Wakazi wa madale container tunalia kwa kukosa maji

Monseur

JF-Expert Member
Dec 5, 2016
655
522
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza mimi ni mkazi wa madale kata ya mivumoni eneo la Container maarufu Kwa Mwanajeshi! Tuna ratiba ya kupata maji siku moja tu kwa wiki, yaani siku ya JUMANNE mchana hadi jumatano mchana!

Kulingana na idadi ya wakazi iliyopo ratiba hii haitutoshi, kwani mara nyingi maji yanapotoka yanakuwa na pressure ndogo sana kiasi kwamba hayana uwezo wa kupanda kuingia kwenye ma Tank!

Na isitoshe kuna wakati ratiba hiyo haifuatwi na tunalazimika kupitiliza hata wiki mbili bila ya kuwa na maji! Jiulize tunaishije?

Tuna mifugo, tuna bustani, na tuna watu! Tunamuomba muhusika wa kufungua maji ndugu Mohamed, maarufu Mudi, anayepatikana kwa namba ya simu 0714 029 193 awe na moyo wa huruma na atufungulie maji kwa kufuata ratiba na walau iwe siku mbili mfululizo au tatu kwa wiki yaani ianze JUMATATU hadi jumatano kuliko hii ratiba ya sasa ya saa 24 tu kwa wiki yaani JUMANNE mchana hadi jumatano saa nne asubuhi

Na isitoshe Mudi anafungulia maji pale anapojisikia bila kufuata ratiba! Sisi ni binadamu na sio wanyama tunahitaji Maji! Ili tuweze kuishi, maana maji ni uhai
 
Back
Top Bottom