Mkuu kwa uelewa wangu mdogo najua suala la kuunguza account linawahusu wanaofanya mambo ya forex.
Kama ulinunua crypto currency yoyote ikawa kwenye wallet yako. Thamani ya zile crypto currency inaweza kuongezeka au kupungua kutokana na bei ya crypo hiyo ukilinganisha na USD, ila idadi ya crypto currency zako hazitapungu au kuongezeka.
Tuchukulie mfano ulinunua ethereum 1 kwa bei ya 50 USD, ikawa kwenye wallet yako. Siku ikiporomoka thamani na kufikia 10USD wewe utaendelea kua na ethereum yako moja ambayo itakua na thamani mpya ya 10 USD.