Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 579
WAJUE WACHAWI WA RAIS SAMIA.
Kwangu Mimi naamini UCHAWI upo duniani kama ambavyo Mwenyezi Mungu amedhihirisha upo kupitia vitabu vyake vya Bibilia na Qur'an. Kidunia vile vile mimi nautafsiri Uchawi kama Sanaa (An Art) na pia ni Sayansi (A Science), ambayo kama ingelitumika vema; Familia, Nchi, Mabara na Dunia nzima tungekuwa na mafanikio makubwa zaidi ya sasa katika nyanja zote za kimaisha iwe Kisiasa, Kiuchumi, Sayansi na Teknolojia, Kiutamaduni na hata Kijamii.
Ila nadhani changamoto na makwazo makuu yatokanayo ama yadhaniwayo juu ya Sanaa na Sayansi hii ya UCHAWI ni namna ambavyo WANATAALUMA wa Kitengo hiki wanavyoutumia hasi UJUZI wao dhidi ya Mafanikio ya wengine- na hapa ndipo MADA yangu inapoegemea.
Rais Samia wa Tanzania kwa nyakati tofauti tangu aapishwe Ijumaa Machi 19, 2021 Ikulu Chamwino jijini Dodoma na kipekee alipolihutubia Bunge kama Rais kwa mara ya kwanza Aprili 22, 2021 Dodoma ameendelea kuviweka wazi VIPAUMBELE vyake VINAVYOAKISI KILA HITAJI MUHIMU LA MTANZANIA.
Kama Rais anayeziongoza nchi za Zanzibar na Tanganyika zilizoungana tangu Aprili 26, 1964; Ukivitafakari kwa kina VIPAUMBELE vyake Mama Samia utagundua Sasa tuna Rais ambaye hakika hajaacha eneo lolote linalolipa RAHA na FURAHA kila kundi nchini. Yaani kimombo bila kumumunya maneno tunaweza kusema; President Samia is a True Comforter-In-Chief FOR ALL.
Kama ni WAKULIMA ambao ndio zaidi ya 65% ya Watanzania wote, ambao ndio wazalishao chakula tegemewa kwa 100% kwa Watanzania wote karibia milioni 60 sasa, ambao huzalisha malighali viwandani kwa 45%.... Rais ametangaza Serikali yake ya Awamu ya Sita itawahakikishia Wakulima Mbegu na dawa za kisasa, Kilimo cha Umwagiliaji badala ya kutegemea Mvua na kikubwa zaidi Masoko ya uhakika ndani na nje n.k ; yaani hapa vile viazi na Alzeti za SINGIDA, Korosho za Mtwara, Samaki kutoka ukanda wa Maziwa na Bahari ya Hindi na hata mazao ya mifugo kutoka Umasaini na Usukumani tutauza 'kiuhakika' humu ndani na nje ya nchi badala ya sasa kuozeana, kudoda au kuuzwa kwa bei ya hasara ukilinganisha na gharama za uzalishaji.
Hapa kama ATAKUWA Mchawi wa Wakulima kama Sio Wasaidizi wake ambao ndio watekelezaji (Wasaidizi) wake kuanzia Wizara ya Kilimo ni nani?
WATUMISHI WA UMMA Mchawi wao mkuu ATAKUWA nani kama sio Wasaidizi wa Rais? Kama Mhe. Rais Samia ameshatangaza haoni tija WATUMISHI wote wa umma kufanya kazi bila kutekelezewa maslahi yao muhimu ikiwemo Kupandishwa madaraja na mishahara? Katika hotuba yake ya kwanza Aprili 2020 Bungeni Mama Samia alisisitiza hili kwa umakini kabisa... Kama ni mkwamishaji mkuu wa kipaumbele hiki basi ataanza na TAMISEMI ya sasa ya Odo, Waziri, Ummy Mwalimu.
Mataifa yote duniani hutegemea WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI kukuza Chumi zao na wananchi wao. Rais wetu Samia kama ni kipaumbele chake cha kwanza kukitangaza pale tu alipoingia Ikulu Machi 19 mwaka huu basi ni agizo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Kaka yangu, Dkt Mwigulu Nchemba, TRA na Wizara na Mamlaka zingine zinazohusiana na eneo hili Kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya biashara na Uwekezaji huku Kodi kandamizi na za dhuluma kufika kikomo. Sasa hapa mjue kama Wachawi wakuu wa Wafanyabiashara na Wawekezaji ni akina nani...
Kwenye anga la Kimataifa; kwa muda sasa salam zetu ni ubaya ubayani tu; Ila Rais Samia ametangaza kwamba nchi yetu si kisiwa, ili tufike pahala panapotustahili lazima TUHUSIANE NA TUSHIRIKIANE VEMA na Nchi zingine za Kikanda, Bara la Afrika na Dunia. Utayari huu kama Mchawi Mkuu wa kuudumaza basi ataanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye kwa sasa ni Mama Mulamula.
April 26, kila mwaka huwa tunasherekea Muungano wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia alishasema kwa umakini kabisa anataka Awamu yake kuona Muungano unazidi kuwa na tija kwa pande zote mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Akiwa Ikulu ameonesha kwa vitendo kwamba anamaanisha hili; tumeona hata katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC ambao alipaswa aende yeye, amemtuma Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi, kitendo ambacho KIHISTORIA hatujawahi kukishuhudia. Makamu wa Rais Samia, Dkt Mpango na Waziri wa Muungano na Mazingira Ndugu Jafo kama ni Wachawi wakuu wa kumwangusha Rais kwenye kipaumbele hiki basi wataanza kuwa wao.
Rais Samia ametangaza anataka HAKI kila pahala itamalaki. Hataki raia wake aonewe. Anataka kila Wizara itende haki. Kila msaidizi wake awe furaha ya anaowaongoza. Kama ni kesi basi zile za hovyo Serikali yake isizipeleke Mahakamani kuepuka fedheha na matumizi yasiyokuwa na lazima. Hataki watu walundikwe magerezani bila sababu. Kama ni DEMOKRASIA ametangaza utayari wa kukutana na vyama vya Siasa, kama Uhuru wa Vyombo vya Habari ametangaza vyombo vilivyofungwa kuachiwa huru..
Jamaan hapa kama watakwepo Wachawi wakuu wa HAKI bila shaka tutaanza na Mahakama, Vyombo vya Dola, Wizara Husika ikiwemo ya Sheria Chini ya Prof Kabudi na ile ya Habari chini ya Bashungwa....au sio?
Kwenye HUDUMA ZA JAMII akina nani watakuwa Wachawi wakuu hapa, Kama sio Wasaidizi wa Rais? Maana kama ni Maji, Rais Bungeni juzi amesema kwa msisitizo Mkuu kwamba hataki hadi ifikapo mwaka 2025 kuona Kijiji au mtaa una tabu ya Maji na hata akamwambia Waziri wa Maji Ndugu Axweso "akimzingua naye atamzingua"... Kama ni afya amesema hataki Mama wajawazito wala Watoto wao wanakufa wakati wa kujifungua, hataki hadi 2025 kiwepo Kijiji Tanzania hakina Umeme kama ilivyoelekezwa na Chama Tawala kupitia Ilani yake ya Mwaka 2020/2025... Hivi hapa bado Rais Samia atakuwa Mchawi wa HUDUMA mbovu za Jamii? Jibu mnalo.
Kwa leo niishie kutaja hivi VIPAUMBELE vichache vikuu kutoka kwa Rais wetu vinavyotugusa wote. Naamini Sasa mtakuwa mnawajua Wachawi wakuu wa Safari njema ya Rais kwamba KAMA WATAKWEPO basi wataanza kuwa WASAIDIZI WAKE, MAHAKAMA, BUNGE NA SISI WANANCHI.
Rais Samia ameonesha kila aina ya nia njema na Matumaini Makuu kwa sisi SOTE kilichobaki Sasa ni SISI SOTE kwa PAMOJA KUSHIRIKIANA naye kuifanya Tanzania kuwa Sehemu Bora zaidi ya kuishi kwa wote na kila binadam duniani.
Mungu mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania na
Mungu Wabariki Watanzania.
Suphian Juma,
Singida, Tanzania.
Aprili 27, 2021.