Wakati mzee kilomoni anapinga janja ya Mo dewji alionekana mbaya

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,007
Mzee kilomoni aliona mbali sana na alipinga janja janja ya mohamed dewji kipindi kile cha mabadiliko ila wana-simba wengi walimbeza na kumuona msaliti na anayekwamisha mabadiliko

Ukweli ni kwamba kilomoni aliona mbali sana leo hii simba mwenyekiti anatumia gharama kubwa ya kumleta manzoki kwenye kampeni za uchaguzi alafu kiutendaji hana mamlaka yeyote hiki ni kituko kikubwa sana ni bonge ya kanyaboya

Mangungu hana mamlaka kikatiba ambayo simba waliipitisha mwaka 2018/2019 ni jambo la ajabu mashabiki kumlalamikia na kumtaka aondoke mangungu yeye sio chanzo cha tatizo bali chanzo cha tatizo ni dewji na wapambe wake try again na kajuna

Hiki kinachotokea leo simba ni ishara asilimia kubwa sana ya sisi watanzania tuna upeo mdogo sana sio watu wa kufikiria mbali na hii itatukwamisha kwenye mambo mengi sana ni akili ya wapi unawapa wanachama asilimia 51 hisa ambayo hata hawachangii chochote hiki ni kituko cha mwaka

Mo dewji akiondoka hata sahivi simba hawawezi kosa mwemezaji matajiri wengi sana wanaitamani simba
 
Hivi hiyo timu angepewa mzee Kilomoni angeweza kulipa hata jezi ya mchezaji mmoja?

Timu ina gharama zake,safari za ndege na mafuta ya gari kila mechi misimu yote,hoteli za kulala,malazi na vyakula .

Halafu unaanza kuleta mada za futuhi kabla ya kufikiri
 
Mkuu hoja yako ni Mo au Mangungu? Maana kichwa cha habari ni Mo ila kwenye maelezo unasema Mangungu kaleta janja janja. Kama mleta janja janja Mangungu basi Mo mtoe kwenye uzi wako. Na kama Mo naye anahusika na janja janja basi toa maelezo ni kivipi Mo ni janja janja toa sababu za msingi.

Maneno yamekuwa mingi sana kwa timu ya Simba vidole vimekuwa vingi sana ili wavurugane, lakini pamoja na yote Simba ndiye muanzilishi wa mafanikio ya soka la kimataifa chini ya huyo huyo Mo.
 
Mzee kilomoni aliona mbali sana na alipinga janja janja ya mohamed dewji kipindi kile cha mabadiliko ila wana-simba wengi walimbeza na kumuona msaliti na anayekwamisha mabadiliko

Ukweli ni kwamba kilomoni aliona mbali sana leo hii simba mwenyekiti anatumia gharama kubwa ya kumleta manzoki kwenye kampeni za uchaguzi alafu kiutendaji hana mamlaka yeyote hiki ni kituko kikubwa sana ni bonge ya kanyaboya

Mangungu hana mamlaka kikatiba ambayo simba waliipitisha mwaka 2018/2019 ni jambo la ajabu mashabiki kumlalamikia na kumtaka aondoke mangungu yeye sio chanzo cha tatizo bali chanzo cha tatizo ni dewji na wapambe wake try again na kajuna

Hiki kinachotokea leo simba ni ishara asilimia kubwa sana ya sisi watanzania tuna upeo mdogo sana sio watu wa kufikiria mbali na hii itatukwamisha kwenye mambo mengi sana ni akili ya wapi unawapa wanachama asilimia 51 hisa ambayo hata hawachangii hiki ni kituko cha mwaka
Huwa napata shida kuwafundisha wanafunzi wangu kwambwa Kampuni ya Simba Mo ana kama asilimia 49 na wanacha wana 51 na MO ndio anasauti,yaani mwenye share chache ana sauti ya mwisho,Hii ni inawezakana Tanzania pekeee
 
Hivi hiyo timu angepewa mzee Kilomoni angeweza kulipa hata jezi ya mchezaji mmoja?

Timu ina gharama zake,safari za ndege na mafuta ya gari kila mechi misimu yote,hoteli za kulala,malazi na vyakula .

Halafu unaanza kuleta mada za futuhi kabla ya kufikiri
So hii timu yetu kiujumla haitengenezi faida zaidi ya hasara

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Inatengeneza faida lakini mtu kama kolomoni angefanya simba iwe ombaomba,tulishapita huko enzi hakuna uwekezaji,timu inahitaji mwenye hela awekeze siyo mtu asiye na kipato ategemee kwanza faida ndo aendeshe timu
Kilomoni anataka 51% iwe na nguvu ili yoyote atakayekuwa mwenyekiti afanye maamuzi kwa maslahi ya wanachama wenye hisa 51% na sio mwenyekiti anafanye maslahi ya muwekezaji
 
Wakati tunamkabidhi timu Hersi mlitucheka sana, mliongea yote tulipompa Urais.

Yako wapi? Mnazunguka mbuyu tu lakini mnatamani sana kuwaambia viongozi wenu waige mfano kwa Hersi kuendesha timu kisasa.
Mimi niliwaonya niliokuwa nao kazini,wakawa wanatuita timu bakuli .Tukawaambia Bora bakuli kuliko kuwa mke mdogo ,na Dewj alitamka yeye kwamba Simba ni mke mdogo wake.Hawakuelewa.Sasa Nasemaje! Nnasemaje " MPAKA WaSEME,naa WATASEMA.
 
Hivi hiyo timu angepewa mzee Kilomoni angeweza kulipa hata jezi ya mchezaji mmoja?

Timu ina gharama zake,safari za ndege na mafuta ya gari kila mechi misimu yote,hoteli za kulala,malazi na vyakula .

Halafu unaanza kuleta mada za futuhi kabla ya kufikiri
Hahahahaha,mkuu ishu ni nguvu ya mwenyekiti anawakilisha wanachama wenye hisa 51% inamezwa na Mwekezaji
Hili liko wazi ,ndio kuna kundi lina fanya harakati vipengele vibadilike nguvu iwe kwa mwenyekiti wa klabu amabaye anawakilisha 51% ya hisa za wanachama
 
Rita walishaona tatizo, wakazuia kubariki mchakato wa Simba . Walisema haiwezekani mwenye asilimia 49 akawa na sauti kubwa kuliko mwenye asilimia 51. Uongozi uliomba upewe muda Hadi mwezi wa Tisa, hapo ndio Mangungu anabeba lawama.
Hivi kweli mkuu vitu vingine tutumie akili tu ya kawaida kufikiria. Mnataka mwenye asilimia 51 awe tu na sauti kubwa za mdomoni tu pasipo utendaji? Yaani mwenye asilimia 49 atoe pesa zake kusajili na kulipa mishahara halafu nyie msiotoa ela mue na sauti kwasababu mna asilimia 51. Hilo jambo gumu sana, kama mnataka hivyo na nyie wenye 51 inabidi mtoe mpunga kuendesha timu
 
Wakati tunamkabidhi timu Hersi mlitucheka sana, mliongea yote tulipompa Urais.

Yako wapi? Mnazunguka mbuyu tu lakini mnatamani sana kuwaambia viongozi wenu waige mfano kwa Hersi kuendesha timu kisasa.
Hapa GSM walitumia akili ndogo tu ,kwa kua hizi club wanachama ndio kila kitu ,basi Eng ,,aende kuwa chairman wa club ,1.kuondoa mgongano 2.kudhibiti nguvu ya wanachama na maamuzi ,3.kusimamia yale wanayoyaamini yakiwa watafanikiwa 4. Kuepuka makundi ya wanufaika ktk club
 
Kuchekana ndio utani wenyewe, ni upepo tu,, unafikiri Hersi apigi 10%? Kutesa kwa zamu,, mda wenu huu mfuraie kwani kukaa namba 1 haishindikani ila kukaa milele haiwezekani,

Miaka ile enzi za sarpong 😁 mliona kila rangi,,
 
Hivi kweli mkuu vitu vingine tutumie akili tu ya kawaida kufikiria. Mnataka mwenye asilimia 51 awe tu na sauti kubwa za mdomoni tu pasipo utendaji? Yaani mwenye asilimia 49 atoe pesa zake kusajili na kulipa mishahara halafu nyie msiotoa ela mue na sauti kwasababu mna asilimia 51. Hilo jambo gumu sana, kama mnataka hivyo na nyie wenye 51 inabidi mtoe mpunga kuendesha timu
Mpira wa Tanzania umebadilika unafikiri kwanini mo alikataa Simba isipokee pesa za Azam kwa mkataba wa miaka 10, Simba masikini ilikuwa inasajili vizuri kuliko hii tunayoambiwa Ina pesa.
 
Hapa GSM walitumia akili ndogo tu ,kwa kua hizi club wanachama ndio kila kitu ,basi Eng ,,aende kuwa chairman wa club ,1.kuondoa mgongano 2.kudhibiti nguvu ya wanachama na maamuzi ,3.kusimamia yale wanayoyaamini yakiwa watafanikiwa 4. Kuepuka makundi ya wanufaika ktk club
Ntashangaa asipokuelewa
 
Back
Top Bottom