki kurejea kwenye ulingo jimboni humo badala yake ameanza taratibu za maandalizi ya ubunge wilayani serengeti ambako anasema "bhala bado nabhakangi" yaani bado ni wajinga, kwa hiyo wanaserengeti wameshaanza kumshtukia na wameanzisha taratibu za kula na kipofu bila kumugusa mkono. Nne Muhongo kama maprofesa wa ukweli walio wengi hawezi kupambana na bwana mdogo Vicent Nyerere kwa hoja na sababu kubwa ni uzoefu katika masuala ya siasa na ujengaji wa hoja, suala ambalo limemtimua aliyekuwa mpinzani wa dogo nyerere baada ya kuona dogo akizidi kujizatiti kutokana na ujengaji wa hoja za ukweli sio za kipropaganda kama ilivyozoeleka kwa wana CCM wengi. Tano Wizara waliyompa ni wizara ya kashfa nyingi na mafisadi walio wengi akiwemo rais wetu wamewekeza kwenye wizara hiyo, kwa hiyo ama aamue kuisafisha kiukweli kwa kuvunja mikataba ya kijambazi inayotutia hasara kama taifa na madudu mengine yote yaliyomo au aungane na hao majambazi kuendeleza naye achukue chake mapema. Ushauri wangu kwa muhongo ni huu, kama atajisikia kugombea ubunge basi akagombee Musoma (V) na hii ni kutokana na utafiti
nilioufanya ktk wilaya ya musoma (V).
 
1778.jpg

Wanabodi..

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM ameombwa na wakazi Musoma Mjini kugombea ubunge jimboni humo mwaka 2015.

Profesa Sospeter Muhongo, ni msomi na mzaliwa wa Musoma Mjini wakazi wa mkoa Mara wanasema wakati umefika wa kumpa ubunge Profesa Muhongo, kutokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake ili hawatumikie wananchi wa Mkoa wa Mara.

Jimbo la Musoma Mjini kwa sasa linaongozwa na chama cha Chadema kupitia mbunge wake Vicent Nyerere.

Wakazi wengi wa Musoma Mjini wanaoneka kumkubali zaidi Prof Muhongo, kutoka utendaji wake wake katika Wizara ya Nishati na Madini..

waambie hao ccm wa mussoma mjini wamebugi meeen! Katiba ijayo haitaruhusu waziri kuwa mbunge
 
Ritz maswali ya msingi kwako:
  1. Kikako ambacho kilitoa hayo maoni kilifanyika lini na wapi?
  2. Hao unaowasema ni Wananchi wa Musoma Mjini au Wanachama wa CCM?
  3. Muhogo amewafanyia nini wananchi wa Musoma Mjini? au Kwakumsimamisha kazi Mhando?
Good friday!
 
Kaaah!

Tanzania na watanzania wake wana safari ndefu sana!
"Utendaji wake ktk wizara ya Nishati na Madini"
Yaani muda alokaa ndani ya hiyo wizara tayari umekwisha thibitisha utendaji kazi wake - kiasi cha kuvutia kuombwa kugombea ubunge!!!!
Kazi kweli kweli,
Huku mtaani kwetu bado tuna mgao usokuwa na ratiba, sijui huko Musoma!
 
Akiwa anaongea na baadhi ya wageni katika msafara wa obama na wafanyabiashara wachache wa kitanzaniakatika viwanja vya Ikulu, Waziri Muhongo amesema baada ya rais kikwete, kutakuwepo na vacuum wa uongozi nchini. baada ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya umeme iliyochangia rais obama kuja tanzania, anaonelea agombea urais kwa sababu wanaotarajia kugomea kwa sasa ni mafisadi....
 
Muhongo for presidency, of all the people????? Anyway, ana haki ya kikatiba kufanya hivyo, ingawa sio aina ya watu tunaowahitaji kwa Tz tuitakayo. Akafundishe na kufanya tafiti professor huyu, siasa hawezi!
 
Sina shida ya yeye kugombea urais. Shida yangu ni hayo maendeleo makubwa anayosema ameyaleta kwenye sekta ya umeme kiasi cha kumvutia Obama.
Kusema kweli mimi sijaona maendeleo yoyote kwenye umeme. Kwa hiyo naomba anifafanulie kidogo kwenye eneo hilo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Akiwa anaongea na baadhi ya wageni katika msafara wa obama na wafanyabiashara wachache wa kitanzaniakatika viwanja vya Ikulu, Waziri Muhongo amesema baada ya rais kikwete, kutakuwepo na vacuum wa uongozi nchini. baada ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya umeme iliyochangia rais obama kuja tanzania, anaonelea agombea urais kwa sababu wanaotarajia kugomea kwa sasa ni mafisadi....
Ni haki yake kikatiba. Kama anataka kupima kama simba ana meno kwa kuweka mkono kwenye mdomo wake, ajaribu.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Alaf hyo wizara kaiweza saa ngapi.....au analeta mauzauza ya mchana hapa!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Alaf hyo wizara kaiweza saa ngapi.....au analeta mauzauza ya mchana hapa!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Prof. Muhongo akifanikiwa kuwasambaza umeme vijijini. Atakuwa na wapiga kura wengi na URAIS UTAMUNUKIA. Na atakubalika mno! Wengi humu wanatumika kuleta majina na si hoja!, na ndio Maana wanakataa majina ya watu potential , Muhongo Ana agenda umeme vijijini ,


Je wengine wana agenda ya kuwa rais then like taifa la UNGA na kumwaga mipesa?
 
Nchi yetu ilipofika inahitaji raisi jasiri, mwenye msimamo, asiye yumbishwa na wana siasa, wafadhili na wafanya biashara kwenye mambo yenye maslahi mapana kwa taifa.

Pia tunahitaji raisi mwenye uwezo binafsi wa kuchambua na kufanya maamuzi based on logical thinking. MTU ambaye atakaye jiamini na mwenye kua tiari kushindanisha mawazo tofauti kisayansi/kisomi na kamwe si kisiasa.

Pia awe MTU mwenye udikteta kiasi angalau kias cha Ben mkapa.

Mpaka sasa Prof Muhongo amedhihirisha kua na sifa hizi kwa kias kikubwa.I know this may seem to be an awkward opinion, but this is a hard truth.

Nashauli vyombo vyetu vya kiusalama vichukue ushauli huu kwani naamini the first and last vetting of a coming president is done by them(TISS).

Nawakilisha
 
Back
Top Bottom