PreGE2025 Wajumbe CCM wamchangia Manunga zaidi ya shillingi laki 5 kuchukua fomu ya kuwania ubunge Chato kaskazini

PreGE2025 Wajumbe CCM wamchangia Manunga zaidi ya shillingi laki 5 kuchukua fomu ya kuwania ubunge Chato kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita Mhe. Batholomeo Manunga ametangaza nia ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Chato Kaskazini.

Mhe. Manunga ametangaza nia yake hiyo jana Juni 16, 2025 katika kikao Cha kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kata ya Bwongera kwa kipindi cha Miaka minne kuanzia 2021 hadi 2025.

Taarifa ya Utekelezaji wa maendeleo imewasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kata ya Bwongera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Mhe. Manunga ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo ya Bwongera, pamoja na kutangaza nia yake hiyo, Wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM kata, wameonesha kufurahishwa na nia yake hiyo na kuamua kumchangia fedha za kuchukua fomu ya ubunge zaidi ya Shilingi laki 5.




 
Back
Top Bottom