Wakala wa kuuza umeme wa TANESCO ya Selcom ni janga la taifa kwa watanzania wajasiriamali

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Selcom iliyoingia mkataba wa kusaidia kuuza token za umeme kuisaidia TANESCO; lakini cha kushangaza hili kampuni kupitia huduma ya kuuza umeme limekuwa na ukajanja mwingi.

1. Ikifika mwisho wa mwezi wanachezesha mtandao saa za jioni ukiuza umeme. Inakuambia huduma inamatatizo lakini cha kushangaza pesa wanakata. Anayeathirika ni muuzaji wa Selcom, mteja anaondoka na pesa yake wakati wewe wamekata mtaji . Ukienda kudai wanakuambia peleka barua TANESCO - mzunguko wa TANESCO kwa umeme wa 2000. Unaacha pesa zinapotea , wateja wengi ni wa shilingi 1000-5000.

2. Mwezi uliopita tarehe 19-20. Wateja waliohudumia walikatwa pesa lakini hakuna mesegi yoyote kuwa mtandao ulikuwa unamatataizo . Ukienda kuwadai wanakuomba mita no uliyohudumia na meseji ; ukiwaambia meseji hawakutuma, unaonekana mkorofi na hawapokei simu; hatujui katika mkataba hakuna kipengele cha customer support.

3. Ukiwa na tatizo simu hawapokei mpaka uje ofisi mjini ni longo longo kibao unapewa na wahindi .

4. Machine mbovu hatujui TBS hawakagui kitengo cha electronics au wanjua kukagua vipodozi tu . Na sio electronic equipment.

5. Mimi niliongezatoken bei ya umeme baada ya 20,000. Nikaandika 200,000. Ni miezi 5 sijapewa pesa yangu mpaka sasa. Nimereport tatizo . Walinipa barua nipeleke TANESCO ; wakiniahidi watanilipa. Ukienda wanakuambia tanesco hawajawajibu niesabu hasara.

5. Sijui kampuni in ya kuuza vifaa au kuuza huduma za umeme

images

''Selcom offers a wide range of technical multiaxial fabrics products designed to meet the various needs of our clients in any field of application. Selcom.

Selcom group | we are innovative. Inside.''

Hili ni janga la taifa uongozi huu wa awamu ya tano

Ndimi
Muathirika
 
Ujanja ujanja tu.
Sijui tumuamini nani maana kila mtu kigeugeu ~Jaguar
 
Mkuu hawa jamaa ni JANGA, huduma kwa wateja wako watatu tu sasa sijui wana handle wateja kivipi ambao kwa wanaotumia mshine tu ni zaidi ya 18,000 tanzania nzima, hii kampuni ya kihindi wanatakiwa kuboresha kitengo chao cha huduma kwa wateja..kwa kweli ni wachache sana nilishafika ofisini kwao ni kachumba tu ndo unaambiwa hapa ndio makao makuu ya huduma kwa wateja.
 
Tatizo Tanesco wamelala maofisini laiti kama wangekuwa na dirisha dogo ofisi za selcom; sijui kama matatizo yangejitokeza
waige NHIF kila hospital kuu na kubwa wanadirisha dogo. Nilitegemea wangeweka makao makuu ya selcom kitengo chao cha IT na Customer care.

au wanabariki wizi huu na ubabaishaji huuu. Nchi hii wahindi wataacha kutuchezea lini.

Kwanini wasiwe TANESCO na machine zao : Mbona TRA wanzao na watu nanalipia ???????????
 
Hao selcom wanacheza na hela za wateja weekends wanazizungusha kwenye short time loans wahindi wajanja sana hao
 
Kumbe povu lote ni kwamba ulikosea kununua umeme wa 200,000 badala ya 20,000 hapo inabidi uwe mpole tu,kama usingekosea na umeme hukupata unastahili kulaumu, na jambo lingine ikumbukwe huu mfumo ulitengenezwa wakati wateja wakiwa wachache na hawakuwa na utaaratibu wa kununua umeme kwa njia hiyo,kwa sasa wanatakiwa wa Upgrade mfumo
 
baadhi ya mifano asilia.
Mapovu tunayomengi si haya......... wakibeep tunawapigia kama Gwajima
 
Kumbe povu lote ni kwamba ulikosea kununua umeme wa 200,000 badala ya 20,000 hapo inabidi uwe mpole tu,kama usingekosea na umeme hukupata unastahili kulaumu, na jambo lingine ikumbukwe huu mfumo ulitengenezwa wakati wateja wakiwa wachache na hawakuwa na utaaratibu wa kununua umeme kwa njia hiyo,kwa sasa wanatakiwa wa Upgrade mfumo
Kwahiyo mzee umeona neno laki mbili tu? Haujaona alivyoonesha urasimu uliokuwepo wa kurudishiwa haki yake?
Au hao wadau wa juu hapo walioonesha matatizo mengine ya selcom?

Vyote hivyo haujaona?
 
Kuwa mjasiliamali km serikali inavyodai ; Serikali inaiachia sekta binafsi ikupige tu
 
Kumbe povu lote ni kwamba ulikosea kununua umeme wa 200,000 badala ya 20,000 hapo inabidi uwe mpole tu,kama usingekosea na umeme hukupata unastahili kulaumu, na jambo lingine ikumbukwe huu mfumo ulitengenezwa wakati wateja wakiwa wachache na hawakuwa na utaaratibu wa kununua umeme kwa njia hiyo,kwa sasa wanatakiwa wa Upgrade mfumo
Wewe jamaa ni hasara kwa familia yako..... Kama walitengeneza program kwa ajili YA watu wachache kwa nn walizalisha machine nyingi zaidi YA uwezo Wao.... Alafu jamaa amesema awana customer care call centre Wewe unakuja kuongea crappppp hapa..... Wewe Bado Sana upo stone Age.....wewe kubali Selcom ni janga nilinunua vocha kuweka ikanigomea nilitafuta ofisi za jamaa nilipofika no mwendo wa sound tu.... Muhindi ukishampa pesa akujui Ila wakat wa kukushawish umpe pesa hata magoti hatakupigia
 
Mkuu kuna biashara ili uifanye inatakiwa mshirikiane na unaeshirikiana nae kutoa huduma selcom wanaonekana hawako kibiashara japo wako kwenye soko la biashara

Mi huwa kufanya kazi na kampuni za kibabaishaji siwezi huwa narudisha garama zangu naanzisha biashara nyingine ili kulinda thamani ya pesa yangu

Kama utaweza tafuta mteja muuzie hiyo mashine pesa yako ipeleke katika biashara nyingine

Unaweza ukafungua
M-pesa eartel money Tigo pesa na bado ukaifanya hiyo Huduma ya kuwanunulia watu umeme
 
Mkuu acha kabisa hawa jamaa wamezidiwa uwezo wa kuhudumia wateja kabisa hawana msaada kabisa na pindi unapokabiliwa na tatizo kuwa pata kwa njia ya simu ni JANGA, sielewe taasisi husika wanaichukulia vipi hii kampuni..
 
Mkuu kwenye simu hii ndo imewafanya waonekane wanahuduma mbovu zaidi maana inapo tokea dharula unakosa msaada ila kama unaweza toa pesa yako yote iingize katika biashara nyingine ukiona wameboresha Huduma ndo uendelee nao
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Mkuu kuna biashara ili uifanye inatakiwa mshirikiane na unaeshirikiana nae kutoa huduma selcom wanaonekana hawako kibiashara japo wako kwenye soko la biashara

Mi huwa kufanya kazi na kampuni za kibabaishaji siwezi huwa narudisha garama zangu naanzisha biashara nyingine ili kulinda thamani ya pesa yangu

Kama utaweza tafuta mteja muuzie hiyo mashine pesa yako ipeleke katika biashara nyingine

Unaweza ukafungua
M-pesa eartel money Tigo pesa na bado ukaifanya hiyo Huduma ya kuwanunulia watu umeme
tatizo ni risti ya vat; wanataka hardcopy risti mfano wapangaji ili wajue km umenunuliwa
 
Kumbe povu lote ni kwamba ulikosea kununua umeme wa 200,000 badala ya 20,000 hapo inabidi uwe mpole tu,kama usingekosea na umeme hukupata unastahili kulaumu, na jambo lingine ikumbukwe huu mfumo ulitengenezwa wakati wateja wakiwa wachache na hawakuwa na utaaratibu wa kununua umeme kwa njia hiyo,kwa sasa wanatakiwa wa Upgrade mfumo
Hujui unalolisema rofa ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom