Wakati mwaka waisha

Mwali

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
7,018
0
[h=3]Wakati mwaka waisha[/h]

Mwaka huo wayoyoma, tuwache uende zake,
Wacha uende salama, ulijaa mambo yake,
Tuombacho ni uzima, tupewe baraka zake,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

Penzi lako haliishi, kama mwaka uishavyo,
Niseme halinichoshi, kama mwaka uchoshavyo,
Wala halikinaishi, vyovyote vile iwavyo,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

Kwako nimesharidhika, kwingine nif'ate nini?
Nanena kwa uhakika, yanikaayo moyoni,
Sifikiri nitachoka, siku zote maishani,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

U nuru waniangaza, maisha kunipa raha,
U ua wanipendeza, moyo kujawa furaha,
Sauti yaniliwaza, daima kutoa karaha,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

U chakula nishibacho, kwingine siwezi kwenda,
U mboni ya langu jicho, daima nitakulinda,
Amini nikisemacho, sidiriki kukutenda,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

Shida zote za maisha, wewe kwangu ni faraja,
Hofu yangu waishusha, kila tuwapo pamoja,
Daima huniwezesha, kuyavuka madaraja,
Wakati mwaka waisha, penzi lako haliishi.

Source: Fadhy Mtanga, Mbeya (diwani ya fadhili: Wakati mwaka waisha)
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,458
2,000
Mashairi kama haya hupaswa kujibiwa kwa ushairi pia...ngoja tutulie nasi tuweke tenzi kadhaa.
 
Mwali

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
7,018
0
Mashairi kama haya hupaswa kujibiwa kwa ushairi pia...ngoja tutulie nasi tuweke tenzi kadhaa.

Sijatunga mimi. Nimekuta mahala, nikaona ni-share nanyi maybe kuna atakae mtumia mpenzi wake...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom