Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,765
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
 
hao wote ulio wataja ni wajasiriamali katika engo ya imani, lazima kila platform inayojitokeza waitumiekujulikana na kufikia wengi , katoliki hatuhitaji hivyo, mfumo wa sala na maombi na ibada inaenda kiliturigia huko kwenye redio na tv ambazo saa moja nyuma ilikua inaonyesha ufuska na saamoja mbele kusifu na kuabudu na Roho mtakatifu anashuka kweli na kujaza upako studio!
 
Uinjilishaji siyo kuhubiri tu.

Yakiwemo mahubiri; imani hujengwa na vitu vingi: sala, kwaya, historia ya Kanisa, kuelezea mafundisho mbalimbali, kujifunza maisha ya Watakatifu, n.k.

Haya yote utayapata Kanisani, kwenye media za Kanisa, Jumuia Ndogondogo za Kikatoliki, n.k. Imani ya Ukatoliki, na Ukristu kwa ujumla, haikujengwa kwenye miujiza na matangazo.

Infact Kristu alipotenda miujiza, ukiacha ule aliowaambia wakajioneshe kwa viongozi wa dini, mara zote aliwasisitiza wasimuambie mtu. Maana imani haijengwi kwenye miujiza, bali msalaba.
 
Ukristu upo kwenye msalaba. Wokovu wetu upo kwenye msalaba... Siyo miujiza na matangazo.
KITUO CHA PILI
Yesu anapokea msalaba

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Yesu anakubali kupokea msalaba kwa ajili ya wokovu wa watu. Ndivyo anavyonifundisha moyo wa sadaka, moyo wa kujitolea na kujisahau kwa ajili ya wengine.

Ee Yesu wangu mkarimu, mimi pia ninao msalaba wangu: jirani zangu, mwenzangu wa ndoa, watoto, wazazi wangu, kazi zangu, joto, baridi, njaa, kiu, vishawishi, magonjwa na matatizo mengine ya maisha, wajibu wangu kwa Mungu, kwa umma na kwa Kanisa.

Unipe ukarimu wako ee Yesu niyapokee bila kunung'unika, na kuyabeba vyema.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana utuhurumie W. Utuhurumie

Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.
 
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Umesema ukweli.

Dini zote saivi zimegeuka biashara. ndomanaa unasikia mchangonwa kwanza, wa pili, wa tatu, sijui mchango wa baba askofu mara mchango wa kitu gani sijui. Michango imekuwa mingi sana wanaibadilisha majina tu.

Pamoja na mambo ya msingi lazma watu lazima wachangamshwe.

Mm sio mtabiri ila nazan baada ya miaka fulani huko mbele hilo kanisa litakosa watu hasa vijana damu changa watakapo kujakushtuka itakuwa wamechelewa sana.
 
Back
Top Bottom