Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakifurahia usafiri wa treni za mjini

Hii regime haiishi unafiki.......watuache na jf yetu na si kila wakati kututishia kuufunga mtandao wetu wakati kuna idara za serikali nazo wanautumia kupata faida kibiashara bila kulipia matangazo
 
Usafiri wa train umesaidia sana wakazi wa kigogo, gongo la mboto, kitunda, banana na ubungo. Japo ni ngumu sana kufuata ratiba zake, ila limesaidia
 
Boresheni vituo, havina sehemu za kukaa abiria hasahasa kipindi cha mvua. Na hata wakati wa jua kali.
Reli ya ubungo pale daraja la mto msimbazi, mto umeanza kuhama kwa kufanya umbo mfano wa herufi S. Maji yataharibu reli na kusababisha lihitajike daraja refu zaidi. Mto unyooshwe kufuata daraja.

Kule Pugu station, abiria wanaotoka Pugu Bangulo hawana daraja maji yakijaa mtoni hawawezi kuvuka. Fanyeni mpàñgo wa kuwawekea daraja hata kwa vyuma vya reli
 
Back
Top Bottom