Wakazi wa Madale, Mbopo na Kangwe wakosa mawasiliano ya barabara kwa zaidi ya wiki mbili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Wakazi wa mitaa ya Madale, Nakasangwe na Mbopo manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam wameendelea kukosa mawasiliano ya barabara kwa zaidi ya wiki mbili sasa kufuatia daraja kiunganisho kukatika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kuleta adha kubwa ikiwemo kukosa usafiri wakiwemo wanawake wanaojifungua na watoto kwenda shule.

Wakiongea na ITV wakazi hao wakiwemo viongozi wa mitaa mitatu ambao wanaeleza daraja hilo kuvunjika mara baada ya bwawa tegemezi la uchumi wa kilimo cha mbogamboga la skauti kujaa na kupasua kuta zake kabla ya kuvunja daraja hilo na kuomba msaada wa ujenzi wa daraja kwenda sambamba na kurejesha bwawa katika hali yake kwani ndio tegemezi la uchumi wa akina mama wanaolisha masoko ya manispaa ya Kionondoni na Ubungo.

Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata ya wazo diwani Joel Mwakalebela amesema tayari wamesha iarifu ofisi ya kitengo cha maafa mkoa na kwamba mvua hizo zilizonyesha mwanzoni mwa mwezi huu zimeharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya barabara madaraja kiasi cha kuihtaji fedha nyingi kutoka serikalini.


ITV
 
Back
Top Bottom