Wakati tunasonga ugali wa SGR na JNHPP, tusimwage viporo vya jana

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,037
9,953
Kuna miradi mingi ilianzishwa awamu ya nne na baada ya awamu ya tano kuingia iliachwa kiporo kwanza. Ipo iliyokuwa na kasoro za kiutekelezaji na ipo iliyosimama kwa mapungufu ya kifedha na ipo iliachwa kwa changamoto mbalimbali, naamini kuna sababu za msingi zilizopelekea kuachwa. Lakini sio vizuri kuitelekeza wakati fedha nyingi zilishainjikwa mle.

1. Mradi wa ujenzi wa mji mpya Kawe; Huu mradi chini ya NHC ulikuwa uwe na vitu vizuri ikiwemo makazi bora, ulianza awamu ya nne na kusuasua awamu ya tano ni vyema tukaangalia namna gani tutauendeleza. Nakumbuka tulikopa fedha ndefu kutoka Exim Bank china, naimani chenji bado ipo yakumalizia huu mradi.

2. Dege Eco village; huu mradi ulianza kwa speed sana awamu ya nne, awamu ya tano ukashikwa break, hebu turekebishe kasoro zilizopo mradi uendelee, zipo fedha za investors, developers za wanachama wa nssf, kuuacha ufe natural death ni kukatisha tamaa shughuli za uwekezaji, naamini hili linazungumzika na linaweza fikia mwafaka.

3. Hotel ya nyota tano ya NSSF Mwanza; huu mradi bora ukamaliziwa fedha za wanachama zianze kurudi, watu wanahangaika kupata mafao yao wakati wanaliona jengo liko pale limetelekezwa na limekula hela ndefu. alternatively liuzwe tu tujenge nyumba ndogondogo zitakazo pangishwa/kopeshwa kwa wanachama wa nssf.

4. Ujenzi wa nyumba za makazi za NHC, wakati wa awamu ya nne NHC walianzisha mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi mikoa yote, japo hii miradi ilikuwa ya kishenzi shenzi huku watu wakiuziwa nyumba ya chumba na sebule 49m, turekebishe kasoro zilizopo na miradi iendelee. Mfano mji wa Geita una changamoto za makazi kutokana na shughuli za uchimbaji madini lakini tukaweka tena makao makuu ya mkoa wa Geita, isitoshe tukaanzisha tena halmashauri ya mji wa Geita, shughuli zote hizi zimepelekea watumishi wapya kuhamia Geita wakati hakuna mkakati wowote kuhakikisha makazi ya watumishi yanapatikana.
 
Hakuna cha standar Gauge wala Bwawa la Nyerere.

HII NI MIRADI HEWA JIWE ALIWADANGANYA.
HAIKAMILIKI LEO WALA KESHO.

Moja kati ya Characteristics za Project.
1. ni lazima mradi uwe na Duration specific plan ya ku start na end mwisho wake.

SGR NA Bwawa la nyerere havina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom