Wakati Mbowe anaondolewa Mashine ya kupumulia Hospitali ya KCMC, Viongozi 6 CHADEMA waripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Moshi. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi kutokana kusumbuliwa na maradhi ambayo hayajawekwa wazi.

Habari za uhakika zilizoifikia MCL Digital leo Machi 5, 2018, zinasema jana alipofikishwa katika hospitali hiyo saa mbili usiku na madaktari walimwekea mashine ya kumsaidia kupumua.

Taarifa za kulazwa kwa Mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai zilianza kuzagaa leo baada ya watu kumuona hospitalini hapo.

Katibu wa CHADEMA mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa juu ya kulazwa kwa kiongozi huyo alionekana kusita kuzungumza na kuhoji ni nani aliyetoa taarifa hizo.

Hata hivyo amesema, "Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC na madaktari walilazimika kumwekea Oksijeni ili ku stabilize (kudhibiti) afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”

Lema alikataa kuingia kwa undani ugonjwa unaomsumbua kiongozi huyo akisema suala hilo ni siri ya mgonjwa na daktari wake zaidi ya kufafanua tu kuwa alipelekwa hospitalini hapo jana.

Habari zaidi zilizopatikana zilieleza kuwa asubuhi hii madaktari bingwa wa hospitali hiyo walikuwa wakimchukua vipimo ili kubaini maradhi yanayomsumbua.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vicent Mashinji na viongozi wengine wa chama hicho wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo asubuhi Machi 5, 2018.

Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye leo hayupo kwa maelezo kuwa ni mgonjwa, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.

Viongozi hao wakiongozwa na Dk Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa 2:15 asubuhi walikuwa wamewasili wote kituoni hapo.

Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Halima Mdee; Mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa BAWACHA.

Viongozi hao wameambatana na wakili Frederick Kihwelo na Alex Massaba pamoja na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.

Massaba ameieleza MCL Digital kuwa Mbowe hatoweza kufika kwa kuwa ni mgonjwa.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa CHADEMA akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.



Mwananchi

Habari zaidi...

Hali ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya KCMC inaendelea vizuri baada ya kuondolewa mashine ya Oskijeni.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha hivyo ambapo amesema kwa sasa anapumua mwenyewe bila msaada wa mashine hiyo.

Mbowe alifikishwa katika hosptali hiyo akiambatana na baadhi ya makada wa chama hicho ya saa 10:30 Jioni jana Jumapili Machi 4, akiwa katika hali mbaya.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema, amesema Mbowe alianza kuugua gafla wakati akipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Tulikuwa tukipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys lakini Mwenyekiti alisema anajisikia vibaya na afya yake haiko sawa hivyo akataka tumpeleke hosptali ya KCMC kwa ajili ya kuangalia afya yake zaidi.

“Baada ya kumfikisha hosptalini hapo madaktari bingwa walimpima afya yake na kumtaka kubaki chini ya uangalizi wa madaktari kwa matibabu zaidi,” amesema.


Madaktari wa Muhimbili wamesema Mbowe alikuwa akimumwa kichwa na hali hiyoimesababishwa na uchovu na sasa anaendelea vizuri


Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene
Chanzo: Mtanzania
 
Jamani maradhi ni kawaida kwa binadam, tumuombee mwenyeketi mbowe kwa Mwenyezi Mungu, ili aweze kumponya maradhi yanayomsumbua na arejee katika afya yake.

Nyie mnaofurahia mbowe kuugua, hizo ni tabia za kinyama. Tofauti za kisiasa haziondoi ubinadam wetu. Sote ni ndugu. Kwa pamoja, tumuombee Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe.
 
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA amelezwa katika hospitali ya rufaa KCMC baada ya kupata mshituko.

Mpaka sasa bado haijajulikana chanzo cha mshtuko uliosababishwa kulazwa kwake
 
mbowez.jpg
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Elikaeli Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi kwa kuugua ghafla usiku wa kuamkia leo na kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua.



Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema, “Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC, madaktari walilazimika kumwekea mashine ya Oksijeni ili kuweka sawa afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”

 


Freeman Mbowe anatuhuma za Kuhamasisha ghasia katika uchaguzi wa Kinondoni uliosababishwa Askari kujeruhiwa Vibaya na Kifo cha Mwanafunzi wa NIT.
 
Mwenyezi Mungu umponye Mh. Freeman Mbowe. Awe na afya njema aendelee kutekeleza majukumu yake ya kitaifa kwa jili ya Watanzania wote.
 
Namuombea Mheshimiwa uponyaji na nguvu za kutosha kabisa, Tanzania bado inamhitaji saana!
 


Freeman Mbowe anatuhuma za Kuhamasisha ghasia katika uchaguzi wa Kinondoni uliosababishwa Askari kujeruhiwa Vibaya na Kifo cha Mwanafunzi wa NIT.

Kesi inavyokuwa ngumu ndivyo ugonjwa unavyoongezeka
 
Back
Top Bottom