Waka’ ya Diamond Platnumz yaweka rekodi mpya Afrika Mashariki

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
3,334
2,000
Wakati wimbo mpya wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Rapper Rick Ross kutoka Marekani unatoka haukuwa na nguvu kubwa pengine kutokana na kuahirishwa kwa tarehe iliyotakiwa kutoka video ya wimbo.


Lakini hiyo haikuwa kigezo kikubwa kwa wimbo huo wa ‘Waka’ kwani ndani ya siku tatu ulikuwa tayari umefikisha views milioni 1.

Ukweli ni kwamba ‘Waka’ ulipata mapokezi ya kawaida ukilinganisha na nyimbo nyingine za Diamond Platnumz kama Hallelujah, Salome, Kidogo n.k , Lakini kitu cha kushangaza wimbo huo kadri siku zinavyozidi kwenda ndio unazidi kutazamwa zaidi sio tu Tanzania bali na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kwa sasa wimbo wa ‘Waka’ unaweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza kutrend namba moja kwa nchi tatu za Afrika Mashariki kwenye mtandao wa YouTube.

Video hiyo mpaka jana usiku ilikuwa ndiyo video inayotazamwa zaidi mtandaoni (Trending) kwa kushika namba moja kwa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.


Wimbo wa ‘Waka’ awali ulipotoka ulikaa siku mbili kwenye mtandao wa YouTube hapa Tanzania bila kukaa kwenye namba 1 ya video zinazotrend hapa nchini. Lakini mpaka sasa video ya wimbo huo yenye siku saba mtandaoni ipo namba moja kwenye Trending.

Awali rekodi ya video iliyotrend namba 1 kwa nchi mbili tofauti tofauti ilikuwa ilikuwa inashikiliwa na video ya wimbo wa ‘Zilipendwa’ wa WCB , Salome ya Diamond Platnumz na Video ya wimbo wa ‘Seduce Me’ wa Alikiba ambapo video zote wakati zinatoka zilishika namba moja Tanzania na Kenya kwa muda tofauti tofauti.
 

Attachments

  • Screenshot_2017-12-15-12-58-25.png
    File size
    854.6 KB
    Views
    70

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,265
2,000
Huu wimbo wa hovyo sana sema kwa kuwa yupo rick ross tu kifupi hauleweki.
 

Wissman

JF-Expert Member
Dec 12, 2014
994
1,000
Unachofurahia ni wale akinadada wanaocheza bila nguo? Unaweza ukawa upo na mzazi wako au wazee wenye heshma mkaangalia bila wasiwasi? Ujinga tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom