Wakati wengine wakila na kusaza

Wakati wengine wakila na kusaza

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,116
attachment.php

Wengine mboga ni ishu
 
Attachments

  • 1416639149947.jpg
    1416639149947.jpg
    11.4 KB · Views: 1,508
Ukiangalia pesa zinavochukuliwa na viongozi waweza toa machozi
 
Acha tu, nimehisi huzuni sana kama ningejua kilichomo nisingefungua kabisa hii
 
Acha tu, nimehisi huzuni sana kama ningejua kilichomo nisingefungua kabisa hii

Mlo huo ni mpaka kesho muda kama huo tena...!!!! Ukitafakari kwa makini hata kama uko kwenye starehe gani furaha yote hukatika
 
Mlo huo ni mpaka kesho muda kama huo tena...!!!! Ukitafakari kwa makini hata kama uko kwenye starehe gani furaha yote hukatika
Inasikitisha sana.

Mbaya zaidi wengine wanatupa tujitahidini kukiheshimu chakula, kama unaona hutoweza maliza jitahidi upakue/upakuliwe kile utakachomaliza sio kingi kisha haukimalizi. Au pakua chakula kidogo kama hautoshiba utaongeza kuliko kubakiza na kisha kukitupa.

Nashukuru wazazi wangu nimekuzwa kwenye mazingira ya kukiheshimu chakula
 
HARUFU wakati tukiwa chuo cha Kibuddha tulifundishwa kuwa chakula ni ibada! Huwa sisahau hii mada na imenisaidia mno na nimewasaidia wengi pia kuwaelimisha kuhusu chakula
 
Last edited by a moderator:
HARUFU wakati tukiwa chuo cha Kibuddha tulifundishwa kuwa chakula ni ibada! Huwa sisahau hii mada na imenisaidia mno na nimewasaidia wengi pia kuwaelimisha kuhusu chakula

Barikiwa Kiongozi.

Ndio maana tunaamrishwa kufunga bila shaka umeshafahamu lengo. Ila kwa faida ya wengineo pengine wapo wasio fahamu ngoja tuendelee kuwanufaisha.
Lengo la kufunga ni kutufundisha tuifahamu njaa pale unaposikia njaa kwa mtu mwenye fikra za kuwajali binaadam wenzio ndipo unapata funzo iwapo wewe kila siku unakuwa uifahamu njaa kaa ukijua wapo wenzako ambao hali ile unayoisikia wewe kwa masaa kadhaa wenzio wanakutana nayo katika maisha yao ya kila siku, ndio maana funga ni ibada kubwa sana.

Ngoja nikupe kisa changu kidogo, ni hivi- tulipokuwa watoto kulikuwa na kawaida mwisho wa wiki mara nyingi babu anawachukua wajukuu zake kutoka kwa wanawe, sasa tukishakutana kwa babu tunakuwa kundi, sasa ikifika muda wa chakula sisi watoto(wajukuu) tunakusanyika chakula tunawekewa kwenye sinia moja. Sasa kama ujuavyo watoto tena tunakula vizuri ikifika mwisho tunaanza kugombania chakula ilhali chakula bado kipo ni kiasi cha kumaliza na mnawekewa kingine. Sasa bibi yetu(mke wa babu akawa ameistukia ile tabia ya kugombania chakula mwishoni) Akawa anatutegea tukianza kugombania anakuja kisha anatuambia "tabia mbaya sana ya kugombania chakula" anachofanya anawaongezeeni tena chakula cha ajabu mkiongezewa mnabakisha akawa anatusimamia na bakora hiyo hata ushibe vipi hatowaelewa anataka lazima mmalize chakula.

Nikichanganya na maadili ya wazazi wangu baadae nikaja kugundua kumbe bibi alikuwa anatufundisha tusiwe tunachezea chakula
 
Inauma sana, huku mwingine anasema bill 371 mil ni za tobacco!
 
Yaani kwao ugari mkavu ni kama mkate,yanachekesha ila hayafurahishi.
 
Back
Top Bottom