Wakala wa meli ya ‘wezi’ wa samaki ajisalimisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakala wa meli ya ‘wezi’ wa samaki ajisalimisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 12, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,783
  Trophy Points: 280
  Wakala wa meli ya ‘wezi’ wa samaki ajisalimisha

  Na Festo Polea

  HATIMAYE Wakala wa Meli ya Tawariq1, iliyokamatwa hivi karibuni ikijihusisha na uvuvi haramu katika ukanda wa Tanzania ambaye ni raia wa China, Ho Hanqing (39) amejitokeza na kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es salaam.


  Kujisalimisha kwa wakala huyo kunafanya idadi ya watuhumiwa wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kwa tuhuma za kufanya uharamia wa samaki katika eneo la bahari Tanzania kufikia 36.


  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema wakala huyo alijisalimisha juzi akiwa na nyaraka mbalimbali zinazohusiana na meli hiyo ambazo alifahamisha kuwa zinachunguzwa ili kufanikisha uchunguzi wa polisi dhidi ya watuhumiwa hao.


  Alisema pamoja na kujisalimisha wakala huyo atajumuishwa katika kesi inayowakabili watuhumiwa 35 ambao kati yao 15 ni raia wa China, watatu Vietnam, nane Philippine, Sita Indonesia na watatu ni raia wa Kenya.


  Akizungumzia kuhusu kuchelewa kwa watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani, Kamanda Kova alisema tatizo limesababishwa na lugha zao kutoeleweka kwa sababu wanazungumza lugha ambazo zimelazimu watafutwe wakalimani ili uandikishaji wa maelezo yao ufanyike kwa usahihi na kila mmoja apate haki yake.


  “Tayari tumeshapata wakalimali na kwa kuwa linahusisha watu wa kimataifa, uchunguzi huo unatakiwa kufanyika kwa umakini kwa kuwashirikisha wanasheria wa kimataifa pamoja na kuchambua na kuzingatia sheria za baharini na za mipaka,” alisema Kova.


  Kamanda Kova alisema kwa kuwa suala hilo linamuonekano na mvuto wa kimataifa linashughulikiwa kwa uangalifu mkubwa na baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani, huku kila mmoja akijua makosa yanayomkabili.


  “Kwa sasa bado ni mapema kuzungumzia zaidi jambo hilo, kwa sababu uchunguzi wa sakata hilo unaendelea vizuri. Tuna kundi kubwa la wapelelezi ambao wanafanya kazi kwa umakini zaidi na kwa muda mfupi kwa ajili ya kutengeneza mashitaka yatakayowakilishwa mahakamani dhidi ya watuhumiwa hao,” alisema Kova.


  Katika hatua nyingine, upakuaji wa samaki zaidi ya tani 70 waliokutwa katika meli hiyo uliendelea. Samaki hao wakihifadhiwa katika kiwanda cha Vick Fish kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam na maafisa wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi walionekana wakichunguza samaki hao mara kwa mara kiwandani hapo.


  Upakuaji wa samaki hao aina ya Jodari (Tuna) na Sord (Nduaro), unatarajiwa kukamilika leo.


  Kwa mujibu wa Waziri wa wizara hiyo, John Magufuli mmiliki wa meli hiyo atashitakiwa kwa sheria za kimataifa kwa kuwa imekiuka sheria za kimataifa na adhabu yake ya chini ni kulipa dola bilioni 20 ama kutaifishwa meli yake ama vyote kwa pamoja.


  Meli hiyo ilikamatwa hivi karibuni ikiwa katika Bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania, haikuwa na bendera ya kuonyesha nchi ilikokuwa ikitoka, vibali vya uvuvi na hata vibali vya kufanyia shughuli hiyo katika Bahari ya Hindi na ilifikishwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ukaguzi zaidi.


  Kukamatwa kwa meli hiyo kunatokana na juhudi za serikali kukamata maharamia wa samaki katika Bahari ya Hindi. Ili kufanikisha azma hiyo, serikali ilikodisha meli maalumu kwa kazi hiyo kutoka Afrika Kusini na kushirikisha wanamaji wa Tanzania, Afrika Kusini na Msumbiji ambao walifanikiwa kuinasa meli hiyo ikivua samaki ndani ya eneo la bahari la Tanzania karibu na mpaka wa visiwa vya Mauritius.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Inaelekea hii meli ilikuwa inavua na kupeleka mali hii china.
  Kwa sababu walitujengea uwanja, mi nawambia mtasikia tu kuwa sirikali imeamua kuwaachia waende. Subirini mtaona wenyewe. Hii ni nchi ya wacheza sinema:)
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo wafuasi wa Sultani CCM lazima watapigania kuwa mashahidi ,dola bilioni ishirini yaani wafuasi wakikatiwa dau la Milioni 10 tu mtasikia kimya ,ndio imetoka hiyo. :D
  Kila mmoja amekuwa kiranja kumbe kuna ulaji .Ni ulaji tu hapo akuna lingine naamini mwenye meli kishazungumza nao sasa uone uchunguzi utakavyokuwa mrefu.
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Dollar BILIONI 20? That cant be correct.
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,173
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280

  From what I know ni TZS 20 Billion, ................. $ 20 Billion si ni sawa na trilion kadhaa in TZS
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  UKIONGEZA NA HILO HAPO JUU,hili swala litakuwa transormed kwenye POLITICS!..........ukishaingiza siasa kwenye serious matters kama hizi YOU ARE FINISHED THEN!

  Ndio tatizo letu waswahili
   
Loading...