Wakati umefika kuigawa CRDB Bank

Wakati umefika kuigawa CRDB Bank

CRDB benki tatizo ni management wamefungua vibranch vingi lakini ufanisi zero.,,ndio shida ya ajira za kindugu
Kuna siku nilienda bank ya crdb tawi la buzuruga. Atm zilikua hazifanyi kazi, tulikaa pale kwa muda kama saa nzima. Kwa pembeni kwenye parking ya magari yao tuliona jamaa mmoja hivi mrefu mwembamba, sijui ndio manager au mfanyakazi wa kawaida. Tulimuiliza tatizo nini, tupo muda mrefu hapa atm hazitoi fedha?

Alitujibu kwa nyodo kubabake akaendelea kuongea kwa simu yake.
 
Watz kwa ujumla bado tunajikokota.
Crdb mlikuwa mnafanya vizuri lakini mara ya mwisho Msasani branch mliniangusha. Kuna watu niliuliza wakasema tawi hilo ndo zao. Uongozi mliangalie.
Issue ya ukabira isipuuzwe maana mteja akihisi hivo tayari inakula kwa benki.
 
Ila tawi la Kijitonyama lilikuwa linanibariki sana hasa tailer Dina. Sina hakika kama bado yupo
 
Na nyie Watanzania wa NMB Tanzania mlioko karibu na huyo mzungu mjifunze uwajibikaji na jinsi anayofanya kazi ili akiondoka mchukue nafasi na mlisongeshe kama huyo mama.

Maana tumezoea kampuni/taasisi/kiwanda ikiwa inaendeshwa na mzungu, akiondoka na kukabithiwa mwafirika inakufa hapo hapo.

Waafrika sijui tuna shida gani.
 
Hii bank kwa kweli ina huduma mbovu sana. Juzi juzi nimejaribu kufungua account pale, kwanza wana fomu nyingi na complications zisizoisha. Siku 3 nazungushwa tu, nikaenda NMB ndani ya nusu saa nimemaliza.

Na ukishafungua account na hawa CRDB bado kuna matatizo mengi sana unakumbana nayo na account yako na huwa wanakuwa hawana msaada sana. Nasema hayo kwa sababu tayari nina account nyingine pale na ni kama nimeikacha. Hata ukiwa pale tu utaona idadi kubwa ya wateja wao wanaokuja na kuondoka bila matatizo yao kutatuliwa.

Naona hii benki inaenda au inastahili kugawanywa kama NBC ya wakati ule iliyozaa NMB. Tunaambiwa tupende vya kwetu ila inaonyesha hadi aje mzungu ndiyo huwa tunakaa sawa na kutoa huduma zinazoeleweka.

Najua hili linaweza lisitokee kwenye utawala wa Magufuli kwa sababu sera na mitazamo yake ni tofauti sana na Mkapa ila hii benki inabidi imulikwe.

Na samahani kama kuna nitakayemkwaza ila kuna element ka ukabila pia kwenye ile benki. Naona kama wafanyakazi wengi katika matawi niliyowahi kwenda ni watu wa kutoka sehemu moja!! Sijui kama hilo litakauwa linachangia matatizo waliyonayo ila niliondoka nikijiuliza maswali mengi ambayo sijapata majibu. Kwanza inawezekana wanachukua fomu za watu ambao mwisho wa siku wanaamua kutoendelea na application au hata kufanya makusudi zangu wanaweza wakawa wanakatisha tamaa watu wenye account halafu wanatumia hizo account au information za watu kuchukulia mikopo bila wateja wenyewe kujua? Je hili linawezekana? Nimefikia kujiuliza maswali kama hayo kwa sababu ufanisi wao ni wa mashaka sana.
Kimei mdo tatizo kwa benki hiyo. Aliifanya kuwa benki yake na wapambe wake...
.
 
Mkuu mfikishieni salam huyo mkurugenzi
Pia napenda kutoa pongezi kwa tawi lenu la Mwanhuzi wilaya ya Meatu.

Kuna Jamaa pale ni bank Teller, mwembamba na mweupe sana.

Aisee, nina accounts benk 3, NMB, CRDB na Diamond Trust.

Lkn ktk bank zote na Branch nilizowahi pata huduma sijawahi pata customer care nzuri kama ya yule jamaa.

Kwanza jamaa anaioenda kazi yake, anasikiliza kila mtu.

Hachoki kukuhangaikia kutatua shida yako.

Kiukweli nilitokea kupenda utendaji kazi wake.

Jina lake silifahamu ila kila mwezi naonaga anashinda kuwa mfanyakazi bora.

Ni mweupe sana na mwembamba.

Salam zimfikiee.

Zimefika mkuu na asante kwa mrejesho kutoka tawi lenu la Mwanhuzi wilaya ya Meatu.

Tunaendelea kuwa karibu yako zaidi
 
Hivi NMB mna online payment options like mtu akitaka kuunga na PayPal or kufanya direct online purchases?
Salaam Ndugu,

Ndio huduma hiyo ipo, karibu katika tawi la karibu yako tukuwezeshe kupata huduma hiyo.

Asante sana
 
Katika dunia ya leo kufungua bank account kinatakiwa kuwa tendo la dakika zisizozidi 10, na tena ni kitu unachoweza kufanya online.

Kuna hii kasumba imejengeka katika wafanyakazi hasa sekta ya umma ya kudhani ufanisi unapimwa kwa kiasi gani unasumbua na kuwatilia ngumu wateja/wananchi na kuwapa wakati mgumu badala ya kutatua matatizo yao haraka iwezekanavyo. Hilo ndiyo inabidi iwe kipaumbele na kama kuna kasoro zozote katika rekodi au documents zake unakuja kuzitatua baadae. Kuna wakati wanatumia visingizio tu kwa sababu wamepotoka, hawajui majukumu yao ni nini hasa. Inabidi kweli tubadilike.
Naam Keynez,
Ndio maana NMB tumelitambua hilo na sasa huna sababu ya kutokuwa na akaunti ya benki. Ukiwa na simu yako ya mkononi tayari una huduma za kibenki wakati wote. Jiunge sasa kwa kupitia *150*66# au pakua NMB KLiK App kwa iOS na Android ujiunge na ulimwengu wa mfumo rasmi wa kifedha.
Asante sana
 
Counter nyingi ziko empty mabinti ni kupiga story tu na kuzurura tu wanauza sura
 
Kuna huu mchezo wa bank kuifunga account yaani nimewaachia elfu sitini zangu exim nilitakwenda crdb lakini nikaona bora tu nitulie na bank moja sasa bank yangu ni mpesa na NBC japo huduma zao si za kuridhisha nitasonga nao hivyo hivyo
 
NMB ni bank ambayo naikubali sana mbali na kuwa na changamoto ndogondogo ila hii NMB ni nzuri sana maana wao kitu kinacho wezekana leo lazima wakikamikishe leo. (Just forget about personal weaknesses) wako vizuri sana(NMB KARIBU YAKO) CRDB inazidi kuwa ya hovyo kila uchao japo miaka ya nyuma ilikuwa nzuri sana ila sasa hivi kuna mdudu anawavuruga tu hawajielewi tena.
 
Bank la hovyo hilo niliwaacha tangu mwaka 2017, na niliwatabiria anguko lao palepale tawi la Mbagala. Nilichofanya ni kutoa visent vyangu Sim Banking na kuhamishia NMB.



Ila Bank ni hizi international Bank tu.
 
Write your reply.
NMB Tanzania naomba kuuliza hivi ukitaka kubadili NMB mobile kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine inawezekana? mfano nataka kubadili kutoka voda kwenda halotel
 
Back
Top Bottom