Chato waomba serikali irejeshe safari za ndege

Chato waomba serikali irejeshe safari za ndege

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,552
Reaction score
139,887
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, Batholomeo Manunga, ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kurejesha safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Chato ambazo zimesitishwa tangu Novemba 2024 bila kutolewa sababu rasmi.

Akizungumza na Manara TV, Manunga amesema kuwa kusitishwa kwa safari hizo kumeathiri si tu wakazi wa Chato, bali pia mkoa mzima wa Geita na wasafiri kutoka nchi jirani kama Rwanda na Uganda waliokuwa wakitumia uwanja huo kwa shughuli mbalimbali.

“Kusitishwa kwa safari hizi kumeathiri sana uchumi wa wananchi wa Geita na maeneo ya jirani. Wasafiri walishazoea kutumia ndege kufanikisha shughuli zao za kijamii na kiuchumi,” amesema Manunga.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa tayari ameshafanya jitihada binafsi kwa kukutana na Waziri wa Uchukuzi ili kujadili suala hilo. “Waziri aliniahidi kuwa safari za ndege zingerejeshwa mwezi Machi mwaka huu 2025, lakini hadi leo hatujaona utekelezaji wake,” amesema.

Hata hivyo, amesema kuwa baada ya kuona ahadi hiyo haijatimizwa, aliamua kukutana tena na Waziri huyo hivi karibuni, ambapo aliahidi kwa mara nyingine kuwa safari za ndege zitarejea mwezi Julai mwaka huu.

Manunga amesisitiza kuwa yeye binafsi ni mdau mkubwa wa usafiri wa anga kwa kuwa hutumia ndege kwa shughuli zake mbalimbali za kibiashara, na kuongeza kuwa rekodi za safari zake zilizopita zinaweza kuthibitisha mchango wake katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, kurejeshwa kwa safari hizo kutasaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kuongeza ajira na kuinua sekta ya utalii katika Wilaya ya Chato na mkoa wa Geita kwa ujumla.
 
Kile kiwanja bora kinge kuwa chuo cha urubani
 
Sababu kubwa ilikuwa ni kutokua na wasafiri wa kutosha,lakini tusisahau kuwa wakati tunanunua ndege zetu hatukuwa na uhkika wa kujaza ndege zetu,lakini sasa zinajaa mpaka nafasi zinakosekana,kwahiyo hata sasa ziklirudi tena kule Chato watu wakishajua kuna connection ya ndege pale ndani ya muda mfupi tunaweza kushuhudia ongezeko kubwa tu la abiria....
 
Sababu kubwa ilikuwa ni kutokua na wasafiri wa kutosha,lakini tusisahau kuwa wakati tunanunua ndege zetu hatukuwa na uhkika wa kujaza ndege zetu,lakini sasa zinajaa mpaka nafasi zinakosekana,kwahiyo hata sasa ziklirudi tena kule Chato watu wakishajua kuna connection ya ndege pale ndani ya muda mfupi tunaweza kushuhudia ongezeko kubwa tu la abiria....
Kipindi kile wasafiri wa huko walikuwa wengi sababu ya mzee, sasa hayupo and no body cares

Laki pia kiuchumi na mzunguko wa pesa upo? Maana mtu hachomi nauli kuja chato kushangaa shangaaa
Unless kama ni kusalimia
 
Yaani kati ya upuuzi uliofanywa ni kusitisha safari za ndege za chato. Watu wa Ngara, chato na sehemu zingine za karibu wameathirika na hili jambo. Cha ajabu ndege zenyewe ni zile zinazoenda mwanza. Route ni Dar-chato-mwanza-Dar. Wamefanya unyanyasaji sana.
 
Sa hivi uwanja wa ndege unatumika kuanika michembe na mbute, henee gete 😢
 
Back
Top Bottom