Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

uta ni tag
 
Ila mlininanga jamani mweee.Hakuna marefu yasiyo na ncha jaribu lilishaisha.
 
Nimepandisha wazungu mlimani Kilimanjaro kama mgumu (Porter).. Nimefanya kazi ngumu nyingi duniani, lakin hakuna kazi ngumu duniani kama hiyo. Ndo maana wanaitwa wagumu.
Nikiwa huko enzi hizo unapewa mzigo wa kg 30 upandishe, hapo bado bag lako la nguo za baridi..hivyo unakuta unabeba kama 40 kichwani au mgongoni, na unatembea ukipanda mlima kwa masaa sio chini ya 8 kwa siku.

Nimeshuhudia wagumu wakifa njiani kwaajili ya njaa na mzigo. Mtu anatua mzigo anaegemea jiwe apumzike, ndo mazima anatangulia! Wengine wanakufa kwa baridi. Ule mlima umeua watu kibao sana, ukiwa unapanda utaona tu sehemu kibao watu wamekusanya mawe, ujue hapo mtu alikufa. Sasa hizo ni nyingi sana. Kuna wakati unanyeshewa mvua mwanzo mwisho, unaloa na kadri unapanda ndivyo baridi inaongezeka. Unafika camp site jioni umeloa, na ni baridi kali, na nguo hadi za kwenye bag zimeloa.

Kupanda mlima kwenyewe ni kugumu balaa.. hasa ukipitia machame route, upo na kilo 40 begani na unapanda vigongo vya ghafla vya kutosha.. kweli ile kazi ni ya wagumu, nimeshuhudia hawa wanajeshi mnaowaamini, wakichemsha kupanda mlima ule na vibeg vyao vya kg 20. Naamini kama serikali wanataka kweli makomando wa ukweli wanatakiwa waka recruit wagumu wa mlima Kilimanjaro. Wale ndo wagumu kweli kama jina lao linavyojulikana. Duniani hakuna kazi ngumu zaidi ya "ugumu".

Afadhali siku hizi serikali imeweka msisitizo kupima mzigo usizidi kg 20, zamani ulikuwa unapigwa hata kg 40, na unatakiwa utembee zaidi ya km 30 kwa siku, na ongezea bag lako mgongoni. Unatembea umeelemewa na mzigo kwa masaa na masaa mpaka unajiuliza umemkosea Nini Mungu? Au hiyo ni adhabu unapewa hapahapa duniani?Unakuta mwamba unatembea masaa zaidi ya 8 una kg 55 mwilini. Ndo maana wanaume wengi wa mikoa ya kaskazini ni watu wagumu kwasababu wengi wamepitia hii kazi au za kuchimba madini Mirerani, ambayo ni ngumu lakin haifiki ugumu wake kwa hii hata nusu. Na inatakiwa utembee uwapite wazungu njiani, wakifika kambini wakute mmeishapigia matent yao ya kulala na kuwapikia chakula. Siku zote wa kwanza kuamka, mwisho kulala. Noma sana ugumu.


WAGUMU
 
nimecheka sana kaka japo siyo mazuri
 
Duuuhh kweli sio paoh
 
Hakika wagumu ndio wanaodumu
 
Uliwahi kusomoa wewe alafu unageuka na kiroba usiku kucha
 
Hope Ulipata mzungu maisha yakaendelea
 

Stori yako imefanana vile vile na yangu.

sasa sisi ilikuwa godown la tumbaku
tunabeba magunua ya tumbaku.

Nilimwambia msimamizi kuwa hiyo kazi naiweza na ni baada ya kuona vitoto vinabeba.Nikaambiwa kesho njoo uanze kazi.

La haula mzee siyo poa nilitwishwa gunia la kilo 90 begani unapandisha ngazi kupakia fuso trip 3 nkasikia kiuno na miguu vimeseparate, nkashindwa huku naona wale madogo mpka wanakimbia na mizigo kama hawana akili.

Nkahamishwa kweny mizani kazi yangu ni kupima gunia ili karani abebe halafu ipakiwe kweny fuso, huko guni la kilo 70,80,90,100,110 mnatakiwa kulibeba na kulipima mnakuwa wawili mnashikizana ila mnatakiwa kuwa na speed ya 5G ili wale wabebaji wasisimame,

nakumbuka niliingia saa 2 asubuhi, kufika saa 3 nikaanza kuwaza namna ya kukimbiaa.

Nguo kwenye begi slipa mkononi na tumbaku kichwani nanuka kama sigara nduki ghetto.

Siku 3 mwili unauma ni mwendo wa panadol na diclopar.Nikaiheshimu elimu, nikaona bora ntembeze CV tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…