Wakaguzi wa mashule wabadili mbinu

Prispian

Member
Jan 22, 2017
33
39
Hakuna haja kuendelea kukagua maandalio pekee bali wapewe japo dakika hata 20 wafundishe darasani ili kuona pia nature ya wanafunzi walioko mashuleni.

Kama wakiendelea kukagua tu maandalio wataishia kuandika clean certificate kwa shule mwishowe wanafunzi wanafeli na walimu kuishia kufukuzwa ama kuhamishwa au wakuu kushushwa vyeo.

Madiwani na maafisa watendaji pia waelimishe wananchi wao kuhusu ushiriki wao juu ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao kielimu badala ya kuendelea kushambulia walimu.

Jamii inapaswa kuwa makini na hili la elimu kwanza badala ya kuendelea na mambo ya ushabiki usio na tija.
 
Hakuna haja kuendelea kukagua maandalio pekee bali wapewe japo dakika hata 20 wafundishe darasani ili kuona pia nature ya wanafunzi walioko mashuleni. Kama wakiendelea kukagua tu maandalio wataishia kuandika clean certificate kwa shule mwishowe wanafunzi wanafeli na walimu kuishia kufukuzwa ama kuhamishwa au wakuu kushushwa vyeo. Madiwani na maafisa watendaji pia waelimishe wananchi wao kuhusu ushiriki wao juu ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao kielimu badala ya kuendelea kushambulia walimu. Jamii inapaswa kuwa makini na hili la elimu kwanza badala ya kuendelea na mambo ya ushabiki usio na tija.

Watakaguaje shule yenye walimu 3 au 4 toka darasa la I - VII. Wamwambie baba yao kuwa apeleke walimu shuleni kwanza ndipo tuone uzembe ni wa nani.

Hali vijijini ni mbaya. Shule hazina walimu lkn ukaguzi kila leo.Nani atafundisha? Kwao mwalimu asiye na andalio ndo nongwa hata kama anafundisha kikamilifu.

Wanachofanyiwa ni kupewa maandalio na maazimio 100% lkn ufundishaji ni 10%. Halafu ni wala rushwa hawa, wachunguzwe.
 
Halafu lesson plan hata haisaidii chochote wakat wa kufundisha. Ni kusumbuana tu kuandika ila sio kwamba eti ukiandika lesson plan watafaulu, wala tu.
Wamekariri badala ya ubunifu. Yangu nazaliwa nasikia andalio na azimio. Lkn matatizo ni palepale.
 
Pole sisi wananchi maana watoto wetu au wadogo zetu ndo wanaumia huko. Sio kila mtu anaeandika kuhusu siasa ni mwanasiasa, sio pia kila aandikae kuhusu elimu ni mwl.
Pole Mwl Mwanasiasa.
 
Mimi ni mwalimu na napenda sana kusomea ukaguzi japo kwa sasa wamebadili jina na kuita "Udhibiti ubora wa elimu" nisaidieni kujua sifa za kujiunga na chuo na fursa za kutoka zaidi ya ualimu nilionao@
 
Mimi ni mwalimu na napenda sana kusomea ukaguzi japo kwa sasa wamebadili jina na kuita "Udhibiti ubora wa elimu" nisaidieni kujua sifa za kujiunga na chuo na fursa za kutoka zaidi ya ualimu nilionao@
Zamani hakukuwa na chuo zenye hiyo kozi ila kwa sasa nenda pale bagamoyo chuo cha Adem!zipo hizo course!
 
Watakaguaje shule yenye walimu 3 au 4 toka darasa la I - VII. Wamwambie baba yao kuwa apeleke walimu shuleni kwanza ndipo tuone uzembe ni wa nani.

Hali vijijini ni mbaya. Shule hazina walimu lkn ukaguzi kila leo.Nani atafundisha? Kwao mwalimu asiye na andalio ndo nongwa hata kama anafundisha kikamilifu.

Wanachofanyiwa ni kupewa maandalio na maazimio 100% lkn ufundishaji ni 10%. Halafu ni wala rushwa hawa, wachunguzwe.
nilishawahi kuwaambia ofisini kitu ya namna hii wakaniona mbwiga
 
Mimi ni mwalimu na napenda sana kusomea ukaguzi japo kwa sasa wamebadili jina na kuita "Udhibiti ubora wa elimu" nisaidieni kujua sifa za kujiunga na chuo na fursa za kutoka zaidi ya ualimu nilionao@
Kuwa mnoko
 
Hivi ni akina Nani wenye jukumu la kukagua usafi wa mazingira ya shuleni? Kwa mfano uzoefu unaonesha Shule nyingi zina matatizo ya kutokuwa na vyoo vyenye kufaa Kwa matumizi ya kibinadamu Kabisa ! Hii ni Kwa maeneo ya mjini hadi vijijini! Vyoo vyoo jamani , vyooni hakuna Maji imagine vyoo vya mashimo vimetitia au kubomoka yaani mmm...
 
Ukienda mahospitalini halikadhalika vyoo Vichafu Maji hakuna Mtu aweza kwenda mzima akarudi mgonjwa
 
Mimi ni mwalimu na napenda sana kusomea ukaguzi japo kwa sasa wamebadili jina na kuita "Udhibiti ubora wa elimu" nisaidieni kujua sifa za kujiunga na chuo na fursa za kutoka zaidi ya ualimu nilionao@
nipm nikupe muongozo wa kupata nafasi ya kusoma hiyo koz.nipo adem-bagamoyo.
 
Back
Top Bottom