NMB Tanzania
Official Account
- Sep 13, 2014
- 94
- 232
Huyu mzungu wa NMB kaiboresha sana benki hiyo, kutoka kwenye benki iliyokuwa na huduma duni , foleni kutoka hapa na masaki, majengo mabovu lakini sas hivi hakuna foleni, majengo yameboreshwa ni ya kisasa kabisa na wanafanya open office systerm ambapo kuanzia meneja mpaka watendaji hawajajifungia mavyumbani wapo wazi wanaonekana jinsi wanavyo fanya kazi. Hakuna kutegea. Wamejiunga na VISA hivyo fedha unachukulia popote, wana ATM za kutosha na wanafungua matawi kila mahali, huku magari yao ya mobile bank yaizunguka vijijini. Bank zingine zikae chonjo
Hello Wanajukwaa,
Asante sana Avogadro kwa kutambua jitihada zinazochukuliwa na viongozi wetu hapa NMB, ni faraja kwetu kuskia kuwa juhudi zetu zinatamalaki kila kona na kuwanufaisha Watanzania wengi zaidi kwa kwa kupitia maboresho ya huduma na bidhaa zetu. Pia bila kusahau salaam zako tutazifikisha kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi Ineke Bussemaker
Tunaendelea kuweka mipango na mikakati thabiti kuweza kuwafikia na kuwafikishia huduma watanzania wengi zaidi ili waweze kuingia kwenye mfumo rasmi wa kifedha na kunufaika na huduma za kibenki hasa ukizingatia matumizi sahihi ya teknolojia.
Endelea kuwa pamoja nasi na tusaidie kuwafikishia habari watanzania wengi zaidi kuwa sasa wanaweza kujiunga na benki yao kupitia kiganjani tu kwa kutumia *150*66# na kufungua akaunti kwa urahisi zaidi au kutumia NMB KLIK App inayopatikana iOS Store na Google Play.
Tunaendelea kuwa karibu yako zaidi #NMBKaribuYako