Wakati tukisubiri vita kubwa sana kati ya Iran na Marekani

tubalayya

Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
69
Reaction score
105
Kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nielezee kwa kifupi sababu halisi za vita hivi, ili mtu akijitia upumbavu iwe ni shauri yake. Maana kuna watu tayari wamejazwa punzi kuwa Iran ni magaidi, wasiotaka maendeleo, wanaotaka kuuangamiza Ufalmu wa Mungu wa Israeli, na... 'malakia' mengine!

Iran ilifanya mapinduzi ya Wananchi mwaka 1979 na kufanikiwa kumwondoa mfalme aliyekuwa kipenzi cha Marekani, Shah Mohammad Reza Pahlavi. Shah (Mfalme) alikuwa nambari 1 Mashariki ya kati kwa kupendwa na Marekani kuliko hata Israel, Turkey au Saudi Arabia hivi sasa. Kama unavyoiona Israeli hivi sasa ilikuwa Iran.

Tukio la kupinduliwa Reza halikuipendeza Marekanai na kwa kweli lilikuja kama kustukiza kwani Marekani haikufikiria hata siku moja hilo lingewezekana. Kama unavyojua katika serikali vibaraka wananchi hawa patilizwi, na ndivyo ilivyokuwa hivyo Iran. Mapinduzi yalikuja kama tija ya umaskini katika nchi iliyokuwa nambari 1 kwa kuuza mafuta nje.
Fast Forward....chuki zilianza mara moja. Marekani ikijaribu kumrudisha Shah na Wairan, wote wakati huo, wakipinga. Ndipo Ayatollah Khomaini akaamuru Wanabalozi wa Marekani wazuiwe kuondoka nchini ili wawe kama dhamana ya kutotokea mapinduzi. Jambo hili lilipandisha mori wa Marekani na chuki. Tangu siku hiyo Marekani ikaiwekea vikwazo Iran hadi leo!
Kinyume na wengi walivyodanganywa, Ayatollah Khomeini alisimika Jamhuri ya Kiislamu baada ya kura ya maoni 1979, ambapo mfumo wa Kiislamu, Islamic Republic, ulikubaliwa na wengi kwa kura ya maoni ya asilimia 98.2. Hii ilikuwa kura ya wazi, huru na amani kabisa katika Mashariki ya Kati kuwahi kutokea, hata kushinda kura za Israel na Uturuki (zinazosifiwa kuwa na demokrsia), kwa mujibu wa UN wakati huo.

Wamarekani waliposhindwa kumrudisha Shah mapema, wakasuka mpango wa kumshawishi rais jirani wa Iraq, Saddam Hussein, kuishabulia Iran, angalau waweze kuiangusha Jamhuri changa kwa vita. Hilo halikufanikiwa, na kwa miaka 8 iliyofuata vita ikapiganwa. Kwanza Wairan walikuwa wanyonge, waliwekewa vikwazo vya kununua silaha na nchi zote, hata risasi! Hata na Soviet Union, nchi iliyojitambulisha kwa kuwatetea wanyonge na wanaokandamizwa!
Ila kutokana na akili, vipaji na ubunifu wa Wairan, kidogo kidogo wakajitengenezea silaha hadi ilipofika 1985 wakakomboa ardhi zao zote, bali wakaingia Iraq! Kumbuka, nchi zote za Kiarabu zilikuwa zikiisaidia Iraq kwa mabilioni. Ni Syria na Libya pekee waliomwunga mkono Iran, zaidi kwa maneno.
Ni katika kipindi hiki ndipo Iran ilipoanza kujijengea viwanda mbali mbali hasa vya silaha baada ya kupata fundisho baya.
SUALA LA NUKLIA
Hili ndilo suala ambalo Marekani inasema inaingia vitani kwa ajili yake.
Ni hivi, kwanza kuna tofauti baina ya silaha za nuklia na nishati ya nuklia. UN, baada ya kuona maafa makubwa yaliyosababishwa na Mabomu ya nuklia yaliyoangushwa na Marekani kule Nagasaki na Heroshima Japan mwishoni mwa vita kuu ya pili, iliweka taratibu kufanya Mataifa yote mengine yasiyokuwa bado yameunda silaha za nuklia kufikia mwaka 1950, wazuiwe kabisa kuundfa silaha hizo, lakini wapewe ruhusa ya kufaidika na nishati za nuklia, kwani nishati hizi zinaweza kutumiwa katika matumizi ya amani kama kufua umeme, madawa, kilimo na safina ziendazo chini zaidi baharini au kwenye anga za nje nk.

Hadi hapo ni Marekani, Urusi, China, France, Uingereza ndiyo zilizokuwa na silaha hizo pekee, Baadaye wengine wakazipata kinyemela, Israel, India, Pakistan na Korea ya Kusini (Hiyo ni hadithi kando).

Ili kuratibu utumiaji wa nishati za nuklia, mwaka 1968 wakaunda NPT, Nuclear non Proliferation Treaty, Yaani Mkataba wa Kuzuia Kusambaa kwa Silaha za Nuklia.
Kwa mujibu wake, nchi inayotaka kutumia nishati ya nuklia kwa mambo ya amani, labuda kwanza wajiunge na NPT, waahidi hawatatengeneza silaha, na pia vinu na mitambo yote ya kufulia nishati hiyo viwe chini ya udhibiti na uchunguzi wa mara kwa mawa wa Shirika hili NPT.
IRAN INABAGULIWA
Program ya nuklia ya Iran ilianza tangu wakati wa Shah ambaye alisaini NPT mwanzoni kabisa 1968. Marekani hasa ndiyo iliyomjengea Shah mitambo miwili ya mwanzo ya nuklia bila nongwa. Iran ilikuwa inanunua madini ya Urani au Kinywe kutoka Marekani bila matatizo yoyote, kwa ajili ya kutengeneza madawa hasa ya Kansa.

Tatizo likaanza kujitokeza wakati Serikali mpya ya Kiislamu, mwaka 1990, ikataka kununua mzigo kutoka Marekani kwa ajili ya wagonjwa wake. Wakati huo Iran ilikuwa na wagonjwa wasiopungua 40 elfu wa Kansa. Malimbikizo yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi yalikuwa yamekwisha. Lo! Hammadi. Marekani, ikakataa kuuza urani kwa Iran, ingawaje hili ni kinyume cha Sheria za Kimataifa na NPT! Zaidi ya hivyo, kila Iran ilipokwenda kutafuta nchi nyingine, kama Brazil, Argentina, Japan....walikuta katazo la Marekani wasiuziwe!
Ungefanyaje kama wewe ni kiongozi wa nchi yako? Hapo ndipo Iran ilipanza fikra ya kuweza kutengeneza enrichment (kutakasa) yenyewe.
Kama nilivyokuambia, Wairan ni watu wana akili za ajabu sana. Lakini pia, kitu cha kwanza Serikali ya Kiislamu kukitilia mkazo ilipofika madarakani ni elimu. JHakuna kazi nzuri Iran kama mwalimu. Serikali imefungua vyuo vya viwango vya nchi zilizoendelea na zaidi. Hivi tusemavyo, kila mwaka wanafunzi wa Iran ndiyo wanaochukua namba 1, 2 katika mashindano ya Hesabati duniani (World Maths Olympics). Vyuo Vikuu vinne vya Iran ni kati ya 10 vinaongoza duniani katika Engineering!
Kifupi...wakaweza kujifanyia wenyewe enrichment...kurutubisha madini ya kinywe! Wamarekani macho yakawatoka, hawakuamini kamwa Wairan wenyewe wangeweza kufanya enrichment! Ni elimu ambayo hata nchi kama Italy, Spain, Sweden etc bado hawajafika!

MIZENGWE YA MAREKANI
Kwa kutaka kuzuia maendeleo ya Iran, Marekani ikishakizwa na Israel, ikaanza kuchochea kwamba Iran ina nia ya kutengeneza silaha za nuklia, ingawaje Iran imetia saini ya kutotengeneza silaha hizo, bali na Kiongozi wake wa Kidini Ayatollah Khomeini alitoa fatwa kwamba kutengeneza silaha kali za kuuwa binadamu kwa jumla bila kuchagua ni marufuku katika Uislamu.

Marekani imeshikilia Iran ina nia ya kutengeneza silah! Baya zaidi, marafiki wa Marekani, kama Israel, ina silaha za nuklia hasa na imekataa kutia saini ya kudhibiti silaha hizo....lakini Israel ndiyo hasa iko mbele katika kuisakama Iran ambayo haina!
NPT iliibana Iran kwa kuipa masharti magumu zaidi, mfano wawe waweza kutembelea mitambo yote bila hodi na bila kutoa taarifa.... Iran ilikubali hiyo ingawaje haikuwa lazima, lakini havijawaombea!

Kama unajua dunia vizuri, basi utajua kuwa Marekani ni koloni la Israel na kwa hiyo inafanya kila inaloamriwa na Israel, ikiwemo vita hii ijayo.
Israel haitaki kuona nchi yenye nguvu inayoshindana nayo. Na sababu kuu hasa ni kwamba inaogopa kwamba kukiwa na dola linaloweza kusikizwa duniani, hatimaye dola hilo litakuja kuilazimisha Israel kuwapa Wapalestiona sehemu zao ilizoziteka mwaka 1967 kwa mujibu wa UN.
Sehemu hizo, kama Gaza na Ufukwe wa Mashariki wa Mto Jordan, Wayahudi wanadai Mungu wao aliwakabidhi wao, miaka 3,000 iliyopita! Sisi tuliouliza tuone Hati hiyo Miliki ya Mungu....bado twasubiri majinbu. Ila baadhi ya madhehebu ya Kikristo huunga mkono hilo, Huko Marekani, Wakristo hao ndiyo wanaoshinikiza serikali yao juu ya kuisapoti Israel hata kinyume na sheria za Kimataifa!

Utaona ingawaje kuna udini fulani katika vita hivi kwa mtazamo wa Israel, lakini kwaa mtazamo wa siasa za dunia yetu ya sasa zinazosimamiwa na misingi ya haki na sheria....hii ni vita ya mbabe mwenye silaha kubwa kumkanyaga mnyonge. Might is right!
 
Trump alianza na nitavuruga Iran kwenye uso wa dunia
Baada ya Putin kutia timu
Ameaanza tushambulia kwa kiasi, na muda si mrefu itakuwa tumewasamehe huku akiufyata mkia

Israel na US wote hawana hypersonic missiles...
Unaweza imagine nchi iliyowekwa kwenye vikwazo kwa miongo mitano wanatengeneza hypersonic na kurutubisha urani.

Wanatengeneza Air defenses zao , radar, Wametengeneza shaheed drones ambazo Russia ame copy na anazitumia kwenye vita yake na Ukraine, US na yeye ame copy anatengeneza sasa shaheed drones akiziita LUCAS, Russia wanaziita Geran kama sijasahau...

Waajemi ni watu wenye akili... hata jinsi wanavyoendesha mikakati yao kivita na strategies si watu wa mchezo, wamewa out smart Israel...
 
Umeaandika uwongo mwingi sana mkuu.

Usitumie udhaifu wa watu kutofatilia mambo kuwadanganya.

Mfano mdogo tu wa uwongo wako ni kwamba Iran ndio imekuwa ikiongoza kwenye mashindano ya hesabu kila mwaka.

Huo ni uongo, anayeongoza kitakwimu ni China,

Iran haiisogelei hata kidogo nchi Kama Vietnam.

Rekebisha mada hii iliyojaa uongo.
 
Mi mwenyewe naelewa hii ni Ze Comedy...

Trump anasogeza hayo mameli sijui yanakwenda kufanya kazi gani hapo, hizo meli ni za kutishia nchi za ulimwengu wa tatu, kwa nchi zenye tech hizo meli si chochote, hayo siku hizi wanatumia kama deterrence tu...

Hadi sasa sielewi US ina lengo gani, maana position ya hizo meli ni ndan ya range ya missiles za Iran... na hizo carriers pamoja na meli zake zinazoilinda hazina uwezo kuzuia hypersonic...

Ninachoona hapo kituko.. tusubiri lakini..
 
Huyu ng’weng’we Echolima1 lazima akuibukie kwa hii komenti
 
Ali Hosseini Khamenei siku zake zinahesabika.

Marekani imeendelea kufanya build-up kubwa sana ya kijeshi katika Middle East kwa siku za hivi karibuni bila kuvutia attention au kutengeneza headlines za kimataifa. Ni hivi karibuni tu Vladimir Putin alikiri kwamba linapokuja suala la media propaganda, huwezi kuishinda USA. Sasa hivi international headlines nyingi zinaongelea masuala ya Greenland, Epstein files, na kauli za Donald Trump kuhusu Gaza Board of Peace, huku Marekani ikiendelea kuimarisha build-up ya kijeshi Middle East. Kuna jambo linaonekana kuandaliwa katika Mashariki ya Kati, hasa kwa Mzee wetu Khamenei.
 
Mi mwenyewe naelewa hii ni Ze Comedy...

Trump anasogeza hayo mameli sijui yanakwenda kufanya kazi gani hapo, hizo meli ni za kutishia nchi za ulimwengu wa tatu, kwa nchi zenye tech hizo meli si chochote, hayo siku hizi wanatumia kama deterrence tu...

Hadi sasa sielewi US ina lengo gani, maana position ya hizo meli ni ndan ya range ya missiles za Iran... na hizo carriers pamoja na meli zake zinazoilinda hazina uwezo kuzuia hypersonic...

Ninachoona hapo kituko.. tusubiri lakini..
Lengo la USA ni kuipiga Iran mbona ipo wazi sana hiyo haitaji rocket science.
 
Taarifa yako ndefu imepoteza lengo kwa kuweka mambo mengi yasiyohitaji maelezo au kuwa ndani ya mada.
1. Inachosha kusoma
2. Umechagua waziwazi upande unaotetea
3. ndiyo, ni kweli hao wanaopeleka vita huko wanazo sababu zao, na si lazima kama ulivyozieleza wewe
4. hebu jaribu tena kueleza kwanini Cuba nchi nzima wamewekwa jela gizani, na Venezuela Je, unayo maelezo juu yake?

Mada hii hukuitendea haki.
 
Israel na US wote hawana hypersonic missiles...
Unaweza imagine nchi iliyowekwa kwenye vikwazo kwa miongo mitano wanatengeneza hypersonic na kurutubisha urani.

Wanatengeneza Air defenses zao , radar, Wametengeneza shaheed drones ambazo Russia ame copy na anazitumia kwenye vita yake na Ukraine, US na yeye ame copy anatengeneza sasa shaheed drones akiziita LUCAS, Russia wanaziita Geran kama sijasahau...

Waajemi ni watu wenye akili... hata jinsi wanavyoendesha mikakati yao kivita na strategies si watu wa mchezo, wamewa out smart Israel...
Hizi hypersonic ballistic missiles; kama Oreshnik zitakuja kufanya nuclear missiles kuwa obsolete; kwa maana kwamba hadi hapo kinga dhidi yake itakapopatikana, hakuna haja ya kukimbilia nuclear ; kwa sababu zinasababisha uharibivu wa maeneo yaliyolengwa bila ya pingamizi lolote

System inarushwa angani, ikishuka inayo mishale minne au sita na kila mmoja umelenga eneo tofauti; na inauwezo wa kubadili mwelekeo. ikidondoka ilipolengwa joto la centigrade 4000 linaunguza kila kitu!

Kwa nini utumie nuclear na kupata laana bure!
 
Waisrael wainataka middle east yote , kikwazo ni lran . Vita ni Kwa maslahi ya israel.
Sasa tunamtaka trump achukue hatua ili tumalizie kipande kilochobaki asipo fanya hivyo mafile ya upstein yata wekwa wazi na Siri za Donald na marafiki zake WA maga zitajulikana. LGBT 🌈 foreva .
ujue world order ina Toka Israel marekani anafuata tu maagizo
 
Nimekukubali! Si hawa wengi 'wasiochanganya na zao'!
 
Umeaandika uwongo mwingi sana mkuu.

Usitumie udhaifu wa watu kutofatilia mambo kuwadanganya.

Mfano mdogo tu wa uwongo wako ni kwamba Iran ndio imekuwa ikiongoza kwenye mashindano ya hesabu kila mwaka.

Huo ni uongo, anayeongoza kitakwimu ni China,

Iran haiisogelei hata kidogo nchi Kama Vietnam.

Rekebisha mada hii iliyojaa uongo.
Pengine kuna takwimu sikuzicheki zaidi kutokana na muda, hasa katika mara Iran walizoshinda Olympiki hizi. Ila ni uwongo kusema mna uwongo mwingi humu. Orodhesha!
 
Trump anasogeza hayo mameli sijui yanakwenda kufanya kazi gani hapo, hizo meli ni za kutishia nchi za ulimwengu wa tatu, kwa nchi zenye tech hizo meli si chochote, hayo siku hizi wanatumia kama deterrence tu...
Ungekuwa umepitia mgambo tu ungeelewa kwa nini Trump anafanya hivyo lakini wewe raia wa kawaida huwezi kuelewa chochote maana ni Mbumbumbu katika mambo ya kijeshi.
Hadi sasa sielewi US ina lengo gani, maana position ya hizo meli ni ndan ya range ya missiles za Iran... na hizo carriers pamoja na meli zake zinazoilinda hazina uwezo kuzuia hypersonic...
Utaelewa nini wakati wewe ni zuzu tu!,, Leo hii usiku kaa karibu na TV yako ndipo utajua nini wanaenda kufanyiwa wafadhili wa magaidi huko Mashariki ya kati!!
 
Waisrael wainataka middle east yote , kikwazo ni lran . Vita ni Kwa maslahi ya israel.
Sasa tunamtaka trump achukue hatua ili tumalizie kipande kilochobaki asipo fanya hivyo mafile ya upstein yata wekwa wazi na Siri za Donald na marafiki zake WA maga zitajulikana. LGBT 🌈 foreva .
ujue world order ina Toka Israel marekani anafuata tu maagizo
Endelea kuwadanganya Mazuzu wenzako!!!
 
Kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Nielezee kwa kifupi sababu halisi za vita hivi, ili mtu akijitia upumbavu iwe ni shauri yake. Maana kuna watu tayari wamejazwa punzi kuwa Iran ni magaidi, wasiotaka maendeleo, wanaotaka kuuangamiza Ufalmu wa Mungu wa Israeli, na... 'malakia' mengine!

Iran ilifanya mapinduzi ya Wananchi mwaka 1979 na kufanikiwa kumwondoa mfalme aliyekuwa kipenzi cha Marekani, Shah Mohammad Reza Pahlavi. Shah (Mfalme) alikuwa nambari 1 Mashariki ya kati kwa kupendwa na Marekani kuliko hata Israel, Turkey au Saudi Arabia hivi sasa. Kama unavyoiona Israeli hivi sasa ilikuwa Iran.

Tukio la kupinduliwa Reza halikuipendeza Marekanai na kwa kweli lilikuja kama kustukiza kwani Marekani haikufikiria hata siku moja hilo lingewezekana. Kama unavyojua katika serikali vibaraka wananchi hawa patilizwi, na ndivyo ilivyokuwa hivyo Iran. Mapinduzi yalikuja kama tija ya umaskini katika nchi iliyokuwa nambari 1 kwa kuuza mafuta nje.
Fast Forward....chuki zilianza mara moja. Marekani ikijaribu kumrudisha Shah na Wairan, wote wakati huo, wakipinga. Ndipo Ayatollah Khomaini akaamuru Wanabalozi wa Marekani wazuiwe kuondoka nchini ili wawe kama dhamana ya kutotokea mapinduzi. Jambo hili lilipandisha mori wa Marekani na chuki. Tangu siku hiyo Marekani ikaiwekea vikwazo Iran hadi leo!
Kinyume na wengi walivyodanganywa, Ayatollah Khomeini alisimika Jamhuri ya Kiislamu baada ya kura ya maoni 1979, ambapo mfumo wa Kiislamu, Islamic Republic, ulikubaliwa na wengi kwa kura ya maoni ya asilimia 98.2. Hii ilikuwa kura ya wazi, huru na amani kabisa katika Mashariki ya Kati kuwahi kutokea, hata kushinda kura za Israel na Uturuki (zinazosifiwa kuwa na demokrsia), kwa mujibu wa UN wakati huo.

Wamarekani waliposhindwa kumrudisha Shah mapema, wakasuka mpango wa kumshawishi rais jirani wa Iraq, Saddam Hussein, kuishabulia Iran, angalau waweze kuiangusha Jamhuri changa kwa vita. Hilo halikufanikiwa, na kwa miaka 8 iliyofuata vita ikapiganwa. Kwanza Wairan walikuwa wanyonge, waliwekewa vikwazo vya kununua silaha na nchi zote, hata risasi! Hata na Soviet Union, nchi iliyojitambulisha kwa kuwatetea wanyonge na wanaokandamizwa!
Ila kutokana na akili, vipaji na ubunifu wa Wairan, kidogo kidogo wakajitengenezea silaha hadi ilipofika 1985 wakakomboa ardhi zao zote, bali wakaingia Iraq! Kumbuka, nchi zote za Kiarabu zilikuwa zikiisaidia Iraq kwa mabilioni. Ni Syria na Libya pekee waliomwunga mkono Iran, zaidi kwa maneno.
Ni katika kipindi hiki ndipo Iran ilipoanza kujijengea viwanda mbali mbali hasa vya silaha baada ya kupata fundisho baya.
SUALA LA NUKLIA
Hili ndilo suala ambalo Marekani inasema inaingia vitani kwa ajili yake.
Ni hivi, kwanza kuna tofauti baina ya silaha za nuklia na nishati ya nuklia. UN, baada ya kuona maafa makubwa yaliyosababishwa na Mabomu ya nuklia yaliyoangushwa na Marekani kule Nagasaki na Heroshima Japan mwishoni mwa vita kuu ya pili, iliweka taratibu kufanya Mataifa yote mengine yasiyokuwa bado yameunda silaha za nuklia kufikia mwaka 1950, wazuiwe kabisa kuundfa silaha hizo, lakini wapewe ruhusa ya kufaidika na nishati za nuklia, kwani nishati hizi zinaweza kutumiwa katika matumizi ya amani kama kufua umeme, madawa, kilimo na safina ziendazo chini zaidi baharini au kwenye anga za nje nk.

Hadi hapo ni Marekani, Urusi, China, France, Uingereza ndiyo zilizokuwa na silaha hizo pekee, Baadaye wengine wakazipata kinyemela, Israel, India, Pakistan na Korea ya Kusini (Hiyo ni hadithi kando).

Ili kuratibu utumiaji wa nishati za nuklia, mwaka 1968 wakaunda NPT, Nuclear non Proliferation Treaty, Yaani Mkataba wa Kuzuia Kusambaa kwa Silaha za Nuklia.
Kwa mujibu wake, nchi inayotaka kutumia nishati ya nuklia kwa mambo ya amani, labuda kwanza wajiunge na NPT, waahidi hawatatengeneza silaha, na pia vinu na mitambo yote ya kufulia nishati hiyo viwe chini ya udhibiti na uchunguzi wa mara kwa mawa wa Shirika hili NPT.
IRAN INABAGULIWA
Program ya nuklia ya Iran ilianza tangu wakati wa Shah ambaye alisaini NPT mwanzoni kabisa 1968. Marekani hasa ndiyo iliyomjengea Shah mitambo miwili ya mwanzo ya nuklia bila nongwa. Iran ilikuwa inanunua madini ya Urani au Kinywe kutoka Marekani bila matatizo yoyote, kwa ajili ya kutengeneza madawa hasa ya Kansa.

Tatizo likaanza kujitokeza wakati Serikali mpya ya Kiislamu, mwaka 1990, ikataka kununua mzigo kutoka Marekani kwa ajili ya wagonjwa wake. Wakati huo Iran ilikuwa na wagonjwa wasiopungua 40 elfu wa Kansa. Malimbikizo yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi yalikuwa yamekwisha. Lo! Hammadi. Marekani, ikakataa kuuza urani kwa Iran, ingawaje hili ni kinyume cha Sheria za Kimataifa na NPT! Zaidi ya hivyo, kila Iran ilipokwenda kutafuta nchi nyingine, kama Brazil, Argentina, Japan....walikuta katazo la Marekani wasiuziwe!
Ungefanyaje kama wewe ni kiongozi wa nchi yako? Hapo ndipo Iran ilipanza fikra ya kuweza kutengeneza enrichment (kutakasa) yenyewe.
Kama nilivyokuambia, Wairan ni watu wana akili za ajabu sana. Lakini pia, kitu cha kwanza Serikali ya Kiislamu kukitilia mkazo ilipofika madarakani ni elimu. JHakuna kazi nzuri Iran kama mwalimu. Serikali imefungua vyuo vya viwango vya nchi zilizoendelea na zaidi. Hivi tusemavyo, kila mwaka wanafunzi wa Iran ndiyo wanaochukua namba 1, 2 katika mashindano ya Hesabati duniani (World Maths Olympics). Vyuo Vikuu vinne vya Iran ni kati ya 10 vinaongoza duniani katika Engineering!
Kifupi...wakaweza kujifanyia wenyewe enrichment...kurutubisha madini ya kinywe! Wamarekani macho yakawatoka, hawakuamini kamwa Wairan wenyewe wangeweza kufanya enrichment! Ni elimu ambayo hata nchi kama Italy, Spain, Sweden etc bado hawajafika!

MIZENGWE YA MAREKANI
Kwa kutaka kuzuia maendeleo ya Iran, Marekani ikishakizwa na Israel, ikaanza kuchochea kwamba Iran ina nia ya kutengeneza silaha za nuklia, ingawaje Iran imetia saini ya kutotengeneza silaha hizo, bali na Kiongozi wake wa Kidini Ayatollah Khomeini alitoa fatwa kwamba kutengeneza silaha kali za kuuwa binadamu kwa jumla bila kuchagua ni marufuku katika Uislamu.

Marekani imeshikilia Iran ina nia ya kutengeneza silah! Baya zaidi, marafiki wa Marekani, kama Israel, ina silaha za nuklia hasa na imekataa kutia saini ya kudhibiti silaha hizo....lakini Israel ndiyo hasa iko mbele katika kuisakama Iran ambayo haina!
NPT iliibana Iran kwa kuipa masharti magumu zaidi, mfano wawe waweza kutembelea mitambo yote bila hodi na bila kutoa taarifa.... Iran ilikubali hiyo ingawaje haikuwa lazima, lakini havijawaombea!

Kama unajua dunia vizuri, basi utajua kuwa Marekani ni koloni la Israel na kwa hiyo inafanya kila inaloamriwa na Israel, ikiwemo vita hii ijayo.
Israel haitaki kuona nchi yenye nguvu inayoshindana nayo. Na sababu kuu hasa ni kwamba inaogopa kwamba kukiwa na dola linaloweza kusikizwa duniani, hatimaye dola hilo litakuja kuilazimisha Israel kuwapa Wapalestiona sehemu zao ilizoziteka mwaka 1967 kwa mujibu wa UN.
Sehemu hizo, kama Gaza na Ufukwe wa Mashariki wa Mto Jordan, Wayahudi wanadai Mungu wao aliwakabidhi wao, miaka 3,000 iliyopita! Sisi tuliouliza tuone Hati hiyo Miliki ya Mungu....bado twasubiri majinbu. Ila baadhi ya madhehebu ya Kikristo huunga mkono hilo, Huko Marekani, Wakristo hao ndiyo wanaoshinikiza serikali yao juu ya kuisapoti Israel hata kinyume na sheria za Kimataifa!

Utaona ingawaje kuna udini fulani katika vita hivi kwa mtazamo wa Israel, lakini kwaa mtazamo wa siasa za dunia yetu ya sasa zinazosimamiwa na misingi ya haki na sheria....hii ni vita ya mbabe mwenye silaha kubwa kumkanyaga mnyonge. Might is right!
Uzi bora kabisa hapa international forum

Katika watu magenius hapa JF wewe pia nakupa mauwa yako

Umechambua kwa umakini sana Big Up
 
Israel na US wote hawana hypersonic missiles...
Unaweza imagine nchi iliyowekwa kwenye vikwazo kwa miongo mitano wanatengeneza hypersonic na kurutubisha urani.

Wanatengeneza Air defenses zao , radar, Wametengeneza shaheed drones ambazo Russia ame copy na anazitumia kwenye vita yake na Ukraine, US na yeye ame copy anatengeneza sasa shaheed drones akiziita LUCAS, Russia wanaziita Geran kama sijasahau...

Waajemi ni watu wenye akili... hata jinsi wanavyoendesha mikakati yao kivita na strategies si watu wa mchezo, wamewa out smart Israel...
Wajinga wenzako ndiyo watakubaliana na uongo wako huu!!!

Katika vita vya siku 12 Ndege-Vita za Israel zilitawala anga lote la Iran hapakuwa na Nywinywinywi wala Nywinywinywi ndege -vita hizo ziliweza kupiga popote zilipotaka hakukuwa na upinzani wowote na Iran hawakuweza kuangusha hata ndege-vita moja ya Israel leo wewe unakuja kusifia Air defense System za Iran huo ni Ujinga uliopitiliza.

Unawasifia Waajemi ambao kwa vita ya siku 12 tu waliuwawa Makamanda waandamizi karibu wote akiwemo Mkuu wa Majeshi kwa kitendo hicho tu utajua hapo hawana Jeshi kulinganisha na Israel.

Majeshi ya Israel yaliweza kuua Makamanda wa IRGC na wataalamu wa Nuclear kama nzige angalia picha zao hapo chini
 
Attachments

  • IMG_3499.jpeg
    IMG_3499.jpeg
    132.9 KB · Views: 6
  • IMG_3483.jpeg
    IMG_3483.jpeg
    59.3 KB · Views: 7
  • IMG_3466.jpeg
    IMG_3466.jpeg
    339.2 KB · Views: 5
  • IMG_3479.jpeg
    IMG_3479.jpeg
    351.6 KB · Views: 8
  • IMG_3419.jpeg
    IMG_3419.jpeg
    35.8 KB · Views: 6
  • IMG_3414.jpeg
    IMG_3414.jpeg
    197.7 KB · Views: 10
  • IMG_3406.jpeg
    IMG_3406.jpeg
    68.7 KB · Views: 6
  • IMG_3405.jpeg
    IMG_3405.jpeg
    65.3 KB · Views: 8
  • IMG_3404.jpeg
    IMG_3404.jpeg
    72.7 KB · Views: 8
  • IMG_3403.jpeg
    IMG_3403.jpeg
    130 KB · Views: 9
  • IMG_3402.jpeg
    IMG_3402.jpeg
    112.9 KB · Views: 4
  • IMG_3401.jpeg
    IMG_3401.jpeg
    59.9 KB · Views: 6
  • IMG_3366.jpeg
    IMG_3366.jpeg
    347.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom