Wakazi wa DSM tabia hizi sio za kiungwana kabisa

Afisa Tabibu

JF-Expert Member
Oct 29, 2021
484
799
Twende kwenye mada, jaman watu wa Dar tabia hizi sio za kiungwana

1. Kumuona mwenzio anaibiwa au kupigwa nyie mnakaa pembeni kuangalia hamtoi msaada, huu sio uungwana

2. Mtu kukusalimia unamuangalia tu halafu humjibu au kumjibu kwa sauti ya chini hasa kwa wadada, kisa anaendesha guta, au hajavaa vizuri.

3. Utapeli, yaan hadi ndugu yako km yupo DSM akakuambia tuma pesa akufanyie manunuzi basi ujue kuna ugomvi mnakwenda kuutengeneza

4. Ubabe na kupandishiana, watu wa dar sio wanyenyekevu, kila mtu ni mbabe, unaweza kumakanyaga kwa bahati mbaya tu lakin akaja juu hata ukimuomba msamaha bado anaona km unamdhihaki

5. Kutoka kimapenz na mpenz wa rafiki yako, hii kwa wote wadada na wakaka, wanakula mashemeji mno.

6. Kila msaada lazima uombwe hela, yaan mtu anaweza kukusaidia kunyanyua kamzigo kadogo tu akimaliza utasikia nitoe basi....

7. Wanaume kumsaidia mdada hadi amle, yaan ukiona mwanaume wa dar anamsaidia mdada au mkeo, lift, vizawad ujue mwisho wake ataliwa, wanaume wa dar hawasaidii wadada hivi hivi

Ongeza zingine......
 
Haya yote ni sababu ya maisha magumu, watu Wana depression sana.

1. kuyumba kwa mahusiano na mapenzi ya muhusika

2. Madeni, upatu, vicoba na kamari mtu akidhani atatoboa kwa betting

3. Ajira ngumu, nyongeza ndogo ya mshahara, na gharama za maisha kuwa juu.

4. Mawazo ya kuzamia ughaibuni, wakidhani pengine watatoboa maana huku mambo si mambo.

5. Matumizi ya vilevi, yaani pombe kali, madawa ya kulevya,humfanya muhusika kuwa chizi japo si wote.

6. Madhara ya punyeto na ukosefu wa nguvu za kiume kwa vijana huwafanya wakate tamaa na kujikuta Wana madeni kwa wenzi wao

Hivyo namna pekee ya waathirika Hawa kupata faraja ni kusikia au kuona mwenzake anapata matatizo, utasikia, Kila mtu apambane na hali yake

Mkuu haya ukiyakuta hapa Dar es salaam yapotezee tu cha msingi chukua tahadhari na jilinde.
 
Ndo maana MMU imejaa malalamiko ya wakaka/wababa kuhusu hela,kusaidia kidogo wadada bila kupewa mbususu

Na pia panyaroad wanatawala dar sababu ni namba hio moja
 
1. Kumuona mwenzio anaibiwa au kupigwa nyie mnakaa pembeni kuangalia hamtoi msaada, huu sio uungwa
Hii nimeikuta mtaani kwetu kijana muuza simu wahuni walimwita kwamba wananunua kijana kufika tu wakamnyanganya na mapanga wakampiga alafu Kuna wapumbavu walikua wanaangalia tukio lote niliumia Sana jamaa damu zinamwajika nilitamani ningekupo kimsaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom