Wakati unatafuta hela kwa udi na uvumba kuna mwenzako amezitupa hela huko kama takataka vile

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,824
Inasemekana alionekana mtu akikuchunuku tu anakuita anakupa "mihela" basi watu wakafaidi hela waliofaidi. Wakatikea waja wema wakamsihi aachane na zoezi hilo maana huenda ingekuwa ni hatari kwa usalama wa maisha yake kwani watu walishaanza kusambaziana taarifa kuwa "kuna mtu anagawa mapesa hovyo huko mtaani"

Basi mtu yule ikawa hajaonekana tena lakini siku ya pili yake sijui ya tatu watu wakawa wanakuta mihela tu barabarani. Wakafaidi wale waliowahi asubuhi barabarani maana wapo waliookota mpaka kufikia laki tatu. Mwanzo ilionekana kama labda ni mtu tu ameangusha pesa zake kwa bahati mbaya lakini baadaye wakang'amua haikuwa bahati mbaya.

Waliokota hela watu katika mikoa mitatu tofauti katika barabara kuu iunganishayo mikoa hiyo. Sasa wanajiuliza kama ni yule aliyekuwa akigawa pesa au ni mwingine tu ila matukio yakaendana! Ajabu zaidi ni kuwa mtu huyo hakujulikana ni nani wala amepotelea wapi!!!

Siku njema
 
" ......... katika barabara kuu iunganishayo mikoa hiyo" hizi ni sadaka za kafara!
 
Naskia Kuna uganga unapewa dawa Kila asbuhi unakuta burungutu la mil.100,gheto ila the twist is inatakiwa siku kabla haijaisha usibakishe hata mia,na sharti lingine hutakiwi uwape ndugu zako,Kwa tetesi ni kwamba wengi wameshindwa Masharti ndani ya wiki.
 
Hahahaa kuna masharti ambayo yana kiwango cha matumizi kwa siku na aina ya matumizi, mfano kila siku 5M lazima itumike na iishe na kuna wigo wa matumizi ikiwemo kugawa pesa kiasi kadhaa. Hio ipo kila siku
 
Back
Top Bottom