Wakati Pengo akiuruka Waraka wa Katoliki, Askofu Shao amesema wapo tayari kwa lolote juu ya Waraka wa KKKT

Watu wachonganishi sana. kwanini mnamchonganisha Askofu Pengo huku? Muacheni jamani!
 
Sidhani kama watafanywa lolote, zaidi sana ya kujiaibisha tu kwa kurukia mambo ya kisiasa na kuyaacha ya dini, halafu wakipewa majibu ya kisiasa, wataanza kuvaa kofia zao za kidini.

Hawa ni kuwajibu tu kisiasa ili wakumbuke nafasi zao kidini, wakatulie na kuchunga kondoo wa bwana.
Lipi la siasa walilorukia ambalo si la wajibu wao,
Umemskia baba enu alivyowaambia maaskofu wahamasishe ujenzi wa viwanda nalo ni jukumu lao?
 
Atueleze kwa ufafanuzi waumini wa KKKT juu ya wizi wa mabilioni fedha za Kanisa uliofanywa na Usharika wa Kaskazini. Shame on you Askofu SHAO kwa kukubali kutumika na WanaSiasa. Najiskia KINYAA kuwa muumini wa KKKT.
Nilivyosoma jina Shoo sijui Shao nikajua Huyu hawezi kuacha dili huyu.
 
Hivi kama watu wanapotea, maiti zinaokotwa baharini, risasi za kijinga zinaua watu (refer kesi ya yule binti wa NIT), police wanaua watuhumiwa (refer tukio la Simiyu) vitisho vya police kwa raia wanapotekeleza mambo ya katiba na police wanasema kabisa kwamba watu wajiandae kua vilema, chaguzi ambazo zilikua kabisa zinazuilika (Kinondoni, Siha) nk; kama yote haya yanatokea halafu mnataka viongozi wahubiri nini!? Uonezi, uuaji, zuruma na matumizi mabaya ya mali au fedha ni sehemu tu ya DHAMBI and hence linabaki kua jukumu la viongozi wa dini kukemea. Wakiacha kuyakemea hayo then hata sisi waumini wao tutawashangaa, remember wana siasa nao ni miongoni mwa waumini wa hao hao viongozi wa dini so maaskofu kusema mambo kama hayo ni kwamba wanawakemea waumini wao.
kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili unaoendelea katika jamii zetu,unaongezeka siku hadi siku kwa sababu wachungaji/maaskofu wako busy kufanya mambo yao kwa maslahi yao binafsi thats so sad naona sasa hivi wameamua kuingilia siasa INASIKITISHA SANA.
 
very true....kondoo wanapotea kila siku kama wangekuwa wanatimiza wajibu wao kama watumishi wa Mungu yanayoendelea kwenye jamii tusingekuwa tunayasikia wala kuyaona sasa huko wameshindwa wanataka kuwa wanasiasa...this is very interesting.
Kondoo ndo haohao wanaoteka, wanaoua, wanaopiga watu risasi, wasiopenda kusikia fulani akikosolewa, wanaonunua watu wengine na kuirudisha nchi mwenye chaguzi ghali. Wanafanya hivyo huenda kwa kutii amri ya mtu fulani, sasa maaskofu wameamua kumkumbusha mtu huyo juu ya hayo maovu. Badilikeni sasa, saa ya wokovu ndiyo hii. Isikieni sauti takatifu ya Maaskofu.
Maaskofu wanaamini kabisa na wanajua huyo anayetoa amri akianza kusikia sauti ya Mungu na kuanzia kutenda haki huku akikemea maovu ya watu kuuawa/kupigwa risasi kikatili, nyie vidagaa mtabadilika automatically.
 
Kondoo ndo haohao wanaoteka, wanaoua, wanaopiga watu risasi, wasiopenda kusikia fulani akikosolewa, wanaonunua watu wengine na kuirudisha nchi mwenye chaguzi ghali. Wanafanya hivyo huenda kwa kutii amri ya mtu fulani, sasa maaskofu wameamua kumkumbusha mtu huyo juu ya hayo maovu. Badilikeni sasa, saa ya wokovu ndiyo hii. Isikieni sauti takatifu ya Maaskofu.
Maaskofu wanaamini kabisa na wanajua huyo anayetoa amri akianza kusikia sauti ya Mungu na kuanzia kutenda haki huku akikemea maovu ya watu kuuawa/kupigwa risasi kikatili, nyie vidagaa mtabadilika automatically.
kuhama chama ni haki ya msingi ya kila raia,kama unaona kuna upande haufanyi vizuri ni ruksa kuhama,haikatazwi...unaweza kudhibitisha ununuzi au kama kawaida na story zenu za vijiwe vya gahawa,tatizo katika waraka wao wamechanganya dini na siasa sasa jumbe kama hizo zikikutana na akili kubwa ZINAPUUZWA VIBAYA MNO wakajipange upya kwa hilo wamechemka tunajua kinachowasumbua.
 
Askofu Mstaafu, Dkt. Martin F. Shao amesema kuwa, tamko la Pasaka la Maaskofu wa KKKT ni neno la Mungu ambalo limekuja kwa ajili ya Tanzania kwa wakati wake. Asisitiza kuwa, kikitokea chochote hata cha kutisha uhai wao, hawataogopa bali watamtegemea Mungu

Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Martin Shao alisema: “Ninafahamu kwamba kwa kutoa huu waraka maaskofu hawa 27 wanaweza kupigwa vita, lakini wasimame hata kama kwa msimamo huo itawagharimu.”

Huku akiwapongeza kwa kutoa waraka huo, Askofu Shao alisema ameusikiliza waraka huo kwa makini na kubaini umetolewa wakati mwafaka.

“Nikiwa askofu mstaafu nimekutana na watu kabla ya tamko hili, wananiuliza askofu unasemaje kuhusiana na hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa?

“KKKT haikurupuki tu kusema, huwa inatafakari sana kabla ya kutoa tamko, huu ni ujumbe wa Mungu kwetu sisi na Watanzania wote. Ujumbe wenu umefika kwa Wakristo wengi na Watanzania. Tutatenda kulingana na hayo mliyoyasema,” alisema Shao

Soma Kuhusu Askofu Pengo hapa - Askofu Pengo: Sikufahamu kuhusu waraka wa Kwaresma wa Baraza la Maaskofu Katoliki. Awaasa wasichanganye dini na siasa

Soma Kuhusu Waraka wa Maaskofu KKKT - Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...

Habari zaidi....


Dar/Moshi. Siku moja baada ya Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka, mkuu wa kanisa hilo, Dk Frederick Shoo amesema wasinyamazishwe kwa kuwa jukumu la viongozi wa dini ni kuonya na kusema ukweli.

Dk Shoo, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini alitoa kauli hiyo jana katika Usharika wa Masama Kati, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika ibada ya Jumapili ya Matawi baada ya mchungaji kiongozi wa usharika huo, Pray Usiri kuusoma waraka huo ambao ulianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu Jumamosi.

“Sisi viongozi wa dini hatutanyamaza na hatutawaachia. Wajibu wetu tunaonya, tunashauri, tunakemea na tunasema. Asijaribu mtu kutuzuia kufanya hivyo,” alisema Dk Shoo katika ibada hiyo jana.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, KKKT ilitoa waraka ambao mbali na kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”

Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Alichosema Askofu Shoo jana

Akifafanua msingi wa kutolewa waraka huo, Dk Shoo alisema wameutoa baada ya kufunga na kuomba ili Mungu awawezeshe kutoka na ujumbe mahsusi kwa waumini wa kanisa hilo, huku akiwakemea wanaouhusisha na siasa.

Alianza kwa kuwapongeza maaskofu waliochangia kuutoa waraka huo aliouita kuwa ni wa kinabii na kuwataka kuendelea na ujasiri huo.

Dk Shoo alisema walipofunga waliomba wapewe ujumbe utakaosaidia Taifa na wakaona hawawezi kukaa kimya hata kama utakuwa ujumbe mzito.

Alisema walikubaliana waufikishe kwa waumini wao na nchi kwa ujumla, huku akiufananisha na uliotolewa hivi karibuni na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

“Tuupokee ujumbe huu siyo kwa kukurupuka, tuupokee, tuusikilize, kuutafakari na tuombe sana ili Mungu atupe macho ya kiroho, tufahamu Mungu anataka kutuambia nini kwa ajili ya nchi yetu,” alisema Dk Shoo na kuongeza:

“Tuweke itikadi ya vyama na kisiasa pembeni, tumuulize Mungu unataka kutwambia nini kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania. Tunawasihi kwa machozi, tumeandika pale, tunawasihi kwa machozi Watanzania, yapo mambo Mungu anayaona, anayaangalia, anaona haya ni mema yatendeni hayo.”

Alisema yako mambo Mungu anayaona kuwa ni maovu na kama Tanzania inayaona hakika mwisho wake hautakuwa mwema.

“Mungu anasema hayo mema yanayotendeka yatafanyika hayo yatendeni, yale maovu yaacheni,” alisema Dk Shoo na kuongeza:

“Yako mambo ambayo tumeyataja katika waraka huo, Mungu atujalie tuyatafakari na kuyatenda kwa ajili ya Taifa letu, yale ya kukataa na kukemea tuyaache kwa ajili ya kulipenda Taifa letu.”

Dk Shoo alisema wao kama viongozi wa kiroho wamefanya hivyo kwa kumheshimu Mungu, kwa kutambua nafasi yao na utume waliopewa.

“Wengine mnaweza kudhani (waraka) ni wa chama fulani au itikadi fulani, hapana! Tumefanya kwa wajibu wetu, hatujafanya na hatutafanya kutoa ujumbe eti kwa sababu ya upande fulani wa chama.

“Isitokee kikundi cha watu kinachoweza kufikiri kitaziba sauti ya Mungu, hatuwezi kunyamaza neno la Mungu halituruhusu kufanya hivyo na ninaomba wajue kutofautisha sauti ya nabii wa Mungu na propaganda za kisiasa zinazoweza kupingwa na wengi.

“Tutofautishe ushabiki pamoja na kauli mbiu za kisiasa au za wanasiasa na matamko ambayo misingi yake ni upendo wa dhati kwa nchi hii, ni uzalendo wa dhati kwa ajili ya vizazi vijavyo,” alisema.

Alifafanua kuwa anaogopa watu wanapokaa na kuanza kuwa na hofu ya maisha na uhai wao, jambo alilosema ni hatari hivyo lazima waseme hapana.

“Mungu wetu ni Mungu wa uhai si wa kifo, si wa mauti,” alisema Dk Shoo na kuwaomba wautafakari waraka huo ili kuona wapi Mungu anataka wabadilike ili iwe Tanzania ya amani.

Alisema wapo watakaoupokea waraka huo kwa fikra mbalimbali, hivyo akawataka watakaofanya hivyo kuweka pembeni fikra zao na kuangalia nia njema.

“Sisi Walutheri si wasikilizaji, ni watendaji na huu uwe ni mchango wetu kwa ajili ya nchi yetu,” alisema.

Akitoa wito kwa wanasiasa, Askofu Shoo alisema: “Nawasihi wanasiasa na vyama vyao, msije kutugawanya gawanya nchi yetu katika vipande vipande, Tanzania ni nchi yetu sote, msije kuigawanya hii nchi na kuipeleka mahali kubaya.”

Chanzo: Mwananchi

Akina Shayo na Ulutheri wao wa ukanda,tunajua kwanini wana wivu wa kike wao walie tu.Askofu mstaafu(?)yeye ni nani hadi atake tumsikilize na huo waraka wa kihuni.Tanzania sio nchi ya kidini,kwa hiyo waishie zao,serikali itawasikiliza wangapi,je wao walimsikiliza nani na hiyo KKKT yao?hizi dini zimegeuka SACCOS za kisiasa.Eti sauti ya Mungu,haha haha sijui hiyo sauti wanaisikia wao tu
 
Kwa hiyo waliutoa kwa ajili ya lolote..ndio shida ya kuchanganya dini na siasa..hivi hawajui vitega uchumi vyao vinavyowapa hiyo jeuri ya kutaka kupambana na serikali msimamizi mkuu ni serikali yenyewe..serikali ikijitoa kuwalipa watumishi kwenye hospital na idara zao mbalimbali wao watamudu?? Au ndio jeuri ya kujisahau..waambiwe huyu sio jk..wakati wao wanapaza sauti za bifu mwenzao anapiga kimya kimya..wasije anza kusema wanaonewa
acha kutisha watu ww hii nchi ni ya wote, hizo hela ni za kwako au baba yako mpk una tishia eti wasipewe?
 
Burden aliyokuwa nayo magufuli kwa sasa ya kuondoa uoza wa rushwa, wizi, matumizi mabaya ya rasilimali za uma isingekuwa kubwa namna hii, kama hawa viongozi wa dini wangetimiza wajibu wao.

Nilitegemea kuona wao wakiwa watu wa kwanza kumuunga mkono Rais katika jitihada zake za kurudisha nchi pazuri lakini ajabu sana, wao nao wanaungana na ule upende mwingine.

Halafu kibaya zaidi wanaquote maandiko ambayo kwa namna yoyote ile hayaendani na mazingira ya sasa katika jamii yetu, ili mradi tu kufit madai yao.

Viongozi wa kidini watusaidie kuona ukweli na sio kutupotosha, jamani jamani.
Kwahiyo wamekupotosha waliposema hali ya sasa ya nchi sio nzuri, uhuru wakujieleza haupo, na wasi wasi uliopo katika jamii. Hauoni matamko ya kutisha raia kila kukicha? Think again
 
Askofu Shao , jina tu linatosha kuelezea kila kitu. Kamanda huyo wa CHAGADEMA.
MGAWO WA ESCROW UNAMZIBA MDOMO BISHOP PENGO

[HASHTAG]#Huu[/HASHTAG] mgawo unamfanya Pengo anashindwa kusimama na Kanisa Katoliki...

[HASHTAG]#Hakuna[/HASHTAG] asiyetambua Pengo kuwa ni mwanachama wa CCM, aliyejivika ukondoo wa kiroho ili kukinzana na dhana na muendelezo wake wa ukosoaji kila mabaraza ya maaskofu yanapotoa kauli moja dhidi ya serikali inayoongozwa na ccm...

[HASHTAG]#Itambulike[/HASHTAG] tu kuwa Kardinal, Pengo hana mamlaka yoyote ndani au nje ya baraza la maaskofu wa katoliki 'TEC' Pengo ni mjumbe wa kawaida tu wa baraza hili la maaskofu..
Mwenye mamlaka na kanisa katoliki ni Rais wa baraza la maaskofu hao, Askofu Tarcius Ngalalekumtwa...

[HASHTAG]#Pia[/HASHTAG] maamuzi ya baraza lote ili yakamilike na yawe halali na iwe timilifu, yanahitajika kuungwa mkono asilimia karibia 75% ya wajumbe wa mkutano wa maaskofu wote...

[HASHTAG]#Matamko[/HASHTAG] ya TEC pia yanatambulika na makao makuu ya kanisa katoliki 'Vatican' na kuidhinishwa, kumbuka tamko la Pengo halitambuliki kule 'Vatican' bali ni TEC pekee...Rejea kanisa katoliki na ile movement yao kule Congo...

[HASHTAG]#Kardinal[/HASHTAG] Pengo, anatia aibu na analitia aibu kanisa katoliki, jina na sahihi yake ilikuwepo pale, sasa kujenga kwake dhana tofauti ya ukosoaji ya maamuzi ya maaskofu wenzake baada jambo kupita anataka atuaminishe yeye ndiyo katoliki na sio TEC...

[HASHTAG]#Askofu[/HASHTAG] Ngwajima alimuita msaliti baada ya maamuzi na maafikiano kipindi kile cha mchakato wa rasimu ya katiba,...Kwahiyo sio mara ya kwanza kwa Pengo kutoka pembeni na kujenga dhana ukosoaji hasa kwa chama chake cha ccm...

[HASHTAG]#Kardinal[/HASHTAG] Pengo, utamkumbuka Ngwajima, alikuambia hufai kuliongoza kanisa kutokana na tabia hii, 'U-snitch'...

[HASHTAG]#Jina[/HASHTAG] na sahihi yako ilifuataje pale kama na wewe haukuadhimia, kiongozi wa kiroho huitaji busara katika kuendesha waumini wake...Ungekaa kimya Mzee, pia ni busara!!!

[HASHTAG]#Dini[/HASHTAG] hubeba vyote vilivyomo ikiwemo na siasa, uchumi, sayansi na mengineyo...

[HASHTAG]#Kardinal[/HASHTAG] Pengo, umebeba waumini wenye kada tofauti kisiasa lakini sio wote ni ccm, waumini wengi wa katoliki ni 'Wazalendo'....

Makavel
 
Teh..kwa hiyo maaskofu tu wa kkkt hao kumi na ngapi sijui ndio wanamuombea?? Wasubiri tu majibu..mtasikia wakipiga kelele..wamejisahau tu..serikali hii haitegemei kanisa kama serikali zingine..na ndio maana kwa sasa iko bize na kuimarisha taasisi zake zikiwemo mashule na hospital..kwa sasa umaarufu wa hizo taasisi za makanisa unashuka kwa kasi na wameshaona hilo
Utakua unaota wewe....hata kama ni mahaba sio kwa kiasi hiki...
 
Naona watu wameshupaa kusema dini isichanganywe na siasa. Hawajiulizi kwanini mkulu alivyoapishwa alishika Biblia.
Kuna serekali zinazoongozwa na dini, hatakama yetu haina dini mbona kila kukicha anaomba aombewe, then hataki ujumbe kutoka kwa wanao muombea?
 
Back
Top Bottom