Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nimebahatika kuona nyuzi mbalimbali zikiponda simu zinazotumia chipset za
MTK na wakisifia simu zinazotumia chipset za
snapdragon au
Qualcomm
Naomba mnijuze hizi chipset zina kazi gani kwenye Android na kwanini zinatofautiana ubora?
Mkuu wadau wengi wameshadefine hio chipset (soc) labda mimi niongezee kwanini zinatofautiana,
Kabla ya kwenda huko kwanza ufahamu Arm na x86, hizi ni Architecture mbili tofauti, x86 hii ndio inatumika kwenye computer kama desktop na laptop, ukisikia i3 ama i5 ama i7 zile zinakuwa ni x86, kwenye simu zinazotumika sana ni Arm, hizi zinakuwa designed na kampuni inaitwa Arm holdings ya huko Uingereza halafu ndio makampuni kama qualcomm na mediatek wanaweka kwenye soc zao, zilivyokuwa designed hizi za arm(processor) zinakuwa na core kubwa na ndogo, core kubwa inakuwa na nguvu ila inakula zaidi chaji ya simu, na core ndogo yenyewe haina nguvu sana ila inakula chaji kidogo. pia hawa Arm wanaruhusu makampuni mengine kubadili design yao na kutengeneza custom ama semi custom chip. hivyo hapa tunapata utofauti wa aina mbili
custom design
-utumiaji wa custom chip sasa hivi tumebakiwa na makampuni matatu Apple na A series zake, Nvidia na Tegra zake pamoja na Samsung na mongoose zake, ila kuna habari kwamba samsung anajitoa hivyo huwenda wakabaki wawili tu. qualcomm wenyewe wanatumia semi custom, na kampuni kama mediatek hawafanyi modification. ila ikumbukwe kitu kimoja chipset za bei rahisi huwa hawamodify kabisa mfano exynos iliopo kwenye galaxy A10 core zake hazijakuwa modified kama mongoose inatumia tu core za kawaida kama mediatek ama qualcomm za bei rahisi.
core zilizotumika
kama juu tulivyosema utofauti mwengine ni hizo core kuna core kubwa na ndogo (big little), makampuni yote yanazitumia, mfano wa core kubwa ni kama cortex A73/A72/A75/A76 na mfano wa core ndogo ni A7/A53/A55. tuangalie mfano wa mpangilio wa core kwenye Note 10
Octa-core (2x2.73 GHz Mongoose M4 & 2x2.4 GHz Cortex-A75 & 4x1.9 GHz Cortex-A55)
then tuangalie na simu low end kama tecno spark
Quad-core 1.3 GHz Cortex-A7
hivyo unaona hapo kwenye note 10 kuna cluster kama tatu hivi moja ni custom core za mongoose, mbili core kubwa za cortex A75 na tatu core ndogo za cortex A55, ila kwenye hio spark kuna core ndogo tu za cortex A57 basi vitu kama hivi vinatofautisha chipset.
mambo mengine yanayoweza kutofautisha ni kama,
manufacturing process
kampuni kama qualcomm, Apple ama mediatek wakimaliza kudesign hizo chipset zao kuna mahala wanapeleka zinaenda kutengenezwa kwa wingi, chukulia mfano wa mchoraji na mmiliki wa printer, mchoraji akimaliza kuchora anapeleka kwa mwenye printer/photocopy machine akatoe picha nyingi zaidi. makampuni makubwa yanayofanya hizi manufacturing ni Intel, samsung na TSMC (taiwan semiconductor), na kila kampuni inaupgrade mitambo yake kufanya manufacturing za kisasa zaidi, kitu kikubwa zaidi kinachowatenganisha ni udogo wa transistor ambao hupimwa kwa nanometre (nm), jinsi transistor inavyokuwa ndogo inamaana kwenye die moja unaweza kuweka transistor nyingi zaidi na kuongeza perfomance, pamoja na kupunguza ulaji umeme. manufacturing process ya kisasa sasa hivi ni 7nm, ipo pia ya 8nm, 10nm, 12nm, 14nm etc hivyo unaweza hapa pia kuzitofautisha.
gpu
vitu kama games, animation za simu ama apps mbalimbali zinatumia gpu, kuna gpu zinazotoka kwa arm wenyewe kama Mali series, kuna gpu za qualcomm kama Adreno, kuna Gpu za imagination kama powervr. hizi gpu zinakuwa responsible kurun technology kama open gl na vulkan ambazo developer wanazitumia wanapotengeza vitu kama games. hapa Qualcomm ana advantage kubwa compare na wenzake Gpu zake za adreno wanatoa drivers mbalimbali zinazofanya simu zao kuwa all around vizuri kwenye gpu, na kuna baadhi ya vitu exclusively vinakuwa developed kwa ajili ya adreno tu mfano emulator mpya ya ps2 kwenye android.
modem
pia hizi chipset zinakuwa na modem ndani inayohandle vitu kama kupiga simu na kupokea na internet tech kama 3g na 4g zinakuwa na modem, kwa modem za kisasa kwenye simu vitu kama 3g na 2g unakuwa covered kote ila kwenye 4g utofauti unaanza kuuona, kuna simu highend ama midrange zinakuwa na support karibia band zote za 4g, popote unapokwenda simu inashika 4g na hata mtandao mpya ukitoa 4g una uhakika wa kuwa covered, mfano mzuri halotel wametoa 4g ndugu zetu wengi wanaotumia simu za kichina ama simu low end hawapati hii 4g kutokana na modem za simu zao.
pia kuna mambo mengine kama wifi, bluetooth, ram technologies, memory bus etc vyote vinachangia kwenye kutofautisha hizo soc.
ila jambo la muhimu zaidi usiangalie tu jina snapdragon, exynos ama mediatek, inaweza ikawa snapdragon lakini ikawa low end sana na ikapitwa na mediatek vile vile, cha muhimu angalia tech husika iliotengeneza hio soc ili kufanya uamuzi sahihi, tumia website kama notebookcheck ama anandtech kupata deep reviews za soc mbalimbali.