Wakati Watanzania ‘ tukijidanganya ‘ kwamba Wachezaji wetu wa Serengeti Boys ni wazuri ‘ Mawakala ‘ bado hawajaona anayefaa.

Kila Siku huwa navikosoa mno kama siyo sana Vyombo vya Habari nchini Tanzania na hasa hivi vya Michezo kwa tabia yake ya Kupenda Kusifia vitu ‘ Kipuuzi ‘ huku vikiwajaza Watu ‘ Ujinga ‘ kinyume hata na uhalisia wake hali ambayo baadae huja kuharibu kabisa.

Wakati Watanzania nasi pia tukiingizwa katika ‘ Upuuzi ‘ huo huo wa hawa Wanahabari wa Michezo jana nilikaa na Mawakala wakubwa tu ambapo hadi mpira ule unamaliza hawakuona Mchezaji yoyote mzuri kutoka Serengeti Boys. Walichosema tu ni kwamba wengi wao wanajitahidi tu Kucheza mpira ila bado hawaujui Mpira.

Kuna Wakala Mmoja ndiyo alinimaliza kabisa na Kukubali kuwa kweli ' Wazungu ' huwa hawabahatishi na hawana ' Unafiki ' katika maelezo yao pale alipomchambua Mchezaji Mshambuliaji Kelvin John ambaye kwa Watanzania na hivyo Vyombo vya Habari vya Tanzania ' vinamtukuza ' kuliko hata Messi na Ronaldo kuwa hajui Mpira na anacheza mpira wa Jukwaani na siyo wa Kiufundi hali ambayo itamuwia vigumu kwa Yeye kupata Klabu kubwa huko Ng'ambo ( Ulaya )

Na ili muone kwamba hawa Mawakala hasa wa Kizungu huwa hawana ' Uswahili Uswahili ' wetu kama tulionao wakati Watanzania wengi tokea jana ' tukimlaumu ' Golikipa wa Serengeti Boys Mwinyi Yahaya kuwa ' alituchomesha ' hadi Kufungwa vile Mawakala wawili walisema kuwa kwa uzuri wa Timu ya Nigeria ulivyo kama kuna Mchezaji ambaye Kwao Wao jana alifanya vyema na alijitahidi basi alikuwa ni Golikipa huyo na wakasema kuwa ' Kiufundi ' ana Vitu vichache sana vya Kuongezewa ila huko mbele wakamtabiria kuwa atakuja kuwa Golikipa mzuri mno hapa Tanzania.

Baada ya Kauli hizi na Mitazamo hii ya hawa Mawakala wa Kizungu sasa nimeamini kuwa Watanzania wengi ( ukimuondoa GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ) ni Mashabiki tu wa Mpira ila siyo Watu wa Mpira. Na kwa tabia hii ya Vyombo vya Habari vya Tanzania kupenda Kusifia hata ' Upuuzi ' au vitu ambavyo sivyo vya Kiuhalisia Tanzania itaendelea kubaki hapa hapa japo mwaka huu Taifa Stars ' tumebahatisha ' tu Kufuzu AFCON nchini Misri baada ya Waganda kutuonea huruma na kuweka Ujirani mwema ila nina uhakika kama Uganda wangeamua ' Kukaza ' basi kama kawaida Watanzania AFCON 2019 tungeisikia tu katika ' Bomba ' huku tukiendelea na zile tabia zetu za Kuchagua Timu za Kushangilia na Mataifa ya Wenzetu.

Nawasilisha.
Wachezaji 6 walioachwa na kocha na kutuletea hii mizoga,walihusika kuleta kombe la cosafa ila wakachujwa kuiwakilisha taifa kisa hawana marefa huko tifuatifua acha tuendelee kupigika tu maana hatutaki kufuata weledi.

Huwa siamini katika kocha mzawa Tz maana ni sanamu tu anaamuliwa kila kitu.

Leo pale Taifa na Uganda kabadili kikosi hadi kipa,kipa mechi zote za, maandalizi alicheza leo hajawahi cheza,leo ilikuwa game yakwanza,kocha anayeijua kazi yake asingefanya changes golini,waleo alikuwa anatetemeka tu.

Tupigwe zote ili tufanye mambo kwa weledi
 
Serengeti wanahitaji kuwafunga Uganda tu j5 Hiyo ndio mechi muhimu kwao. Angola atafungwa nyingi zaidi na Nigeria hivyo sisi tutahitaji draw tu tukikutane naye mechi ya mwisho.

Hili kundi tunapita na world ndio tushaingia tunatambau kuna watanzania hawaamini uzuri wowote wa chochote kutoka Tanzania ila ndio hivyo sasa tunapita na World Cup ya vijana tunaingia.
Mkuu tupe mrejesho tafadhali
 
Back
Top Bottom