Wajue wabunge VIHIYO wa CCM...

mnataka kusema mpaka naibu waziri wa fedha ni kihiyo???
 
si afadhali ya hawa chadema walitaka kutuletea makamu wa rais wa darasa la saba sasa wanaweza kuwakosoa ccm kweli? Angekua anaenda nje ya nchi na mkalimani kama marehemu kawawa? Au angeongeaje na mabalozi wakimtembelea?

wewe mwehu, acha akili za matope, hapa tunazungumzia elimu na uwezo wa ku analyze mambo na si kuongea kiingereza..kuna warasta kibao ferry hawajaenda hata darasa moja na uwezo wao wa kufafanua mambo ni mdogo mno ila wanaongea lunga kadhaa za kimataifa, so huitaji kwenda shule ili kujua kiingereza..acha kukariri..sijui umetokea kijiji gani wewe unayedhani kuongea lugha ndo elimu..mwanangu ana miaka mitano, hajaanza hata shule na anavunja yai...be critical na uache wehu!!
 
actually kihiyo ni mtu anayefoji cheti, hawa mpaka sasa tuhuma zao ni kwamba wana elimu ndogo, kwa hiyo sifa ya ukihiyo hawana, watafutie jina lingine.

hii definition ya kihiyo umeitoa wapi hii??
 

hapo ndo huwa mnakosea kuifananisha Tanzania siji na UK au Marekani, nyie watu hizi ni nchi mbili tofauti kabisa, kwa system za uchaguzi na uongozi za wenzetu unahitaji tuu sifa fulani kuweza kuongoza, lakini hiyo si kwa nchi masikini zinazotafuta kuendelea kama Tanzania..hizo quotes zako za biblia ngoja niziache kwanza, ila kwa kuwa wasomi wachache hawajaperform then you can not jenerolaizi na kusema hatuhitaji elimu,...mnapotoka.tunataka watu walobukua watuongoze..si mnaona mkwere wenu anavojichechetua na kiphd cha heshima, hizo nyerere, mkapa, mandela n.k walikuwa nazo za kutosha, ila ulishasikia wanajiita sijui Dr. mandela, dr. nyerere na kadhalika? kwa sababu walijua maana yake ni nini..mkwere anaona siiifa..kaa darasani, bukua, pata maarifa, elimika na uwe na uchungu na nchi then njoo tuongoze..sawa!!?
 
Kama asilimia 16.7% ya Wabunge ni darasa la saba na form IV basi hii ni nchi ya ajabu kweli kweli. Ndio maana walikuwa wakiambiwa elimu compulsory itakuwa form IV walibisha . Umaskini mtupu. Agrrrrr.
 

Nilimsikia mtu anasema alikuwa rais UDSM, sina history yake lakini but its good to know. Wadau hivi ni kweli Mnyika hana degree?
 
Last edited by a moderator:
WAJUE WABUNGE WALIO NA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI, hawa hapa,!!!!!




1. Jeremiah Solomon Sumari Nne/ IV Arumeru Mashariki, Arusha

Jamani na huyu si Naibu Waziri wa wizara nyeti kabisa ya Fedha? Then form IV? dah. MATATIZO
 
Halafu hiyo headingi yako, "vihiyo....."
Unaelewa ni watanzania wangapi wenye elimu ya msingi na sekondari?? Kwa hiyo kwa mwono wako 80% ya Wa Tz ni vihiyo??
wacha kutukana Watanzania ndugu

ukiwa unapinga uwe unato hoja yenye uzito na sio kupinga..
hivi wakiwa wanaongelea mambo ya uchumio au kukuza elimu iwe bora, unafikiri hao walio na elimu ya chini wanaweza kuchangia hoja???
mana hawajapata changamoto katika elimu za mbele zaidi.. Pia ndo hao hao wanaounga mkono wanachuo wapewe mkopo tena kwa %..
fikiri kabla ya kuchangia mdau mwenzangu

tafakari chukua hatua... HAKI ELIMUUUUUU
 
Vihiyo siku zote watetea vihiyo kumbuka Mwl. Nyerere alijua nini maana ya elimu kwa maendeleo ya nchi ndiyo sababu alipigania sana wananchi wake angalau wajue kusoma na kuandika, bunge ni chombo muhimu sana kwa maendeleo ya taifa kumbuka wabunge hawa ndiyo watakaopitia bajeti najaribu kufikiria jinsi mh. Ngonyani atavyochangia mapungufu na maongezeko ya bajeti athari za vihiyo hazitaathiri majimbo yao tu bali nchi nzima, tusikatae ukweli viwango vya elimu ni muhimu sana kwa wabunge. Kina Chenge walipitisha mikataba mingi mibovu kwani wanajua udhaifu wa wabunge wetu kielimu, hawana wanachoelewa.
 


Hao wenye nyekundu wote ni wahitimu wa Seminary ya Kipalapala

mmhhhh SEMINARY??

Kweli CCM yajenga nchi.

ZIDUMU FIKRA ZA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE
 

Aliipata wapi? Simba sports club? tuwekee hapa evidence
 
Nilimsikia mtu anasema alikuwa rais UDSM, sina history yake lakini but its good to know. Wadau hivi ni kweli Mnyika hana degree?
Anayo ya UDSM huyo aliyesema ana elimu ya form six tu kakosea!
 
haki elimu 'elimu ni ujuzi sio vyeti" kama madoctor na maprofessor wamechemsha kuiendesha nchi , kwanini tusirudi kwenye ujima. Waziri wa elimu ni professor lakini changanua maamuzi yake utapata jibu.
 
Na hapo je?
 
Turudi kwenye ujima mara ngapi? utendaji wa kazi wa mawaziri hufuata maelekezo ya sera za chama na si uwezo wao kitaaluma, sasa angalia hiyo sekritariati kuu ya chama ilivyojaa vihiyo na wababaishaji unategemea hawa mawaziri watafanya kitu gani?Maelekezo yote yanatoka kwa watu kama kina Makamba Kwa hizo Ph.d na masters hazisaidii chochote kwenye utendaji wao kikazi. Vihiyo tulieni ipeni nafasi elimu ifanye kazi yake. kama elimu haina maana mbona viongozi wengi wemekimbilia kuchongesha Ph.d mpaka leo hii ukiwauliza wamesomea wapi hawana majibu yanayoeleweka?
 
Mbona mgombea mwenza wa Slaa ni darasa la saba? Elimu sio ishu sana.
 
Naambiwa mwaka huu shehe yahaya nae atakuwa mbunge wa kuteuliwa na jk. Elimu madrasa.
 
Actually Kihiyo ni mtu anayefoji cheti, hawa mpaka sasa tuhuma zao ni kwamba wana elimu ndogo, kwa hiyo sifa ya uKihiyo hawana, watafutie jina lingine.
Asili ya hiyo slang ni hiyo, but immediately hilo has been used kumaanisha mtu mwenye elimu hafifu (maamuma) lakini akijikweza ktk social pyramid.
 
Kama asilimia 16.7% ya Wabunge ni darasa la saba na form IV basi hii ni nchi ya ajabu kweli kweli. Ndio maana walikuwa wakiambiwa elimu compulsory itakuwa form IV walibisha . Umaskini mtupu. Agrrrrr.

Ni form VI nafaikiri ulikuwa unamaanisha hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…