Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Watu/waumini wanataka content.
Jana nilibadirisha channel yule dada sijui ni sister sijui ni kateksta alikua anaongea kuhusu watoto kawasagia Kunguni watoto, anahimiza nini km sio ukatiri kwa watoto? Yaan anawahimiza wazazi wawakatiri watoto wao. Nikabadiri channel nikaenda kusikiliza bolingo na maombolezo ya Mwinyi channel gani sijui, alinivuruga sana content maandalizi pia wasiongee ongee tu km wapo kwenye vibaraza vyao wajue watu tupo huku tunawasikiliza
 
nijikite kwenye ukongwe hapo, hakuna wakongwe kwenye dini kama Wayahudi, wao wamekuwa waaminifu kwenye dini mno, lakini dini haijawaokoa, wanakufa na wanaenda motoni kwasababu ni kwa kutumia dini hiyohiyo walimsumbua sana Yesu na waliwauwa mitume waliosambaza hata huu ukristo. Cha msingi, tuishi tukijua kwamba, dini haiokoi, Biblia inasema tunatakiwa kuokoka. kwa kua ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni kwamba Mungu alimfufua katika wafu utaokoka, kwa moyo mtu huamini na kwa kinywa hukiri. tunatakiwa kuokoka, hizi dini ni NGOs tu ambazo tena zimesajiliwa kabisa kwenye secular government hiihii na zinaweza kufutwa au kurekebishwa, ila njia ya wokovu kwa Yesu Kristo ni moja tu, kuokoka ni lazima.
Acha uongo wewe hiv unaijua vizuri historia ya ulimwengu? Huo uyahudi hauna sifa ya kuwa dini pekee kongwe maana kabla yake kulikuwepo dini kongwe zaid ambazo kibongobongo ama Afrika hatuzijui kwa sababu hatukutawaliwa na hawa jamaa wa hizo dini basi hatufahamu data za dini zao ambazo ni kongwe kuliko hata hizi tulizoletewa

Top 10& The most Oldest Religions in the world are
👉1. Hinduism (founded around the 15th- 5th century BCE)
👉2. Zoroanistrianism (found around 10th -5th centyry BCE)
👉3. Yazdânism
👉4. Judaism (found around 9th- 5th century BCE)
👉5. Jainism
👉6. Confucianism
👉7. Buddhism
👉8. Taoism
👉9. Shintoism (3rd century BCE - 8th century CE)
👉10. Christian

Mnaona sasa na hapo bado hatujachimbuachimbua zile dini kongwe zaidi ambazo ndizo mizizi ya hizi dini mpya kongwe kidogo zilizocopy hadith na stories na kuunda dini mpya, mfano the oldest faith civilization of kemet ndio iliyozaa hizo takataka zingine zinazoitwa dini ambazo ndizo zilicopy huko karibia 90% ya stories kwa kubadiri striptures na characters ili kuunda hizo ngonjera za kidini.
Kiuhalisia na kiukweli ukifuatilia historia kiuhalali hizi dini za kiyahudi sijui ukristo na uislam hawa hata Top 20 hawawezi kuwepo katika dini kongwe na zenye ukweli kidogo maana hizi ni dini zilizoanzishwa juzi tu hapo na kabla yao kuna mamia ya imani na dini zilishakuwepo na bado zipo.
Tujitahidi kusoma na kuwa makini tunapotoa komenti humu adharan ili kuepusha aibu ndogondogo za kudanganya watu pia ni vizuri kuwa makini kwa heshima ya JF kwamba ina Great thinkers,
 
Attachments

  • Screenshot_20240305_005148_Opera Mini.jpg
    Screenshot_20240305_005148_Opera Mini.jpg
    543.2 KB · Views: 2
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Mimi ni Mkatoliki Niliyebatizwa na kupokea kipaimara mwaka 1996.

Nilijifunza Imani ya kikatoliki nikiwa Mtu mzima.

Hivyo naijua vizuri.

Lakini pia nimejifunza habari za Neno la Mungu kupitia majukwa mbali mbali ya Biblia na Injili.

Naweza kusema kuwa ktk nyanja ya Elimu Kuhusu Neno la Mungu Kanisa Katoliki Linapwaya sana.

Wale Mapadre na Maaskofu tunaoamini wamesoma sana inawezekana kuna vitu vingine wamesoma lakini sio Neno la Mungu.

Maana sioni wamebobea kwenye nini.
 
FACT.
Ni kweli kabisa, wakatoliki tumezidi kuwa nyuma kama koti la mvua kwa kweli. Tubadilike
 
Acha uongo wewe hiv unaijua vizuri historia ya ulimwengu? Huo uyahudi hauna sifa ya kuwa dini pekee kongwe maana kabla yake kulikuwepo dini kongwe zaid ambazo kibongobongo ama Afrika hatuzijui kwa sababu hatukutawaliwa na hawa jamaa wa hizo dini basi hatufahamu data za dini zao ambazo ni kongwe kuliko hata hizi tulizoletewa

Top 10& The most Oldest Religions in the world are
👉1. Hinduism (founded around the 15th- 5th century BCE)
👉2. Zoroanistrianism (found around 10th -5th centyry BCE)
👉3. Yazdânism
👉4. Judaism (found around 9th- 5th century BCE)
👉5. Jainism
👉6. Confucianism
👉7. Buddhism
👉8. Taoism
👉9. Shintoism (3rd century BCE - 8th century CE)
👉10. Christian

Mnaona sasa na hapo bado hatujachimbuachimbua zile dini kongwe zaidi ambazo ndizo mizizi ya hizi dini mpya kongwe kidogo zilizocopy hadith na stories na kuunda dini mpya, mfano the oldest faith civilization of kemet ndio iliyozaa hizo takataka zingine zinazoitwa dini ambazo ndizo zilicopy huko karibia 90% ya stories kwa kubadiri striptures na characters ili kuunda hizo ngonjera za kidini.
Kiuhalisia na kiukweli ukifuatilia historia kiuhalali hizi dini za kiyahudi sijui ukristo na uislam hawa hata Top 20 hawawezi kuwepo katika dini kongwe na zenye ukweli kidogo maana hizi ni dini zilizoanzishwa juzi tu hapo na kabla yao kuna mamia ya imani na dini zilishakuwepo na bado zipo.
Tujitahidi kusoma na kuwa makini tunapotoa komenti humu adharan ili kuepusha aibu ndogondogo za kudanganya watu pia ni vizuri kuwa makini kwa heshima ya JF kwamba ina Great thinkers,
ni kweli, shetani alishaanza kitamb na hizo dini zake, ndio maana hata Mungu alitoa amri mojawapo kwamba usiwena miungu mingine ila mimi, manake watu walikuwa na imani kwa miungu mingine tangu zamani sana. hilo halina ubishi, ila mimi nililenga kwenye dini inayomtaja Mungu wa kweli. Melkizedeki mfalme wa salem hakuwa myahudi, na alikuwa ni kuhani wa Mungu aliye juu, hadi Ibrahim alimtolea fungu la kumi, hii inamaanisha sio wayahudi pekee walikuwa wa kwanza kumwabudu huyu Mungu wa kweli ambaye walikija kubahatika kuingia naye maagano makubwa mno yanayowasaidia hadi leo, imani ya Ibrahim ili wabeba.

hata sasa, ukiwa na Imani Biblia inasema umekuwa mtoto wa Ibrahim aliyekuwa na imani na utapata vipawa vilevile alivyoahidiwa Ibrahim. hili ndilo tumaini letu. umwendeapo Mungu amini kwamba anaweza kufanya na kwamba yeye ni mwaminifu. sifa kuu ya Mungu ni uaminifu na upendo, kile alichokisema lazima atakitenda kama ukiwa na imani.
 
Kwenye radio maria mwenyewe nashangaaga sana, like how mtu afungulie radio ili asali,
Kama nataka kusali nazima kila kitu nakaa comfortable alone nasali sio nianze kusikiliza radio mara mitambo iingilia niahirishe,

Wajaribu kujikita kwenye kuufundisha ukatoliki, na kutoa neno kwa kufuata ukatoliki ,
Wapunguze unnecessary sala kwa radio, hakuna anaesikiliza
Mkuu unajua ugumu wa Kusali rozari mtu unapokuwa mwenyewe....?

Radio Tumaini na Maria zinasaidia kutupa muongozo wa sala zipi za kusali katika kila kipindi cha mwaka

Pia husaidia kukumbusha mda wa waumini kusali.
 
Mimi ni Mkatoliki Niliyebatizwa na kupokea kipaimara mwaka 1996.

Nilijifunza Imani ya kikatoliki nikiwa Mtu mzima.

Hivyo naijua vizuri.

Lakini pia nimejifunza habari za Neno la Mungu kupitia majukwa mbali mbali ya Biblia na Injili.

Naweza kusema kuwa ktk nyanja ya Elimu Kuhusu Neno la Mungu Kanisa Katoliki Linapwaya sana.

Wale Mapadre na Maaskofu tunaoamini wamesoma sana inawezekana kuna vitu vingine wamesoma lakini sio Neno la Mungu.

Maana sioni wamebobea kwenye nini.
Mapadre ni watu waliosoma sana. Sana. Hivyo wanajua vitu vingi kuhusiana na humanity. Wanapohubiri huwa wanahubiri kimkakati sana ili wasivuke mipaka. Tofauti na hawa wahubiri ambao huwa wanapandwa na mizuka na kuanza kushusha vifungu vya biblia kama hawana akili.
Wako mapadre wahubiri/wainjilishaji. Akisimama jukwaani au mimbarini hungependa atoke hapo. Mmojawapo ni yule padre wa kihaya (jina limenitoka).

Matika kuhubiri, mapadre huangazia pia literature, kwamba kwa mfano ni kwa nini Yesu alipokuja waisraeli hawakumwelewa na walimkataa.
Sasa kati ya haya mengi wayajuayo wangekuwa wanatumegea zaidi pia kupitia media zingine. Si lazima kwa njia ya mahubiri
 
kitu kikubwa sana kanisa lilipoteza, ni Roho Mtakatifu. katika maisha yako usije hata siku moja ukafikiri kuhubiri kwa kutumia kiwango cha elimu, ufahamu wa mambo mengi, kuhubiri kwa kutumia akili zako za mwili n.k kama kunaokoa, elimu ya duniani haiokoi, wala hekima ya kibinadamu haiokoi hata uwe mzuri vipi kwenye public speech maneno yako hayana uwezo kuokoa, kama hayasemwa na Roho Mtakatifu ndani yako, ingekuwa hivyo wala tusingeenda kanisani, maprofesa wasingeenda kwasababu tayari tuna elimu ya kutosha ya kuishi na tunajua mambo mengi mno kuliko hata wanaotuhubiria, au badala ya kuhubiriwa tungeenda tu kwa wanasaikolojia au washauri au watu wenye elimu, au wengine wana uelewa wa dunia wa chin mno kuliko sisi wasingestahili kutuhubiria, hata hao mapadre wapo tuliowazidi elimu wengi mno na uelewa tumewazidi.

Siku ya Pentecost Petro ambaye alikuwa mvuvi tu, alisimama akahubiri watu 3000 wakaokoka, alikuwa hajawahi kufanya jambo kubwa la kiwango kile kabla, kwasababu alijawa na Nguvu za Roho Mtakatifu, hivyo aliyekuwa anahubiri sio Petro, ni Roho Mtakatifu akimtumia Petro kama chombo tu. Mhubiri unachotakiwa ni kusafisha moyo wako sawasawa na vile tunavyosafisha sahani ili itumiwe kwa chakula, wewe unasafisha moyo ili Mungu akutumie kama chombo tu.

Sauti iliyochanganywa na Roho Mtakatifu ina Nguvu za kupasua hata miamba iliyopo moyoni, hata tone moja tu la Roho Mtakatifu likikugusa linaleta badiliko, Roho Mtaktifu ni mafuta, ni mhuri ambao akiongea kwa yeyote aliyekutana naye ni kama mhuri umepigwa, na yeye ndiye anayebadilisha mioyo, ndiye anayeokoa. watu mbona wameanza kusikia mahubiri miaka nenda rudi ila hawabadiliki? ni kwa sababu maneno matupu ya watu hayaokoi, hayabadilishi hata ufanyeje, ila Nguvu za Mungu zikiwepo kwa mhubiri ndizo zinazo hukumu na kubadilisha na kuokoa. wachache wataelewa ufunuo huu.
 
Andiko zuri. Pia sijasema mapadre hawana roho Mt. Nakumbuka mch. Kimaro aliwahi kusema Padre mmoja ni wahubiri 1000. Kwa lugha nyingine wanayo ya ziada kuwashinda hao wanaoibuka kama uyoga. Pia Roho Mt. Hayupo kwenye kuhubiri tu. Ndio maana yapo mapaji 7 ya Roho Mt; hekima, akili, shauri, nguvu, elimu, ibada, na uchaji wa Mungu
 
Mkuu,Nahisi una point ila tatizo sasa unataka vitu vingi.Kwanza,Kanisa Katoliki sio la kulinganishwa na Hayo makanisa na hizo radio na hizo TV.Ni Katoliki Takatifu la Mitume.Pili Kusali Redion Sio Kosa na kimsingi ni jambo zuri.Kama imani yako inakwazika kwa sababu tu unaangalia hizo chaneli zingine basi usiziangalie ila kama bado unatatizika ninakusahuri uende ukamuone kiongozi wako wa kiroho maana hapo shida sio Kanisa katoliki shida ni wewe.
 
kitu kikubwa sana kanisa lilipoteza, ni Roho Mtakatifu. katika maisha yako usije hata siku moja ukafikiri kuhubiri kwa kutumia kiwango cha elimu, ufahamu wa mambo mengi, kuhubiri kwa kutumia akili zako za mwili n.k kama kunaokoa, elimu ya duniani haiokoi, wala hekima ya kibinadamu haiokoi hata uwe mzuri vipi kwenye public speech maneno yako hayana uwezo kuokoa, kama hayasemwa na Roho Mtakatifu ndani yako, ingekuwa hivyo wala tusingeenda kanisani, maprofesa wasingeenda kwasababu tayari tuna elimu ya kutosha ya kuishi na tunajua mambo mengi mno kuliko hata wanaotuhubiria, au badala ya kuhubiriwa tungeenda tu kwa wanasaikolojia au washauri au watu wenye elimu, au wengine wana uelewa wa dunia wa chin mno kuliko sisi wasingestahili kutuhubiria, hata hao mapadre wapo tuliowazidi elimu wengi mno na uelewa tumewazidi.

Siku ya Pentecost Petro ambaye alikuwa mvuvi tu, alisimama akahubiri watu 3000 wakaokoka, alikuwa hajawahi kufanya jambo kubwa la kiwango kile kabla, kwasababu alijawa na Nguvu za Roho Mtakatifu, hivyo aliyekuwa anahubiri sio Petro, ni Roho Mtakatifu akimtumia Petro kama chombo tu. Mhubiri unachotakiwa ni kusafisha moyo wako sawasawa na vile tunavyosafisha sahani ili itumiwe kwa chakula, wewe unasafisha moyo ili Mungu akutumie kama chombo tu.

Sauti iliyochanganywa na Roho Mtakatifu ina Nguvu za kupasua hata miamba iliyopo moyoni, hata tone moja tu la Roho Mtakatifu likikugusa linaleta badiliko, Roho Mtaktifu ni mafuta, ni mhuri ambao akiongea kwa yeyote aliyekutana naye ni kama mhuri umepigwa, na yeye ndiye anayebadilisha mioyo, ndiye anayeokoa. watu mbona wameanza kusikia mahubiri miaka nenda rudi ila hawabadiliki? ni kwa sababu maneno matupu ya watu hayaokoi, hayabadilishi hata ufanyeje, ila Nguvu za Mungu zikiwepo kwa mhubiri ndizo zinazo hukumu na kubadilisha na kuokoa. wachache wataelewa ufunuo huu.
Tuhuma zako ni nzito sana ila andiko lako linahitaji maswali.Roho mtakatifu ni nini au ni nani?Je ili andiko lako uliloweka hapa umeongozwa na Roho mtakatifu?
 
Uko sawa sana. Mimi ni mkatoliki na hili unalolisema nalielewa sana. Mambo yote yenye ushahabiano na nguvu ya Roho mtakatifu ni kama hayapewi nafasi katika kanisa letu. Mmoja alitangulia kuandika hapa miujiza haina maana. Sasa unajiuliza ni kwa namna gani utageuza mioyo ya wasio ifahamu nguvu ya Mungu usipotenda mambo makuu ya Mungu. Kwa kweli tukaze kuliombea kanisa maana ni wengi wanaangamia kwa kutokuamini nguvu ya Roho mtakatifu. Mathayo 13:58 utaona Yesu hakufanya mujica wowote nyumbani kwao kwa sababu hawakuamini. Nadhan sababu kama hiyo inaweza kuwa ndio sababu kwa nini hatuoni ishara kubwa na nyingi ambazo Roho mtakatifu anaweza kufanya kupitia watakatifu wake.
Kuna wakati naona kanisa limejikita kwenye doctrine za kanisa kuliko ukuu wa Yesu kitu ambacho kwa sehemu huenda tunamuudhi sana Mungu
 
Mkuu kama unaangalia miujiza utapotea maana MiujiA ya Kileo haitoki kwa Mungu.

Jambo lenye kasoro ktk Kanisa letu ni Kukosa Msisitizo ktk Kujifunza Bibilia na Neno la Mungu kwa ujumla.

Yaani Wakatoliki We Are Ignorant Mpaka Mlei au Muumini uchukue hatua we mwenyewe za kujifunza.
 
Acha kulinganisha kanisa katoliki na hao wahuni wanaotumia makanisa kupiga dili. Kanisa katoliki linaongozwa na watu wenye akili nyingi sana na wako mbele ya muda. Kanisa katoliki ni kama CCM. Yaani wako kuanzia ngazi ya shina ambapo wao huita Jumuiya. Anguko la kanisa katoliki ni gumu
 
Andiko zuri. Pia sijasema mapadre hawana roho Mt. Nakumbuka mch. Kimaro aliwahi kusema Padre mmoja ni wahubiri 1000. Kwa lugha nyingine wanayo ya ziada kuwashinda hao wanaoibuka kama uyoga. Pia Roho Mt. Hayupo kwenye kuhubiri tu. Ndio maana yapo mapaji 7 ya Roho Mt; hekima, akili, shauri, nguvu, elimu, ibada, na uchaji wa Mungu
kwa bahati mbaya sana, ni neno gumu nitakuambia, linakwaza na kuonyesha kama vile najiinua au labda natukana watu au nabeza imani za watu, ila dawa hata kama ni chungu ni muhimu kuinywa. MAPADRE HAWANA ROHO MTAKATIFU, KWASABABU HAWAJAOKOKA NA HAWAAMINI KUOKOKA.

Tangu siku ya Pentecost, Roho Mtakatifu aliposhuka, kuna ishara za wazi kabisa zinazoweza kukuonyesha pasi na shaka kuwa huyu ana Roho na huyu hana, imani hii inaweza kukusaidia umpate Roho na hii haiwezi kukusaidia. hata kipindi kile pamoja na kwamba wayahudi walikuwa wanasali sana kwenye masinagogi, tena pamoja na mitume (kwasababu awali mitume walikuwa bado wanaenda kusali kwenye masinagogi yaleyale pamoja na wayahudi), lakini ni mitume tu walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wale waliokuwa wakiokoka. wasiookoka hata kama walishika dini namna gani, hawakuwa na Roho Mtakatifu, na ndivyo ilivyo hadi sasa. kwa bahati mbaya, hata utetee namna gani au kuwasafisha mapadre kwamba wana Roho au la, hautawasaidia, wewe sio final say, ila kwa kuangalia Neno la Mungu unaweza kujua huyu ana Roho na huyu hana.

ISHARA ZA ROHO MTAKATIFU

1. KUNENA KWA LUGHA
. kila aliyejazwa Roho Mtakatifu kwenye kitabu cha Matendo ya mitume, alinena kwa Lugha, na wale ambao hawakunena waliwekewa mikono ili wanene. Marko 16:17-18 "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya,..." sasa tuambie ni padre gani ulishawahi kumwona ananena kwa lugha? au mkatoliki gani anene kwa lugha kama hajafukuzwa ukatoliki siku hiyohiyo? why? MATENDO 19:1 -10 inasema, Ikawa Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso, akakutana na wanafunzi kadhaa wa kadhaa huko, akawauliza, je? mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? wakamjibu la hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. akawauliza basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, kyaani Yesu. waliosikia haya wakabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu. na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. sasa tueleze, ulishawahi kuona wapi Padre ana dalili yeyote kama hii? tusijidanganye, bila kujazwa Roho kwa namna hii,hauna Mungu. na huwezi pata kama haujaokoka, na kama dini yako inabeza kuokoka manake wote kuanzia viongozi hadi muumini hamna Mungu, ila mna dini.

2. ROHO MTAKATIFU ANADHIHIRISHWA PIA KWA MATUNDA YAKE. ila hiyo haimaanishi kwamba hutakiwi kunena, unalazimika kujazwa ila tutajua kama bado amekaa ndani yako au ameshakuacha kwa kuangalia matunda yako. yapo Wagalatia 5:22.

3. Wakorintho 12 kuna karama za Roho Mtakatifu. 1Wakorintho 12, ndani yake tutajie ipi ulishawahi kuiona kwa padre yeyote, au mkatoliki yeyote (ukiondoa wale wachache karismatic).

mjadala umefunguliwa, leta hoja, hakuna matusi.
 
Uko sawa sana. Mimi ni mkatoliki na hili unalolisema nalielewa sana. Mambo yote yenye ushahabiano na nguvu ya Roho mtakatifu ni kama hayapewi nafasi katika kanisa letu. Mmoja alitangulia kuandika hapa miujiza haina maana. Sasa unajiuliza ni kwa namna gani utageuza mioyo ya wasio ifahamu nguvu ya Mungu usipotenda mambo makuu ya Mungu. Kwa kweli tukaze kuliombea kanisa maana ni wengi wanaangamia kwa kutokuamini nguvu ya Roho mtakatifu. Mathayo 13:58 utaona Yesu hakufanya mujica wowote nyumbani kwao kwa sababu hawakuamini. Nadhan sababu kama hiyo inaweza kuwa ndio sababu kwa nini hatuoni ishara kubwa na nyingi ambazo Roho mtakatifu anaweza kufanya kupitia watakatifu wake.
Kuna wakati naona kanisa limejikita kwenye doctrine za kanisa kuliko ukuu wa Yesu kitu ambacho kwa sehemu huenda tunamuudhi sana Mungu
dawa pekee kwa kanisa katoliki NI KULIKIMBIA, vua viatu vyako kama unaona vinakuchelewesha, kimbia hata peku mbio nyingi sana, ukibaki hapo hautakuja kumwona Mungu kamwe. kwasababu ni kanisa ambalo awali lilianza vizuri, lakini hapo katikati lilipokuja kuingiliwa na serikali likabadilisha kila kitu. ukichukua kanisa la mitume wale wa Kitabu cha Matendo weka upande huu, na upande ule weka kanisa katoliki (ambalo mnasema ni la mitume), compare and contrast, hakuna hata kimoja vinafanana.

1. Kanisa la kwanza hawajawahi kuomba kwa maria au wafu, waliomba kwa Jina la Yesu tu na ndilo agizo la Yesu, ila katoliki mnaomba kupitia maria na wafu. bado tu hamstuki?

2. Kanisa la kwanza ilikuwa lazima ujazwe Roho Mtakatifu, Yesu alisema huwezi peke yako bila Roho, na kweli huwezi kushinda dhambi au kufanya chochote cha Kimungu bila Roho, je? kanisa katoliki wanahubiri ujazo? wanajazwa? au wanasema hizo ni mambo za kilokole usiende nje ya katekisimo/litulgia ambayo iliundwa na wanadamu tu.

3. kanisa la kwanza, walifanya miujiza, sio kama ya manabii wa uongo, ni real. tuambie kanisa katoliki gani leo linafanya miujiza.

4. Kanisa la kwanza lilihubiri kuokoka, wokovu ni lazima, katoliki hawahubiri wokovu kabisa, na ukisema umeokoka unaweza kufukuzwa.

5. Kanisa la kwanza walihubiri wokovu ni sasa, saa ya wokovu ni sasa, baada ya kifo ni hukumu, katoliki wanaamini mtu akifa na dhambi unaweza kumwombea huko huko akasamehewa dhambi zake. nakuhakikishieni ingekuwa hio ni kweli Mungu asingeweka hata moto wa kuchomea watu wenye dhambi kwasababu nani asingemwombea ndugu yake asamehewe dhambi huko alikoenda? tusijidanganye,

6. kanisa la kwanza hawakuwahi kutumia masanamu au kuabudu masanamu,katoliki wanabusu na kusujudu masanamu ya maria na wafu wengine, kule kwa padre Pio watu hadi leo huwa wanaenda kuomba, na dunia nzima wanaomba, watu wameshika msalaba uliobandikwa mfano wa mtu wamwitaye yesu, au maria wanaomba, lozari ile inaombwa kwa akili wala si kwa roho kisanamusanamu. huu ni ushetani.

HAYO NI MACHACHE TU, HIVI KWELI UNAFIKIRI UTAENDELEA KUSALI HAPO, UKAMWONA MUNGU? NANI ATAKUONYESHA MUNGU ALIYEPO HUMO?
 
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Wakatoliki hata makanisa yetu yamejificha ukiwa na shida yatafute
Sembuse media
 
Tuhuma zako ni nzito sana ila andiko lako linahitaji maswali.Roho mtakatifu ni nini au ni nani?Je ili andiko lako uliloweka hapa umeongozwa na Roho mtakatifu?
ANDIKO nimeweka hapa nimeongozwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni Mungu, naomba Mungu akufungue ujue kwamba hata sileti tuhuma, natamani kila mtu ajue hicho nilichoandika kama ndio mapenzi ya Mungu. huo ndio ukweli halisi.

Yesu alipokuwa na waanfunzi wake, kabla ya kupaa aliwaambia hawezi kuwaacha yatima, atawaletea msaidizi, na aliwaambia wasitoke Yerusalemu hadi Roho atakaposhuka, na kweli siku ya Pentecoste wakiwa gorofani wakisubiri ahadi, Roho alishuka kwa watu kama 120 waliokuwa pamoja na mitume, wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo ndio wakaanza kusambaa na kuhubiri injili hata wewe walau ukaitwa Mkristo kutokana na hilo.

Roho Mtakatifu ni ahadi ambayo Mungu amewaahidia wote watakaomwamini, ukiona huja jitafakari yawezekana humwamini kisawasawa.
 
Back
Top Bottom